Je ni mbunge yupi anayefanya kazi kwa maslahi ya jimbo lake na taifa zima kwa ujumla?

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,781
1,639
Zimebaki wiki chache kabla ya bunge kuahirishwa, wabunge wengi wamechangia mawazo yao kwenye bunge hili la bajeti, je uonavyo wewe ni mbunge yupi aliyesimama kikamilifu bungeni kutetea wananchi wa jimbo lake na taifa zima kwa ujumla?
 
Magufuli
- Kuhusu jimbo lake: jimbo lake hata halitetei. Hajasikika akisema chochote kuhusu wananchi wake waliomleta bungeni kuwasemea. Asisingizie mambo ya uwaziri - wananchi wanamdai na hivyo watapima amefanya lipi jimboni mwake kama mbunge waliyemtuma kuwawakilisha.
- kuhusu masilahi ya taifa: miaka ya nyuma alijitahidi. Kwa sasa sioni lolote - sijui kanyamaziwa na JK na PM Pinda!?

Tibaijuka
-Jimboni mwake: sijamsikia
- Kitaifa: huyu mama alionekana kuanza vizuri sana katika kutetea maslahi ya taifa hasa alipo anza kugusa OPEN SPACE. Nilianza kushangilia kuwa sasa watanzania tutapata mahali pa kupumzika, kupunga upepo, ku-barbecue, etc. Lakini sasa hatuoni tena, na matumaini ya ku-barbecue yameanza kupotea. nahisi naye kanyamazishwa na JK huyu.

endeleza orodha
 
Back
Top Bottom