Je, ni kweli plate namba D zinachongwa?

mfate42

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
3,777
4,269
Je, nikweli sikuhizi plate namba D zinachongwa tu kihuni hata kama gari lilikuwa namba B. Inabadilishwa na kuwa namba D ili baadaye ikauzwe kwa Bei ya juuu?

Naomba ufafanuzi.
 
Hicho kitu hakipo so usidanganywe ndugu,kitu unachoweza kudanganywa tu ni kwamba mtu anaweza nunua gari zanzbar iliyotumika miaka 6 alafu akaifikisha bara akafnga namba Dv sababu inaruhusiwa kisheria.

Ztajuaje kama ni gari ya zanzibar
1,condition ya gari inaweza isiwe nzuri hasa body upande wa rangi

2,Pia ukiangalia kwenye vioo vya side mirror vingi huwa vinaandikwa namba za zanzbar (plate no)

3,Ukiona gari huielewi unaruhusiwa kwenda kuangalia uhalali wake na historia ya ilikopitia kupitia ofisi za TRA samora
 
Hicho kitu huwa hakipo, ni maneno tu.

Ndg yangu alikuwa na hela ya kununua gari tangu miezi mitatu imepita...anapata gari nzuri lakini hiyo ya kuhusu kuforge namba imempotezea muda sana

Ila nakuhakikishia hakuna hicho kitu
 
Je nikweli sikuhz plate namba D zinachongwa tu kihuni hata Kama gari lilikuwa namba B..inabadilishwa na kuwa namba D ili baadae ikauzwe kwa Bei ya juuu...?..naomba ufafanuz
Hahaaaa!!halafu na kwenye mfumo wa tra , wanabadirisha?maneno ya kijiweni hayo.
 
Inawezekana kama gari lilikuwa na namba za zanzibar.. ila kama limeingilia bara.. ni haiwezekani kabisa
 
Kuna scenario ya special number. Mimi nimeona gari aina ya Cruser Vx yenye number T xxx IMG
ni gari ya takribani miaka 3 iliyopita ikuwa na namba hiyo , hivyo basi inawezekana kuwa na special number unayoitaka.
 
Gari anagalia ubora wake,mambo ya namba "D" mnapigwa sana tu.
Kwamfano kuna muhindi ana Maruti namba "B" lakini imenyooka utasema imeshuka leo,nahivi hawanaga ruti ndefu za gari,nimemuweka pending akiisukama anicheki.
 
Ni utunzaji mbovu ndiyo unafanya gari lichakae,
Namba D unakuta limechoka kama lori la shule za serikali..
Kunamtu nilimkuta chanika anapakia viroba vya mchanga kwenye buti Primio namba"D"nikamwambia live kwajinsi unavyoifanya hii gari niwazi sio gari yako umeazima tu.
 
Kuna mtu nilishamsikia anasema inawezeka yaani ni kwamba inatafutwa ist no D ilokula mzinga wanachomoa no inaenda kuwekwa kwenye ist ilokuwa na no A pia kadi na vitu vingine vinabubwa kinamna hiyo
NB Usinunue gari kwa no utapigwa mjini hapa
 
Back
Top Bottom