Mlimani health center
JF-Expert Member
- Nov 25, 2021
- 595
- 1,418
Sekta ya utalii Nchini Tanzania imeweka rekodi mpya ya mapato kwa mujibu wa ripoti ya ufanisi wa uchumi kwa mwezi September 2023 iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyoonesha kuwa sekta hiyo imeingiza mapato ya Dola za Marekani Bilioni 3.07 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa katika historia ya sekta hiyo.
Rekodi hiyo ya ongezeko la mapato ya utalii imefanya mapato kwa ujumla kufikia USD Bilioni 5.6 kwa mwaka ulioshia August 2023 kutoka USD Bilioni 4.2 za kipindi kama hicho mwaka jana ambapo utalii umechangia USD Bilioni 3.07 ukifuatiwa na usafirishaji ambao umechangia USD Bilioni 2.09 huku sekta nyingine kwa pamoja zikichangia USD milioni 446.3.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo sekta ya utalii imezalisha mapato mengi kutokana na kuimarika kwa sekta hiyo ( baada ya janga la corona na changamoto nyingine) ambapo Watalii wameongezeka nchini na kufikia 1,686,024 kutoka 1,279,211 mwaka jana.