Je ni kweli bima watalipa kwa ajali iliyosababishwa kwa uzembe wa dereva?

Indungu

Senior Member
Nov 1, 2013
172
37
Wasalaam wakuu
Naomba msaada wa kisheria juu ya ajali ya gari iliyosababishwa na uzembe wa dereva,

Kuna mtu kagonga gari ya jamaa yangu akiwa kwenye speed Kali ya 130+,
Yani kaigonga na kuiharibu vibaya kiasi kwamba haiwezi tengenezeka tena,

Kinachotakiwa ni kulipa gari mpya na mgongaji anasema bima italipa
Je ni kweli bima watalipa kwa ajali iliyosababishwa kwa uzembe wa dereva?maana nimeona kuna figisu zinanukia juu ya jambo hili

Ni hayo tu ndugu zangu naomba kufahamishwa asanteni
 
Bima ndio kazi zake hizo haijalishi ulikuwa speed gani hata kama ulipanga kujiua inalipa tu kasoro gari lihalibiwe kwenye Maandamano au Fujo ikapondwa pondwa au kuchomwa moto hapo Bima haihusiki.

Bima Kubwa inalipa mgongwaji na mgongaji ila Bima ndogo inalipa mgongwaji iwe kwa miguu au ana gari ,pikipiki, au Nguzo ,Nyumba n.k Bima inalipa tu sheshe kwa chombo chako tu wewe ukiumia unalipwa matibabu ila yana kiwango chake hata kifo pia inakiwango chake
 
Back
Top Bottom