Je, ni kweli Dr. Karl Peters aliruhusiwa kuingia Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar? Je, Karl Peters alisali KKKT Azania Front?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,028
142,088
Nimemsikia mtangazaji wa Upendo TV akiripoti kutokea Cathedral ya Azania Front akisema hapo ndipo alipokuwa anasali Dr. Karl Peters.

Na nimesoma kwenye gazeti fulani kuwa Karl Peters aliruhusiwa kuingia Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar wakati huo.

Na zaidi ikasemwa Karl Peters aliwahi kuuwa kijiji kizima cha Wachaga huko Rombo.

Naomba majibu ya swali langu, ikumbukwe Karl Peters ndiye aliyemsainisha Mikataba wa Kitapeli Chifu Mangungo wa Msovero.

Nawatakia Dominica njema 🌟
 
Nimemsikia mtangazaji wa Upendo TV akiripoti kutokea Cathedral ya Azania Front akisema hapo ndipo alipokuwa anasali Dr Karl Peters

Na nimesoma Kwenye Gazeti fulani kuwa Karl Peters aliruhusiwa kuingia Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar Wakati huo

Na zaidi ikasemwa Karl Peters aliwahi kuuwa kijiji kizima cha Wachagga huko Rombo

Naomba majibu ya swali langu ikumbukwe Karl Peters ndiye aliyemsainisha Mikataba wa Kitapeli Chifu Mangungo wa Msovero

Nawatakia Dominica njema 🌟
Aliua kijiji kizima Rombo....

Alikuwa na jeshi au aliua yeye mwenyewe kwa gobole lake?
 
Mnaonaje mtwangane makonde ubishi uishe

Mashekhe vs Mapadre

Waumini wa kiislamu vs Waumini wa Kikristo

Wapagani tutakua marefa

NB: Waamini wa kiislamu na mashekhe hujifunza kung-fu sijajua wakristo, wekeni mambo sawa ili tupange sehemu...kama itakua Dar itafaa zaidi iwe pale Mkapa stadium ili mashabiki tuwe wengi

Asante.
 
Nimemsikia mtangazaji wa Upendo TV akiripoti kutokea Cathedral ya Azania Front akisema hapo ndipo alipokuwa anasali Dr. Karl Peters.

Na nimesoma kwenye gazeti fulani kuwa Karl Peters aliruhusiwa kuingia Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar wakati huo.

Na zaidi ikasemwa Karl Peters aliwahi kuuwa kijiji kizima cha Wachaga huko Rombo.

Naomba majibu ya swali langu, ikumbukwe Karl Peters ndiye aliyemsainisha Mikataba wa Kitapeli Chifu Mangungo wa Msovero.

Nawatakia Dominica njema 🌟
FaizaFoxy
 
Carl Peter alitoka nchi gani kwanza?
Nchi aliyotoka Kanisa gani ndo Lina nguvu?KKKT ndo makao makuu ya Hilo Kanisa na alipotoka Carl Peter??
Carl Peters alitoka Ujerumani na alikuja Africa mashariki kuitafutia nchi yake Makoloni

Carl Peters baba yake alikuwa Mchungaji
 
Mnaonaje mtwangane makonde ubishi uishe

Mashekhe vs Mapadre

Waumini wa kiislamu vs Waumini wa Kikristo

Wapagani tutakua marefa

NB: Waamini wa kiislamu na mashekhe hujifunza kung-fu sijajua wakristo, wekeni mambo sawa ili tupange sehemu...kama itakua Dar itafaa zaidi iwe pale Mkapa stadium ili mashabiki tuwe wengi

Asante.
Naunga mkono hoja
Wapagani tutakuwa tunacheka tu
 
Kabla ya mwaka 1885 Deutsch-Ost Afrika au Tanganyika hazikuwepo.
Wapelelezi wa Kijerumani waliosaini mikataba na machifu ni Dr Karl Peters na Dr Karl Juhlke.
Maeneo mengi ya huku Tanzani bara yalikuwa chini ya usimamizi wa Zanzibar (Under Suzerainity).

Sehemu kama Arusha (Aruscha) na Kilimanjaro zilikuwa ziko chini ya Sultan wa Zanzibar ambaye naye aliwadanganya machifu wa huku bara. Tatizo lilianza ni kwamba Dr Karl Peters na Dr Karl Juhlke waliwashinda waarabu akili. Wenyewe walienda kusaini mikataba mipya na machifu wa huku bara ambapo, hao machifu walisema hawako chini ya Sultan. Aliyewasaidia wakina Karl Peters kumzunguka Sultan alikuwa ni mwarabu na Mkalimani Bwana Ramadhani ambaye alitumika kama mtafasiri aliyesaidia kusainiwa mikataba feki.

Kipindi hiki pia, Sultan wa Zanzibar alikuwa na ofisi ya kibalozi huku bara. Msimamizi wa hii ofisi alisema wazi kwamba Sultan hakuwa anamiliki maeneo yoyote huku bara mbali na maeneo ya Pwani. Baada ya mkutano wa Berlin kuisha mwaka 1884, Sultan wa Zanzibar aliandika barua kwa Mfalme wa Ujerumani na Uingereza, kwanini walimzunguka na hakushirikishwa ilhali maeneo mengi ya huku bara ni yake. Sultan wa Zanzibar alifanya makubaliano mengine kuhusu Mombasa, kipindi hicho akimshirikisha Muingereza na Mjerumani.

Taarifa hizi kuhusu maeneo ya kule Kaskazini na Sultan kutaka kuyatawala, mara ya kwanza kabisa ziliwekwa wazi mwaka 1972 na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania. Wanasheria na watafiti wa Wizara, Bwana Earl Seaton na Sosthenes Maliti waliandaa chapisho zuri kabisa ambalo liliweka wazi hii mikataba na barua za Sultan kwa wafalme wa Uingereza na Ujerumani kuhusu maeneo ya Tanganyika. Kiufupi, hao wanaoshabikia usultan kwasababu za kidini huwa nawaona kama watu fulani waliopagawa akili.

Nikipata wasaa ntayaweka hayo machapisho na zile barua, nadhani bado zitakuwepo kwenye ile maktaba. Kuna machapisho yanaitwa Tanzania Treaty Series, yalikuwa yanaandaliwa na Foreign Affairs Office, lakini waliacha kuyachapisha. Mle ndani hadi mikataba yote kuhusu Tanganyika mnamo karne za 19 na 20 mwanzoni ipo.
 
Alikuja mwaka gani?
 
Na nimesoma kwenye gazeti fulani kuwa Karl Peters aliruhusiwa kuingia Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar wakati huo.

Na zaidi ikasemwa Karl Peters aliwahi kuuwa kijiji kizima cha Wachaga huko Rombo.
Hawatakiwi kukumbukwa kwa lolote
 
Nimemsikia mtangazaji wa Upendo TV akiripoti kutokea Cathedral ya Azania Front akisema hapo ndipo alipokuwa anasali Dr. Karl Peters.

Na nimesoma kwenye gazeti fulani kuwa Karl Peters aliruhusiwa kuingia Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar wakati huo.

Na zaidi ikasemwa Karl Peters aliwahi kuuwa kijiji kizima cha Wachaga huko Rombo.

Naomba majibu ya swali langu, ikumbukwe Karl Peters ndiye aliyemsainisha Mikataba wa Kitapeli Chifu Mangungo wa Msovero.

Nawatakia Dominica njema 🌟
Sultani gani wa Omani alieshi Zanzibar wakati wa Karl Peters ?? Hebu tuwekee sawa hapa
 
Nimemsikia mtangazaji wa Upendo TV akiripoti kutokea Cathedral ya Azania Front akisema hapo ndipo alipokuwa anasali Dr. Karl Peters.

Na nimesoma kwenye gazeti fulani kuwa Karl Peters aliruhusiwa kuingia Tanganyika na Sultan wa Oman aliyeishi Zanzibar wakati huo.

Na zaidi ikasemwa Karl Peters aliwahi kuuwa kijiji kizima cha Wachaga huko Rombo.

Naomba majibu ya swali langu, ikumbukwe Karl Peters ndiye aliyemsainisha Mikataba wa Kitapeli Chifu Mangungo wa Msovero.

Nawatakia Dominica njema 🌟
Sultan wa Oman na Zanzibar alikuwa Seyyid Said alifariki 1856 na himaya yake ikagawqnyika mwanae mmoja Majid akarithi ZanZibar na Afrika mashariki.Mwingine Thuwain akarithi Oman.Kuanzia hapo wakawa maadui.Sultan Majid alirithiwa na Barghash na huyo ndo alikutana Karl Peters.
 
Back
Top Bottom