Je ni namna gani unaweza kuweka kumbukumbu na hesabu za biashara ndogo ili kujua mianya ya faida na hasara?

Nov 5, 2018
28
20
Samahani sana wakuuu mimi ni graduate ambaye nimekutana na changamoto hii na najua wapo wengine ambao wanaendelea kukutana na hichi kitu.

Mimi ninakakibanda kangu ka uwakala wa mitandao ya simu, m-pesa nk. Sasa nilikuwa naomba sana msaada wa jinsi Gani naweza kuwa na weka rekodi zangu vizuri na kumbukumbu ili iwe rahisi kujua hasara zinapoingia na faida maana naona biashara yangu haikui kama ninavyo taka.

Naomba msaada!

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
 
Biashara inaweza kukua pasipo kumbukumbu, mauzo ndio yataikuza biashara.

Muhimu fanya usimamizi yakinifu. Andika pesa inayoingia au inayotoka kwa muda wa mwezi mzima ata kama ni shillingi 50. Baada ya hapo utafahamu wapi kuna hasara/ matumizi ya hovyo.

Mali bila daftari uisha bila kujua
 
Wewe ni msomi gani ambaye hujui hata kuweka kumbukumbu mkuu!?yaani unataka sisi standard 7 ndio tuje tukupe somo!!? Fanya hivi mali pasipo daftari hupotea bila taarifa sisi standard 7 ndio tunatumia mfumo huu na haujawahi kufeli
 
Tafuta app inaitwa kuza business hiyo unakuwa unaweka record vizuri za stock, mauzo, matumizi pia inasaidia kujua siku gani huwa kwako ni nzuri kibishara.
 
Biashara inaweza kukua pasipo kumbukumbu, mauzo ndio yataikuza biashara.

Muhimu fanya usimamizi yakinifu. Andika pesa inayoingia au inayotoka kwa muda wa mwezi mzima ata kama ni shillingi 50. Baada ya hapo utafahamu wapi kuna hasara/ matumizi ya hovyo.

Mali bila daftari uisha bila kujua
Asante sana mkuu ngoja nifanye kazi eneo hilo
 
Wewe ni msomi gani ambaye hujui hata kuweka kumbukumbu mkuu!?yaani unataka sisi standard 7 ndio tuje tukupe somo!!? Fanya hivi mali pasipo daftari hupotea bila taarifa sisi standard 7 ndio tunatumia mfumo huu na haujawahi kufeli
Shukurani sana Mkuu,kuna kitu cha ziada napenda kusikia.mfano kuna mwenzetu pale kasema kuna app ipo pia
 
Back
Top Bottom