Je, ni sahihi kumshirikisha kila kitu mkeo/mpenzi wako?

ginyisi

Senior Member
Apr 6, 2023
147
261
wadau habari, naamini mko salama, nisiwachoshe sanaaaa! kama kichwa Cha habari kinavojieleza, Mimi naishi na mwanamke na nmezaa nae na tuna mpango wa kuoana hivi punde!

Sasa kumekuwa na kutokuelewana kutokana na baadhi ya vitu nafanyaga pasipo kumshirikisha nikidhani ya kuwa Haina umuhimu sanaa, kama vile kununua simu, kwenda kwenye meeting na marafiki zangu yaan yeye anataka kila kitu changu akijue jambo ambalo binafsi naona kama ananinyima uhuru kiasi flani

Naombeni maoni yenu tadadhali, nani yupo sahihi hapo!
 
Wengine umetuacha bado.
Maana,Kuna MPENZI NA MKE.

MKE ni vizuri mkashirikishana kwa Mambo mengi,endapo atakuwa muwazi na mkweli mbele yako,vivyo hivyo nawe unatakiwa kuwa vile.
Mtaishi katika maisha ya furaha.
Ila mpenzi,inakuwa ni kigugumizi,maana hamjawa kitu kimoja bado.
MKE NA MPENZI ni mtu mmoja ila katika sura tofauti kimajukumu.
 
wadau habari, naamini mko salama, nisiwachoshe sanaaaa! kama kichwa Cha habari kinavojieleza, Mimi naishi na mwanamke na nmezaa nae na tuna mpango wa kuoana hivi punde!

Sasa kumekuwa na kutokuelewana kutokana na baadhi ya vitu nafanyaga pasipo kumshirikisha nikidhani ya kuwa Haina umuhimu sanaa, kama vile kununua simu, kwenda kwenye meeting na marafiki zangu yaan yeye anataka kila kitu changu akijue jambo ambalo binafsi naona kama ananinyima uhuru kiasi flani

Naombeni maoni yenu tadadhali, nani yupo sahihi hapo!
Hayati babu yang mzee Mussa (mung amlaze mahala pema peponi), aliwahi kuniambia "Mjukuu wangu Imraan,

Mwanamke sio adui ila ishi nae kama rafiki kwa maana sio ndugu Yako ila watoto wako ndo ndugu zako.

Mshirikishe vyote ila sio kipato chako."

Sijajua alikuwa ana maana gani, ila nazidi kuyatafakar
 
Ili uweze kuishi na mwanamke lazima uwe hautabiriki yani haueleweki heleweki, ila kikubwa mjali ,mtunze na asijue kipato chako sahihi basi.

Maana wanatabia ya kutulinganisha na wanaume wengine
Au ndio maana kila sku unalalamika humu
 
Naona watu mnavyomshauri namna atakavyotengeneza familia yenye migogoro isiyoisha na atakayolazimika kuikwepa the most katika maisha yake . Kama unataka kumuoa anza kufanya practice sasa, nyie ni mwili mmoja, kuwa muwazi kujenga nyumba yenye amani na mawasiliano mazuri. Ukipata shida she is the one to provide details necessary, she is that one person ambaye anapaswa kuwa informed kuhusu out and abouts zako. Amani yake ni amani yako. Mungu akuongoze
 
Mshirikishe ni mwenzio na ukipitiwa mwambie samahani nilipitiwa kukupa taarifa usiri ni mzuri lakin kunawakat unabomoa
 
Back
Top Bottom