Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,432
- 73,078
Katika page ya East African Radio Facebook wametaarifu kuwa wafungwa 31 wamegoma kula kwa siku kadhaa wakipinga kulazwa chumba kimoja idadi kubwa sana ya watu katika gereza la Maweni huko Tanga. Wametoa na picha ya mlindikano huo vyumbani.
Tungependa tujue jee ni kweli nchi yetu imefikia mahali magereza yetu yanaweza kulaza watu kwa namna hii kweli? Maana pamoja na wao kuwa wafungwa bado ni binadamu, pia bado nchi yetu na hasa jeshi la polisi tunashutumiwa kwa kuwa na kesi nyingi sana ambazo watu wanafungwa kwa kubambikwa, kukosa msaada wa kisheria na kushindwa kutoa hongo.
Katika jumuia ya watu waliostarabika inawezekana kweli kuruhusu hali kama hii ikatokea na hakuna hatua madhubuti za kukabiliana nayo huku tunasema tunataka kupambana na udhalimu?
Picha yenyewe ya wafungwa/mahabusu iliyowekwa na East afrika Radio ni hii hapa;
Mambo kama haya si yapo huko Burundi,DRC nk sasa hata kwetu pia?