Je, ni kwanini viwanda vya mifuko ya plastiki havifungiwi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
38,183
44,276
16.jpg
Kwa sasa serikali imefanya juhudi kubwa sana za kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki, hii ni baada ya kuongeza kiwango cha chini cha unene kinachoruhusiwa kutengenezwa kutoka maikroni 30 hadi kufikia maikroni 50. Ila hii haitoshi, inabidi lile agizo lililotolewa na Rais wa dar mh. Paul Makonda la kuvifungia viwanda vyote vya mifuko hiyo ndani ya mkoa wa Dar litekelezwe mada moja na lifanywe kiwa sheria ya kudumu!

Uchafuzi wa mazingira unaotokana na mifuko hii hauvumiliki hata kidogo, vibebeo mbadala na rafiki kwa mazingira kama vikapu haviwezi kukua wala kuimarika endapo mifuko hii ya bei rahisi itaendelea kuzalishwa, tusiishie kwenye viroba tu!
======================================
UPDATE: (15/08/2017)
Mifuko ya plastiki = TAKA ZA MAKAMBA

=================================
Update: 09/04/2019
Mifuko ya plastiki imepigwa marufuku nchi nzima!

hii ishu wakuu wa mikoa au wilaya wakiikurupukia itaisha mara moja. mifuko inakera sana mijini. ila nahisi kuna rushwa na siasa ndiyomaana havifungwi.
 
View attachment 476101 Kwa sasa serikali imefanya juhudi kubwa sana za kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki, hii ni baada ya kuongeza kiwango cha chini cha unene kinachoruhusiwa kutengenezwa kutoka maikroni 30 hadi kufikia maikroni 50. Ila hii haitoshi, inabidi lile agizo lililotolewa na Rais wa dar mh. Paul Makonda la kuvifungia viwanda vyote vya mifuko hiyo ndani ya mkoa wa Dar litekelezwe mada moja na lifanywe kiwa sheria ya kudumu!

Uchafuzi wa mazingira unaotokana na mifuko hii hauvumiliki hata kidogo, vibebeo mbadala na rafiki kwa mazingira kama vikapu haviwezi kukua wala kuimarika endapo mifuko hii ya bei rahisi itaendelea kuzalishwa, tusiishie kwenye viroba tu!
Hata sigara hazifai
 
hii ishu wakuu wa mikoa au wilaya wakiikurupukia itaisha mara moja. mifuko inakera sana mijini. ila nahisi kuna rushwa na siasa ndiyomaana havifungwi.
Inawezekana, lakini mkuu wa mkoa si aloshalitolea tamko, kwanini anashindwa kusimamia utekelezaji wake kama Makamba alivyofanya kwa vifungashio vya pombe aina ya kiroba?
 
Inawezekana, lakini mkuu wa mkoa si aloshalitolea tamko, kwanini anashindwa kusimamia utekelezaji wake kama Makamba alivyofanya kwa vifungashio vya pombe aina ya kiroba?
inaonekana kuna nguvu zaidi ya RC inafanya kazi. kuna naibu alisema eti kama kuna mtu anawajua watengenezaji apeleke taarifa! eti hawawajui watengenezaji!? inaonekana ni dili ya wezi (wakubwa). ila ikifanikiwa itapunguza hata 2/3 ya uchafu mijini.
 
hii ishu wakuu wa mikoa au wilaya wakiikurupukia itaisha mara moja. mifuko inakera sana mijini. ila nahisi kuna rushwa na siasa ndiyomaana havifungwi.

Kwa kweli mifuko ya plastiki ni kero kubwa. Mimi ningependa kuuliza kwanini January Makamba kadanganya wananchi? Alituambia kuwa hiyo mifuko ya plastiki ifikapo January 2017 itapigwa marufuku. Sasa kama hana ujasiri wa kufuatilia kwa karibu maamuzi yake, je angepewa urais ingekuwaje? Mimi naona hili suala apewe Paul Makonda, Kaka wa Maamuzi Magumu! January unatukera! Rwanda mbona wameweza fasta? Sisi vipi?
 
Mnataka vifungwe wenzenu walioajiriwa huko wakale polisi???

Kwani Rwanda waliofungiwa wanakula wapi? Hatuwezi kuendelea namna hiyo! Maamuzi magumu lazima yafanyike. Tutaendelea kupaaza sauti tu! Jumamosi hii nilichukia kweli kweli wakati naokota plastiki mtaani kwetu maji na kinyesi kikanidondokea miguuni! Naambiwa hiyo ndiyo kawaida kwa watu wanaokaa uswazi wasiokuwa na vyoo!
 
KWANN vifungwe? Nina mradi mzuri wa matumizi mazuri ya mifuko hiyo na km mradi huu hautachukuliwa kisiasa nakuambia hv Tanzania itakuwa ni nchi safi na hamtaona tena mifuko.

Changamoto niliyonayo naogopa kukutana na wanasiasa viongozi wa tz maana wengi hufanya siasa siasa na wanaweza jibinafisisha mradi huu mkubwa.

WITO.
Kwaaliye serious aje PM tujadili mradi huu kwanza kisha ntahitaji support ya kuweza kuuwakilisha shirika la mazingira la dunia ili nipate fund/ vifaa vya kuweza kuitumia hyo mifuko kuzalisha bidhaa itakayotumika nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mradi endelea kupursue lakini mpaka uweze kuwa realised itachukua muda. For the time being hivyo vifuko vya plastiki vifungwe. Tumechoka kuviona barabarani, tumechoka kuviona hospitalini, tumechoka kuviona mashuleni, tumechoka, tumechoka. Sasa hui mradi wako nakutakia kila la kheri. Ila kwa sasa we are FED UP! Wafunge tu hiyo biashara. Utakapofanikiwa na mradi wako basi InshAllah. For the time being hatudanganyiki. Tutajuaje kama wewe sio mdau wa wenye makampuni yanayotengeneza hiyo mifuko na unajaribu kutupa false hope? You can be anyone as far as we know! Makamba ametuahidi kufunga hayo maviwanda, he should keep his word!
 
Mi siyo Mmoja wao , nimeoza huu uzi nkajikuta nachangia lkn km huu mradi nilionao utafikia kiwango ninachokifikiria naimani hutaiona popote mifuko hyo maana ukiiona itakuwa sawa na mtu kuokota lulu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi siyo Mmoja wao , nimeoza huu uzi nkajikuta nachangia lkn km huu mradi nilionao utafikia kiwango ninachokifikiria naimani hutaiona popote mifuko hyo maana ukiiona itakuwa sawa na mtu kuokota lulu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo mradi wako kama ni kufanikiwa utafanikiwa awamu hii ya Uncle Magu. Ukimiss hii opportunity hautatekelezeka. Mimi nakushauri usikae nao mfukoni, na hakika kuna watu ambao wenye "network" zao ambao wataona uzi wako na kukulink na the "movers and the shakers" wa nchi hii. Nakutakia kila la kheri, na Mwenyezi Mungu akuongoze na kukuepusha na makanjanja wa mjini.
Kwa sasa humu JF kama kuna mtu wa karibu na Januari amshike sikio. Amwambie hatujasahau alituahidi Januari mwaka huu hiyo mifuko ya plastiki itakuwa historia na sasa anaoption ya kupursue idea yako ya kiwanda cha - i guess - cha kurecycle hizo plastiki.
Meanwhile January Makamba ang'atwe sikio, hatutaki maplastiki mitaani mwetu!!
 
Safi! JICHO LA BUNDI, kaka makamba muda ndo huu tafadhali tekeleza ahadi yako kuhusu mifuko ya plastic! hali ni mbaya sehemu kubwa ya miji yetu zimetawaliwa na mifuko ya plastic badala ya ukijani ni hatari.
Pia wananchi binafsi tupunguze matumizi ya hii mifuko ili tuue hii biashara taratibu kabla serikali haijatia nguvu zake katika hili jambo.

Kweli AbouZakariya, wananchi nao wanayo nafasi yao lakini aliyepewa dhamana ndiye dereva wa Meli hii, hawezi kukwepa jukumu lake! Akiamka yeye wananchi ni rahisi kufuata na kuhamasika. Hebu angalia jinsi Paul Makonda alivyopiga vita biashara ya Sheesha. Alikaza buti na huoni mtu akivuta Sheesha labda avutie chumbani kwake, tena kwa siri! Huku mitaani kwetu mambo ya kukaa kibarazani unajidunga sheesha Kwishni! Sasa huyo Januari Makamba anawaangusha wananchi. Januari amka Kaka, speedi yako ya konokono. Na mimi hili suala nalivalia njuga Walahi Januari sikuachi ng'o hata kama hakuna wa kuchangia nitapaaza sauti mwenyewe mpaka kieleweke! Fanya kampeni ya nguvu, basi anza japo na Kampeni ya "Ondoa Plastiki Mitaani". Hamasisha watu - kwani naona umeingia baridiiii na vita ya makampuni hayo ya plastiki! Sijui unamwogopa Kingunge gani?
Ongea na wakina Ruge wakupe airtime ya Kampeni y ako. Hata hili Kaka wa Kitanga utashindwa? Mimi Januari sikuachi! Hata kwa Gwajima nitaenda anipe sapoti ya kukuombea! Amka bwana!!!!!
 
Tafadhali wadau tupaze sauti kwa pamoja tupige vita matumizi ya mifuko ya plastic, kwani kunyamazia jambo hili ni kukubali kuendelea kuyaharibu mazingira yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapa nakumbushia tu kuwa Mwezi wa nne Mwaka 2016 hili ndiolo tamko lililotolewa kwa wananchi:
"SERIKALI imepiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, kuanzia Januari Mosi mwakani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipiga marufuku jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM).

Mwalongo alitaka kujua lini Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira itakaa na wadau wa mazingira kujadili suala la uzalishaji na matumizi ya mifuko hiyo ambayo imekuwa ikiongoza kwa uchafuzi wa mazingira.

January alisema sasa wanaendelea kufanya majadiliano kuhusu suala hilo na kwamba JANUARI MOSI MWAKANI itakuwa mwisho wa uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Awali, akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri katika ofisi hiyo, Luhaga Mpina alisema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wenye viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ambao wanakiuka sheria na taratibu zilizowekwa."

Sasa kama hayo hapo juu ndiyo yaliyoahidi kwenye Bunge letu Tukufu kwanini Januari anafanya Danganya Toto? Sasa imepita miezi NANE suala hili limewekwa uvunguni. Januari hatukuachi mpaka utuambie hivyo viwanda vinavyochafua mazingira vinafungwa! Haijalishi wameajiri watu wangapi suala lazima lifike mwisho. Hatuwezi kuendelea kuwa na mji uliozagaa viplastiki vyeusi kila mahali. Ushauri wa Bure - Wananchi wnaweza kubuni miradi hata mifuko inaweza kushonwa kutumia reject khanga na kutengeneza mifuko yenye mikono na kubebea bidhaa mbalimbalimadukani. Januari tunasubiri jibu lako. Hapa hakuna chenga hapa! Tunataka kuona unachokifanya kwenye suala hili.
 
Back
Top Bottom