Je, ni lazima kupinga kila kitu?

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,726
5,440
Nimekuwa nikijiuliza hili swali,ila bado sijapata majibu ya uhakika. Je, wapinzani wa serikali na chama kilichopo madarakani, ni lazima wapinge kila kitu kinachofanywa na serikali ya chama kinachotawala?

Tunajua kuwa serikali zinaongozwa na watu, ambao wana mapungufu kadhaa, lakini pia wana mambo mazuri pia wanafanya. Lakini kwa uzoefu mdogo nilionao kwa siasa za nchi, hii, nimeona mara nyingi kama si mara zote wapinzani wakikosoa tu yote yanayofanywa na serikali. Je, ni kweli kwamba hakuna zuri hata moja linalofanywa na serikali?

Je, wapinzani hawawezi kukosoa pale serikali inapofanya vibaya na kusifia pale inapofanya vizuri? Vipi, kuhusu wapinzani wa nchi za wazungu ambazo tumeiga mifumo yao mingi ya utawala na siasa nao wanafanya kama huku kwetu? Naomba wataalamu wa siasa mnisaidie kujua juu ya jambo hili.
 
Ndiyo maana vinaitwa vyama vya upinzani, siyo vyama vya kupongeza!
Ili kuwa na vyama vya kupongeza inabidi serikali ipeleke muswada wa sheria bungeni ili tuwe na vyama kupongeza serikali badala upinzani!
 
Ndiyo maana vinaitwa vyama vya ipinzani, siyo vyama vya kupongeza!
Ili kuwa na vyama vya kupongeza inabidi serikali ipeleke muswada wa sheria bungeni ili tuwe na vyama kupongeza serikali badala upinzani!
Umejibu bila kutafakari hoja ya uzi ,pole sana
 
Huu msamiati wa 'kupinga kila kitu' sidhani kama uko sahihi kuendana na matumizi na pengine umekuwa ukitumika kisiasa tu na si kiuhalisia.

Nini maana ya kupinga kila kitu?

Je, ni kweli kuwa wapinzani wamekuwa wakipinga kila kitu?

Kazi kubwa na jukumu la upinzani katika siasa za nchi ni kuleta mawazo mbadala katika kile kinachofanywa na serikali iliyopo madarakani kwa maslahi mapana ya taifa. Je, huko ndiko kupinga kila kitu?
 
Nimekuwa nikijiuliza hili swali,ila bado sijapata majibu ya uhakika. Je, wapinzani wa serikali na chama kilichopo madarakani, ni lazima wapinge kila kitu kinachofanywa na serikali ya chama kinachotawala?

Tunajua kuwa serikali zinaongozwa na watu, ambao wana mapungufu kadhaa, lakini pia wana mambo mazuri pia wanafanya. Lakini kwa uzoefu mdogo nilionao kwa siasa za nchi, hii, nimeona mara nyingi kama si mara zote wapinzani wakikosoa tu yote yanayofanywa na serikali. Je, ni kweli kwamba hakuna zuri hata moja linalofanywa na serikali?

Je, wapinzani hawawezi kukosoa pale serikali inapofanya vibaya na kusifia pale inapofanya vizuri? Vipi, kuhusu wapinzani wa nchi za wazungu ambazo tumeiga mifumo yao mingi ya utawala na siasa nao wanafanya kama huku kwetu? Naomba wataalamu wa siasa mnisaidie kujua juu ya jambo hili.

Kwanza inaonekana ww ni bendera fuata upepo, ndio maana ukisikia neno unalibeba bila kujiridhisha na kulitamka kama fashion. Kwanza sio wajibu wa wapinzani kuisifia serikali. Tuje kwenye hili la kupinga kila kitu. Nitajie mpinzani yoyote aliyepinga ujenzi wa miundombinu ya maji, au miundombinu ya barabara ama shule, ili tujiridhishe kuwa wanapinga kila kitu. Na ili kufanya hoja yako ipate nguvu, tuambia ni kitu gani ccm wanawaunga mkono wapinzani, ili tujue na wao hawapingi kila kitu cha wapinzani, lakini wapinzani ndio wanawapinga kwenye kila kitu.
 
Akikujibu nitag mkuu
 
Serikali itapata kipi cha ziada ikipongezwa na wapinzani??
Kwanini mnaumia sana na kupingwa?
Miaka yote mitano mnalalamika tuu wapinzani wanapinga kila kitu, kitu ambacho sioni mantiki yake.
Halafu tambua kwa maneno rahisi kuwa wapinzani wanaionyesha serikali namna nyingine ya kufanya vitu(alternative solutions) sio mnakoita nyie "kupinga kila kitu"
 
Kazi ya upinzani sio kuishangilia serikali au kuiunga mkono, ni kuipa changamoto kwa kutafuta madhaifi yaliyopo na kukosoa.

After all vyama vya upinzani lengo lake ni kuuza sera mbadala kwa wananchi ili wafanikishe kuking'oa madarakani chama tawala.

Kama serikali imefanya jambo zuri basi ni kazi ya chama tawala kujinadi na kuisifia serikali yao, wapinzani watakaa kimya kama hakuna cha kukosoa.
 
Asante. Wewe ndiyo nimekuelewa vizuri.
 
Nimekuwa nikijiuliza hili swali,ila bado sijapata majibu ya uhakika. Je, wapinzani wa serikali na chama kilichopo madarakani, ni lazima wapinge kila kitu kinachofanywa na serikali ya chama kinachotawala?

Tunajua kuwa serikali zinaongozwa na watu, ambao wana mapungufu kadhaa, lakini pia wana mambo mazuri pia wanafanya. Lakini kwa uzoefu mdogo nilionao kwa siasa za nchi, hii, nimeona mara nyingi kama si mara zote wapinzani wakikosoa tu yote yanayofanywa na serikali. Je, ni kweli kwamba hakuna zuri hata moja linalofanywa na serikali?

Je, wapinzani hawawezi kukosoa pale serikali inapofanya vibaya na kusifia pale inapofanya vizuri? Vipi, kuhusu wapinzani wa nchi za wazungu ambazo tumeiga mifumo yao mingi ya utawala na siasa nao wanafanya kama huku kwetu? Naomba wataalamu wa siasa mnisaidie kujua juu ya jambo hili.
Je ni lazima kushangilia kila kitu?
 
Back
Top Bottom