Je, ni kweli Moshi na Arusha ndo inaongoza kwa kuwa na mafundi rangi wazuri wa magari?

Kwenye suala la bodi lote kwenye mahari. Hiyo mikoa inaongoza kuanzia rangi kunyoosha gari pasi grade A. Na "modi" zozote ukitaka ni Moshi/Arusha na Tanga kidogo

Nadhani ni katoka kutengeneza sana zile Cruiser za utalii modifications imewapa garage nyingi uzoefu over time
 
Habari wadau,

Ninahitaji Fundi rangi mzuri, nimefanya research kati ya watu 8 katika 10 wanasema nipeleke gari Moshi au Arusha sababu wanajua vizuri kupiga rangi.

Je, ni kweli wanapatikana huko tu?
Siyo tu Rangi, mautundu yote ya ufundi wa magari yapo moshi na arusha. Nakumbuka kuna miaka scania walikuwa wanaendesha mashindano ya kusambaratisha engine za scania na kuzifunga faster kuna jamaa yangu Fulani alikuwa anaongoza kila wakija anachukua no. 1 na mkwanja wa kutosha pale arusha. Yaani kwa kifupi mautundu ya magari yapo kwenye hii mikoa. Udereva nk. Kuna mhindi mmoja alikuwa anatumika kufanyia interview madereva wa semi. Huulizwi chochote yeye anakaa kushoto wewe unaendesha anakuongoza kwenye vichochoro ukitoboa ajira nje nje! Hii ilikuwa arusha
 
Kwa mafundi ambao sio wababaishaji Moshi ni hakika, gari ikiwa ina tatizo unaelezwa straight na anachosema ndicho hasa na gharama zao ndio zitakuacha taya wazi.

Huku Dar mtu kufunga wishbone bush tu anataka umpe 20K wakati moshi kazi hio hio mtu anaifanya hata kwa buku 5!

Overhaul mtu anakufanyia kwa laki 1 Moshi. Ila hapa Daslam mtu wa overhaul lazma umuandalie hela ya tofali za nyumba nzima. Ndio akufanyie hio kazi na pengine hata asiweze akamtafute mtu mwengine ndio amfanyie hio kazi.

Body works ukiwa na 30K gari wana clear dents zote na kurudishia rangi. Hapa Dar hio 30K ni labour charge tu 😂😂😂
 
... Moshi na Arusha wana connection za karibu sana na Nairobi; spare za kila aina zipo Nairobi ni sauala la kuvuka mpaka kwa bodaboda kuzifata. Interaction ya pande hizo mbili imesaidia pia kuwajengea uwezo mafundi wa miji hiyo.

Spare kwa mfano za Peugeot, Volvo, Maserati, etc. utazipata wa Dar? Mpaka uagize mitandaoni wakati Nairobi ziko tu madukani tena GENUINE tofauti na Dar magumashi mengi.
 
Habari wadau,

Ninahitaji Fundi rangi mzuri, nimefanya research kati ya watu 8 katika 10 wanasema nipeleke gari Moshi au Arusha sababu wanajua vizuri kupiga rangi.

Je, ni kweli wanapatikana huko tu?
Njoo Mbezi nifate inbox ushangae
 
Back
Top Bottom