Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,181
- 5,321
Mimi ni nani? Pasina shaka sifahamu, Je huyu anayeongea ndani yangu ni nani?
La! nahisi ni akili au nafsi au roho ama tuko binadamu wawili katika mwili mmoja yaani mmoja anaongelea nje(kwa sauti)na mwingine ndani,pengine huu mwili ni kasha tu ndani yake wameinstall program inayojiratibu yenyewe, au yawezekana ni sauti ikaayo ndani ya mwili kiufupi sina uhakika.
Nimewaza vyema lakini nimewaza mambo magumu na makubwa sana, nilipaswa kuwaza kidogo tu kwa yale madogo na ningeweza kuwa chachu ya mabadiliko katika ulimwengu huu, hivi kwanini badala ya kujiuliza mimi ni nani, nilitokea wapi, lipi ni kusudi la uwepo wangu nakadhalika.
Nisijiulize juu ya yale yaliyowezekana kwa akili za mwanadamu; kwanini kompyuta iundwe ikiwa na processor, hard disk,vihifadhi kumbukumbu,window n.k,
kwanini gari liundwe namna hii mfano liwe na mifumo ya umeme, maji, mafuta, lisukumwe na pressure ndogo sana ya pedeli n.k
Ndege yawezaje kupaa,meli yawezaje kuelea, internet, network inafanyaje kazi,ala za sauti zilitengenezwaje, mtetemo upelekeao sauti unafanyikaje n.k
Bila shaka maswali ya namna hii ni lukuki na hayana maana yeyote mbona vyote hivi tiyari vina majibu na uthibitisho wa kisayansi na karibia vyote nimevisoma na nimevichunguza na kuvitumia tiyari na hivyo sioni jipya lakujiuliza hapo.
Ni kweli niwazavyo niko sawa kabisa, lakini kwanini wawe ni wengine tu ndo wavumbuzi na waanzilishi wa vitu hivi na siyo mimi?
Kwani kipi nimefichwa mpaka isiwe mimi na awe mwingine?
Ila kama siyo mimi kwani ugunduzi huu wanamfanyia nani?
Na je kama wanavumbua vitu ile sense ya kiweje na kitumike vipi au kwa sababu gani huwa wanaitoa wapi?
Je, kabla ya kuamua kiweje hicho walichovumbua akilini mwao nini huwa kipaumbele chao?
Mathalani wanayemuwazia siyo mwingine ni mimi, kuwa kama ni chombo nitakiendesha vipi, dawa niitumie vipi,teknolojia niitumie vipi nakadhalika.
Hivyo yawezekana mimi ndiye chanzo cha uwepo wa vitu vyote vilivyo na vinavyoendelea kuvumbuliwa.
Na pengine kupitia mimi vifaa na vitu hivi ufanya kazi sawasawa na ufatisho bandia/usiyo halisia wa mwili wangu ufanyavyo kazi kwa kuwekewa mifumo iliyoigilizia tabia,mifumo,mijongeo,fahamu na hisia ndani na nje ya mwili wangu.
Sasa kwanini vivumbuliwe vifaa hivi katika mifumo inayoelekeana na sifa za mwili wangu na vifanye kazi kweli japo si katika asilimia mia sawa na ninavyopumua automatic,kutenda ama kufikiri.
Bila shaka mvumbuzi hawezi kuvumbua nje ya upeo wa kile anachofahamu kujihusu yeye na mazingira yake ya ndani sawa sawa na yale ya nje ya mwili wake.
Aghalabu nimekuwa nikizingatia mazingira ya mwili wangu kwa nje na kidogo sana ya ndani ila pia kwa kuwa nilisomea mambo ya udaktari basi hapo unifichi kitu kwenye ufahamu juu ya mwili wa kiumbe hai.
Ila je, nimarangapi nimewahi kufikiri kuwa mkono wa mwanadamu nikiuchunguza kwa umakini na unavyofanya kazi naweza vumbua katapila lenye mfano wa kijiko kikubwa kama mkono litumiwe na mainjinia kwenye shughuli zao?
Je, kama mwili wa mwanadamu unatumia maji(kujipooza),nishati nguvu/umeme(kujiendesha),damu=mafuta(kusambaza hewa na
chakula),ubongo+moyo+n.k(mifumo au parts za injini), mishipa (sawa na mirija na pipe zakupitisha fluid)ute ute na vilainishi kwenye maungio na sehemu laini=oil na greese, kutoa taka mwili=moshi n.k
kwanini niendelee kujiuliza kuwa aliyetengeneza gari aliwaza nini kwanza?
Bila shaka huu ni mfano mdogo tu kati ya vingi alivyovumbua na anavyoendelea kuvumbua mwanadamu vyote uanzia katika akili yake kujitafakari alivyo ndipo hapo wazo uja la kuunda chenye ufanano nae kufanikisha lengo lililokusudiwa.
Hivyo basi nikiamua kubadili chochote au kuja na jambo jipya katika mazingira yangu nisikimbilie nje ya mazingira ya mwili kwanza nikidhani ntaweza unda au kuratibu chochote bali sina budi kuanzia ndani yangu ndipo penye ukweli na uhalisia wa kile ninachokifanya.
Nimejifunza kuwa asili ya vyote ipo ndani yangu na kile kionekanacho nje nimatokeo ya ufahamu au dhamira ya ndani kunihusu, hivyo nilichofichwa siku zote ni kuwa nikijitafakari mimi kwanza nikagundua kisha nikaoanisha na mapungufu yangu katika mazingira ya nje, hakuna cha kunizuia.
Sent using Jamii Forums mobile app