Je, ni kweli kuna baadhi ya wateule wa Rais walipaswa kuwa Mirembe!. watumbuliwe?. Aliyetamka haya ni shujaa au ni mchochezi anaestahili kutumbuliwa?

Rais akisema ni amri "mfano akisema askari fulani apandishwe cheo" mwenye dhamana sasa ndio aanze kumuandalia taratibu muhusika za kupandishwa hicho cheo"
Kipindi rais anaagiza wananchi wasibughuziwe kwenye mapori ya akiba, hapo sasa (kama ipo sawa lakini) lilitakiwa tamko la maandishe litoke kwa katibu mkuu kiongozi likimuelekeza katibu mkuu wizara ya maliasili, pamoja na katibu mkuu ardhi(kama niko sawa) kutengeneza kanuni au kutoa maelekezo kwenda kwa hao maRC na maDC waache kuwaondoa hao wanachi bali kuwapangia utaratibu, ili wasizidi kuingia ndani zaidi......
Kama kuna waraka uliwaelekeza maRC na maDC kulinda maeneo ya akiba ya hifadhi, basi kuwe na waraka wa kuwaelekeza pia... nao wautiii.
Hii staili ya 'one man show' ifikie kipindi km nchi tuachane nayo badala yake tutengeneze mfumo imara wa kudili na ishu km izo, hii staili ya kila kitu mpaka rais aseme kiukweli sometimes inachelewesha hta maendeleo na inaboa sana kiukweli.
 
Hii staili ya 'one man show' ifikie kipindi km nchi tuachane nayo badala yake tutengeneze mfumo imara wa kudili na ishu km izo, hii staili ya kila kitu mpaka rais aseme kiukweli sometimes inachelewesha hta maendeleo na inaboa sana kiukweli.
Hii inaitwa mkuki kwa mtamu mchungu kwa nguruwe binadamu.Polisi wamepewa uwezo wa Kimungu sasa wamekuwa israeli
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali

Jee ni Kweli Kuna Baadhi ya Wateule wa Rais Walipaswa Kuwa Mirembe?. Watumbuliwe?. Aliyetamka Haya ni Shujaa Au Ni Mchochezi Anaestahili Kutumbuliwa?.

Nimeisikiliza kwa makini video clip hii ya jana ikimuonyesha Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kondoa Dr. Ashatu Kijaji, akizumza kwa uchungu mkubwa but with extra ordinary confidence kuhusu kilichotokea jimboni kwake.

Kitu kikubwa nilicho kiona mimi ni jinsi Naibu Waziri Dr. Ashatu Kijaji anavyozungumza kwa confidence kuhusu haki ya Mbunge kuzungumza na wananchi wake wa jimbo lake wakati wowote na mahali popote bila ya kuhitaji ruhusa ya yeyote.

Kiukweli kabisa, huu ni ushujaa wa hali ya juu. Mtu mwenye confidence ya kiwango hiki ndie angepaswa kuwa Waziri Mkuu.

Alichokisema hapa Dr. Ashatu Kijaji ndicho katiba yetu ilichokisema na ndicho sheria yetu ya vyama vya siasa ilichotamka kuwa Mbunge au kiongozi wa siasa yuko huru kufanya mkutano wa siasa kwa kuzungumza na wananchi wake wakati wowote na mahali popote bila kuomba kibali chochote kwa yoyote ila tuu kwa kutoa taarifa kwa OCD just for security reasons na sio kuomba kibali bali kutoa tuu notification.

OCD hapaswi kutoa kibali bali kupokea taarifa na kutoa ulinzi if utahitajija.

Iwapo OCD anazo taarifa za kiitelijensia za kuhatarisha amani, then OCD anayo mamlaka ya kisheria ya kuzuia mkusanyiko huo.

Katika utekelezaji wa hayo Ma OCD wamejipachika umungu mtu wa kutoa vibali vya mikutano na kuisambaratisha mikutano au maandamano yasiyo na vibali.

Amini usiamini, uvunjifu mkubwa wa amani katika mikutano na maandamano ambayo husababisha vifo na umwagaji wa damu, yanasababishwa na Jeshi la polisi na nawahakikishia watu humu, hakuna tone la damu ya mwanadamu itajayo mwagika au kupotea bure bila kufidiwa hapa hapa duniani kupitia karma au mbele ya Mungu kwa kwenda motoni.

Swali ni jee mkutano huu wa Dr. Ashatu Kijaji ulikuwa na kibali?. Kama haukuwa na kibali, mkutano kama huu ungekuwa umeitishwa na Mbunge wa upinzani hali ingekuwaje?!. Wabunge wengi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiswekwa ndani kwa kosa la kufanya mkutano bila vibali, hii video clip ni ushahidi usiotia shaka kuhusu mkutano huu, hivyo natoa wito kwa jeshi letu la polisi kupokea video hii kama ushahidi, Dr. Ashatu Kijaji akamatwe atiwe ndani kwa kosa la kufanya mkutano bila vibali na kushitakiwa kwa uchochezi maneno aliyozungumza hapa.

Jeshi la polisi lisipofanya hivyo, hii itakuwa ni double standards ya hali ya juu. Wapinzani wakifanya mikutano bila vibali ndio hutawanywa na Polisi lakini wakifanya CCM ni halali

Maneno ya Dr Ashatu Kijaji kuwa baadhi ya viongozi wanaopaswa kumsaidia rais walipaswa kuwa Mirembe. Kama ni kweli, inambidi rais Magufuli awaondoe viongozi wanaopaswa kuwa Mirembe, kama rais ameridhika na kazi nzuri ya wateule wake, then aliyesema wateule wa rais wanastahi kuwa Mirembe, ndio atumbuliwe.
Hivyo ndani ya siku mbili hizi ana tutashuhudia viongozi wa Mirembe wakitumbuliwa, au Shujaa wa siri ya viongozi wa Mirembe akitumbuliwa kwa kutoa siri ya mteuzi kuteua wa Mirembe. Kusipofanyika yoyote kati ya hayo, then wote watakuwa ni wale wale

Fuatilia issue yenyewe
Mkuu Joka Kuu, kwanza asante kwa hii nondo, kwa ruhusa yako naomba nitumie kama mbegu kurutubishia bandiko langu fulani

Huyu Dr. Ashatu Kijaji, japo ni Mwanamke wa shoka, na huwa hakopeshi, katika hotuba yake anawachongea RC na DC, hivyo naomba kuwaandaa kisaikolojia ikiwa Dr. Ashatu Kijaji ana powers fulani ambazo leo naomba nisiziseme hapa, mtashuhudia RC na DC wakipumzishwa. Hili likitokea nitamalizia kwa kuzizungumza hizo powers zinazomfanya ana zungumza kwa confidence anayozungumza nayo ikiwemo kufanya mkutano wa hadhara bila kibali. Angekuwa ni opposition amefanya hayo na kuzungumza hivyo, kwanza wangetawanywa kwa mabomu ya machozi na yeye angeishia mahabusu.

Pili amezungumzia kauli za rais kuwa sio ombi ni maagizo, ni amri, zikitolewa tuu zinapaswa kutekelezwa hata bila maandishi.

Ni kweli kauli za rais ni amri lakini kutekelezwa bila maandishi ni heshima tuu lakini sio utaratibu. Kauli za rais ambazo zinatakiwa kuwa amri ni lazima ziandamane na maandishi.

Lakini kiukweli rais Magufuli anatoa kauli nyingi sana na zinatekelezwa papo kwa papo bila maandishi, ila litakapo kuja kujitokeza suala la uwajibikaji, ofisa wa serikali anayetekeleza amri ya rais bila maandishi, iki backfire, inakula kwake, hii imemcost IGP Mangu na Waziri wake Mwigulu naomba nisiiseme zaidi ni mambo yao ya ndani.

Kwenye hili la amri za rais za kauli tuu bila maandishi, mimi nina mambo matatu
1. Tumeshauri humu, rais akitoa maagizo, maagizo hayo yafuatiwe na maandishi. Kama ni kweli rais Magufuli alitoa kauli kuwa wanavijiji jirani na mapori ya akiba, waendelee kulisha mifugo kwenye mapori hayo, ilipaswa ifuatiwe na maandishi, vinginevyo ma DC na ma RC wataendelea kuyalinda mapori ya akiba, watataufisha mifugo yote inayokamatwa ndani ya mapori ya akiba na kuwatwanga risasi wavamizi wote wa mapori ya akiba kwa mujibu wa sheria. Ndio maana RC na DC wamempuuza Mbunge Mhe. Dr. Ashatu Kijaji.

Pili sio kila amri ya rais ni final and conclusive https://www.jamiiforums.com/threads...upigwa-chini-na-mchanga-kusafirishwa.1225154/

Tatu miluzi mingi inamchanganya mbwa anakuwa hajui afuate lipi. Tanzania tunaongozwa na Katiba, sheria, taratibu, kanuni, ilani ya CCM, kauli za rais, kauli za viongozi etc, sasa tufuate lipi?. https://www.jamiiforums.com/threads...uko-kinyume-cha-katiba-sera-na-ilani.1481310/

Namalizua kwa swali, jee ni kweli kuna Wateule wa rais Magufuli walipaswa kuwa Mirembe?.

Aliyetamka haya ni shujaa au ni Mchochezi?.

Jee Wateule wa Mirembe watatumbuliwa au atatumbuliwa shujaa aliyetoa siri za wateule wa Mirembe?.

Nawahi Kanisani
Jumapili Njema
Paskali
Napendekeza Dr Kijaji awe Spika wa bunge la JMT kunako 2020 full stop!
 
PM, ukibishana na kichaa, watu watashindwa kuwatofautisha. Mengine soma halafu potezea.
Sheria ilitamka kutoa tuu notification, polisi wakageuza kuomba kibali.
Maadam polisi wameisha geuza mambo ya vibali, then ukimripoti mtu, tumia hiyo hiyo taratibu yao ya kibali.
 
Back
Top Bottom