Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 4,729
- 5,445
Nimekuwa nikijiuliza hili swali,ila bado sijapata majibu ya uhakika. Je, wapinzani wa serikali na chama kilichopo madarakani, ni lazima wapinge kila kitu kinachofanywa na serikali ya chama kinachotawala?
Tunajua kuwa serikali zinaongozwa na watu, ambao wana mapungufu kadhaa, lakini pia wana mambo mazuri pia wanafanya. Lakini kwa uzoefu mdogo nilionao kwa siasa za nchi, hii, nimeona mara nyingi kama si mara zote wapinzani wakikosoa tu yote yanayofanywa na serikali. Je, ni kweli kwamba hakuna zuri hata moja linalofanywa na serikali?
Je, wapinzani hawawezi kukosoa pale serikali inapofanya vibaya na kusifia pale inapofanya vizuri? Vipi, kuhusu wapinzani wa nchi za wazungu ambazo tumeiga mifumo yao mingi ya utawala na siasa nao wanafanya kama huku kwetu? Naomba wataalamu wa siasa mnisaidie kujua juu ya jambo hili.