Bei ya tv box ya ni 75,000/- kwa arusha
Na hiyo ni AV to VGA. Ukumbuke lazima uwe na kingamuzi.
Ukiweka na kingamuzi hapo kama shs 100,000/-
Ubora wa picha na sauti
Picha yake sio bora sana ,haifikii picha ya tv yaani resolution yake huwa ndogo.
Ubora wa sauti
Sauti itategemea kingamuzi unachotumia kwa sababu sasa hatuna analog TV broadcast.
Kuhusu kuharibika
haiharibiki kirahisi ila kama ikiharibika upande wa powersupply ni majanga. Pia adapter zake ni ngumu kupata endapo itaungua.
Kuhusu kubebeka.
Kwanza hapo unakuwa na vitu vifuatavyo:
1. Monitor
2. TvBox
3. Adapter ya tvbox
4. Vga cable
5. Kingamuzi
6. Remote ya tvbox ambayo mara nyingi zipo kama zile remote za FM modulator za kwenye gari.
Kuna baadhi ya tvbox unaweza kuzifunga nyuma ya monitor endapo monitor nayo ina matundu ya kufungia.