Je! Ni Kweli BVR Machine zina Background Database of Pseudonames?

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Oct 27, 2008
456
0
Leo jioni nikiwa napita eneo moja karibu na kituo cha uandikishaji wapiga kura kulikuwa na zogo. Madai ni kwamba kituoni hapo imebainika mashine moja ya BVR imeonesha imeshakuwa na majina 1000 ya wapiga kura katika kituo hicho wakati ilikuwa ndio kwanza mtu wa kwanza anaandikishwa kituoni hapo.

Kama ni kweli kwamba machine zinakuwa tayari zimejazwa majina feki ya kituo husika kabla ya kuandikwa majina halisi wa kituo husika; hili ni jambo la hatari sana kwa mustakabali wa demokrasia na amani ya taifa hili.

ANGALIZO: Tuwe makini kwa taarifa kama hizi LAKINI pia tusizipuuze.
Vilevile kuna haja ya kujiuliza inakuwaje NEC wanasema wamepita malengo yao ya uandikishaji kwa kiasi kikubwa wakati watu wengi wanalalamika wameshindwa kujiandikisha.
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,194
2,000
Leo jioni nikiwa napita eneo moja karibu na kituo cha uandikishaji wapiga kura kulikuwa na zogo. Madai ni kwamba kituoni hapo imebainika mashine moja ya BVR imeonesha imeshakuwa na majina 1000 ya wapiga kura katika kituo hicho wakati ilikuwa ndio kwanza mtu wa kwanza anaandikishwa kituoni hapo.

Kama ni kweli kwamba machine zinakuwa tayari zimejazwa majina feki ya kituo husika kabla ya kuandikwa majina halisi wa kituo husika; hili ni jambo la hatari sana kwa mustakabali wa demokrasia na amani ya taifa hili.

ANGALIZO: Tuwe makini kwa taarifa kama hizi LAKINI pia tusizipuuze.
Ni kweli kabisa zina kuwa na majina maana machine hizo zilitumika Mikoa /vituo vingine...kazi ya wakala ni kutunza kumbukumbu za kila siku mmeandikisha watu wangapi siyo kuangalia kwenye Database kuna watu wangapi..unaangaliaje kabla zoezi halijaanza mnakagua vitabu vyafomu ambacho kila Kitabu kinafomu 50 kila mkimaliza unaandika Kitabu namba ili mwisho Wa siku ujue Ni fomu ngapi zimetumika..
 
mwl. mziray

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
598
500
mashine hizi zimetoka kutumika mikoani ila inategemea kama hayo majina 1000 yaliandikwa eneo/mtaa huohuo ambapo ndo mtu wa kwanza alikuwa anaanza kuandikishwa ni hatari tupu.
Yani hii serikali ni pasua kichwa balaa
 
punguzo

Member
Jul 9, 2011
51
0
Hilo linawezekana, tena kirahisi sana kuingiza majina fake kwenye database. Kimsingi swali hiyo database ipo inasimamiwa na nani? Na hao waandikishaji wamepewa uhuru kiasi gani wa kuingiza majina kwenye database
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom