FAHAD KING
JF-Expert Member
- Sep 14, 2017
- 301
- 373
James Watson,mwanasayansi maarufu duniani na mshindi wa nishani ya noble katika tiba mwaka 1962, ameleta mjadala mkubwa kwa madai kwamba inaelekea mtu mweusi ana akili ndogo kuliko mtu mweupe. Kauli hiyo imeshikiliwa bango na wapinzani wa ubaguzi wa rangi kwa madai kwamba inamdhalilisha mtu mweusi.
Hata hivyo Watson si mtu wa kwanza kusema hivyo isipokuwa yeye kaisema kisayansi zaidi. Siku za nyuma Waziri Mkuu mmoja wa Japan alipata kusema maneno kama hayo kwamba anatilia mashaka uwezo wa mtu mweusi. Waziri mwingine pia alishanukuliwa anasema hivyo. Wote baadaye waliomba radhi ila ujumbe ulifika.
Chika Onyeani katika kitabu chake cha The Capitalist Nigger naye anashangaa ni kwanini Mwafrika atukanwe namna hiyo na mawaziri wa Japan, lakini bado waendelee kununua bidhaa kutoka japan. Pia anasema jamii nyingi za watu Weusi zinafanana kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano ukikutana na Muamerika mweusi aliyezaliwa marekani au carribean au afrika kwenyewe bado wanatabia zilezile ambazo zinatia shaka kama kweli akili za mtu mweusi si ndogo kwa kiasi fulani.
Ukianza kuangalia matokeo mbalimbali yaliyotokea Afrika enzi za miaka ya nyuma utaanza kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya uelewa wa mtu mweusi.Historia inaonyesha kwamba ,hadi karne ya 16 kiwango cha maendeleo kati ya nchi za Afrika na ulaya kilikuwa sawa
Tunaambiwa pia kwamba miaka ya 1960 baadhi ya nchi za Afrika zilikuwa zimeendelea kimaendeleo au sawa na nchi za Asia ambazo leo ziko mbali kimaendeleo.Bado unajiuliza ni wapi kwenye matatizo? Kwanini waafrika tuachwe kila leo?
Ripoti za umaskini duniani zinaonesha kwamba umaskini umepungua kwa kiasi kikubwa lakini kwa Afrika unaonyesha kuongezeka.Mbaya zaidi maskini wa Afrika wapo kwenye dimbwi zito ambalo si rahisi kujinasua.Utafiti huu unafanywa kulinganisha na nchi za India na China ambazo zina idadi kubwa sana ya watu
Ukipima baadhi ya kauli za hawa tunaowaita wabaguzi utagundua kuna ujumbe wanawasilisha.Ukichukua Tanzania kama mwakilishi wa Afrika utaweza kugundua haya.Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi lakini si nufaishi kwa mwananchi wake isipokuwa wawekezaji wanakuwa na mamlaka makubwa juu ya rasilimali hizi.Kuna mito,Madini na misimu lakini bado tunaagizia dawa kutoka nje.SHAME!!
Watu wanajilundikia mabilioni ya Fedha kwenye akaunti zao za benki zilizopo nchini au hata nje ulaya wakati shule ya AZANIA iliyoko katikati ya jiji kuu la nchi ina wastani wa tundu moja la choo kwa wanafunzi 300
Bado tunazipa likizo ya kodi kampuni kubwa huku tukifuatilia vikodi vidogo vidogo.Kampuni kubwa zinaruhusiwa kubeba hasara na kuipeleka kwenye mahesabu ya mwaka ujao kwa miaka KADHAA lakini hiyo hiyo kampuni inaendelea kufanya biashara.Hapa sisi ni wakusanyaji wazuri wa kodi au wakwepaji wazuri wa makampuni makubwa?
Inafaa tujiulize kunani kwenye akili zetu?Tunasema tuna mafuta lakini tukitaka kuyachimba tunamwita mzungu japokuwa tumekuwa tukizalisha wakandarasi na wanajiorojia kila mwaka.Lazima tujiulize kama elimu yetu ina mushikeli au la!Sasa hivi tunajigamba kuwa na vyuo vikuu 30 lakini bado tunaagizia vijiti vya kuchokonolea meno toka Malaysia. Kweli??
Kabla ya kushika mabango na kuwalaani wabaguzi wa rangi lazima tujiulize kwanza ni wapi tumekosea na sababu za kukwama kwetu.Tusikimbilie kulaumu wazungu kwa kuleta ukoloni na ukoloni mambo leo.Malaysia na Ghana zote zilikuwa koloni za muingereza na zilipata uhuru mwaka 1957 kwa pamoja lakini leo hali ni tofauti.
Wamalaysia walikuwa wanakwenda Ghana kujifunza kilimo cha mawese. Leo hii Ghana wanajifunza kila kitu toka Malaysia kikiwemo kilimo cha mawese.Wazungu wanaopinga kauli za WATSON sio kwamba wanasikitika sana bali wanaonesha kukasirika usoni lakini moyoni wanasema ni kweli hawa wanaujinga wao mkubwa.Wanatutetea ili waendelee kutuvuna.Hawataki tukaechini na kujitathmini tulipoenda mrama.
Nachukia kuitwa kiumbe dhaifu hasa kiakili.Nachukia kwa sababu naupenda uafrika na WEUSI wangu.Nawapenda waafrika wenzangu.Nachukia wanapoambiwa kwamba wanaubongo dhaifu. Lakini nahisi kuna mahali kama watu WEUSI tumekosea
Kama mtu anaiba mabilioni ya fedha za umma kwenye nchi maskini na kuyaweka ulaya au kewekeza mahali popote,huku kukiwa na wananchi wanakufa kwa kukosa madawa hospitalini basi kuna ulazima wa kujiuliza tuliko na kasoro.Kama viongozi wanawaibia wananchi wao waliowachagua kuwawakilisha bila aibu yoyote inabidi tuhoji akili zetu.Kama wananchi wanaridhika na hila za viongozi wao bila ya kuchukua hatua madhubuti basi tuhoji akili zetu
JE? Watson aombe radhi
Hata kama Watson ataomba radhi kama mawaziri wa Japan atakuwa amepeleka ujumbe mzito kwa watu WEUSI kujichunguza.Huu ni ujumbe mzito kwa taifa letu la Tanzania.Mimi ni miongoni mwa wasioamini upuuzi wa James Watson, kwamba waafrika tuna akili ndogo.
Historia inaonyesha kwamba chuo kikuu cha kwanza duniani kilikuwa Afrika,kule Mali.Uvumbuzi wa hisabati ulitoka Afrika,hata mtu wa kwanza duniani anaaminika kuishi Afrika.Pia MAAJABU mengi yapo kule misri (pyramids)
Wapo waliokwenda mbali na kusema kwamba hata YESU KRISTO alikuwa mtu mweusi wa misri na kwamba ndiyo sababu SIMON WA KRENE,ambaye alikuwa mtu mweusi alimsaidia YESU kubeba msalaba.Ilikuwa ni huruma ya kuona mtu mweusi mwezake anateswa.
Jamani ni wapi tumekosea??
Sasa je,ni kweli watu WEUSI tuna akili ndogo??
Sent using Jamii Forums mobile app