Je, ni kweli akina Halima Mdee wanaasisi chama kipya cha Siasa mbadala wa CHADEMA?

Ni haki yao, hofu yangu tu ni kuwa wameshapoteza mvuto wa kisiasa kwa sasa.
 
Mavyama meeengi ya nini wakati hata vyama vilivyopo havijaweza kukidhi haja za watanzania.
Chama gani kipo kwaajili ya kukidhi haja za watanzania!! Ajira za watu hizo, wachumia tumbo tu.
 
Mgaya naona akina Mzee mdee wanataka kuunda CCM C , . Muda ni wakati!
 
Taarifa ya kipuuzi.

Ungesema kuwa kuna watu wanaasisi chama kipya cha kisiasa. Hiyo ya kusema mbadala wa chama fulani ni ujinga. Hakuna chama kimachoasisiwa ili kuwa mbadala wa chama kingine, kama vile hakuna binadamu anayezaliwa mbadala wa mtu mwingine.
 
Kwahiyo CCM kimeumbwa kuwa chama tawala milele.

Una akili sana wewe kijana!
 
Tatizo la Zitto Kabwe aliendekeza ukigoma!
 
Ni haki yao kikatiba, kikubwa watimize matakwa ya kisheria
 

Wakati Zito anaanzisha ACT kwa mgongo wa ccm alikuwa na matarajio makubwa, ila hadi muda huu anategemea back up ya wapemba kutokana na mgogoro wa CUF. Huku bara ameshindwa kutoboa. Hicho chama cha system kimepigiwa debe muda huku mitandaoni, lakini hakuna uhakika wa kutoboa. Hiki sio kizazi cha kuchaguliwa mke, bali watu wanachagua wenyewe.
 
Hivi unadhani kuanzisha chama Ni rahisi kihivyo? Watu wanadhan ukianzisha chama tu Kama umejitoa chadema Basi unapata wanachama tuu. Jaribuni muone na hivi watz walivyokata tamaa na siasa za bongo ndo kabisaa
 
Hakuna chama mbadala kwa Chadema Bwashee. Wasaliti watabaki kuwa ni WASALITI tu kwa Watanzania wengi wanaojitambua.

 
Kabisa Mkuu hata kule Zenj baadhi wameshaanza kumstukia ayatollah Zitto kwamba kipaumbele chake ni madaraka tu. Kama mtakumbuka Act wasaliti walitishia kujitoa kwenye Serikali ya umoja haramu kama uchaguzi wa jimbo la Konde hautarudiwa cha ajabu hawajawahi kutishia kujitoa kwa wale waliopigwa na kuumizwa, kutiwa vilema au kuuawa kutolipwa fidia zao.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…