Je, ni kwanini viwanda vya mifuko ya plastiki havifungiwi?

Havifungiwi kwa sababu, vilifunguliwa kisha milango ikang'olewa na ikatunzwa kwenye mifuko ya vigogo wa awamu zile mbili zilizopita.

Hii comment, imeniponyoka rohoni ikadondokea kwenye hii keyboard.
 
Kwa kweli mifuko ya plastiki ni kero kubwa. Mimi ningependa kuuliza kwanini January Makamba kadanganya wananchi? Alituambia kuwa hiyo mifuko ya plastiki ifikapo January 2017 itapigwa marufuku. Sasa kama hana ujasiri wa kufuatilia kwa karibu maamuzi yake, je angepewa urais ingekuwaje? Mimi naona hili suala apewe Paul Makonda, Kaka wa Maamuzi Magumu! January unatukera! Rwanda mbona wameweza fasta? Sisi vipi?
akipewa makonda litaishia dar pekee
 
akipewa makonda litaishia dar pekee
Nguvu Dar ndio Kioo cha Jamii. Bora tu Makonda abebeshwe hili zigo halafu hao wengine wafuate. Lakini Dar ndio mboni ya Jicho. Januari anafaa kupewa Desk la kuandika Hotuba za Rais lakini hana nyongo ya kupambana na wenye viwanda vya Laana. Vijana wa TISS najua mko humu hebu fikisheni ujumbe kwa Uncle Magu mwambie Januari amrudishe Ikulu abaki anaandika Hotuba hii kazi na nginjenginje awaachie watoto wa Mjini wakina Makonda na Gama. Hapo ndio utaona kazi. La sivyo Januari apelekwe ulaya akatolewe nyongo. Ni operation ndogo sana huko ulaya. Akirudi atachuna sura ya mbuzi. TISS fikisheni malalamiko yetu kwa Uncle Magu, mwambie tumechoka na hivyo viwanda vya makanjanja.. Mi nashauri hizi taka tuziite "Taka za Januari". tusambaze kila mahari, kila mtoto, kijana, mzee anapoziona, waandishi wa habari wooote waziite "Taka za Januari". Labda hapo ndipo atakapoweza kuchukua hatua stahiki.
 
Huo mradi wako kama ni kufanikiwa utafanikiwa awamu hii ya Uncle Magu. Ukimiss hii opportunity hautatekelezeka. Mimi nakushauri usikae nao mfukoni, na hakika kuna watu ambao wenye "network" zao ambao wataona uzi wako na kukulink na the "movers and the shakers" wa nchi hii. Nakutakia kila la kheri, na Mwenyezi Mungu akuongoze na kukuepusha na makanjanja wa mjini.
Kwa sasa humu JF kama kuna mtu wa karibu na Januari amshike sikio. Amwambie hatujasahau alituahidi Januari mwaka huu hiyo mifuko ya plastiki itakuwa historia na sasa anaoption ya kupursue idea yako ya kiwanda cha - i guess - cha kurecycle hizo plastiki.
Meanwhile January Makamba ang'atwe sikio, hatutaki maplastiki mitaani mwetu!!
Ooh jaman km kuna MTU humu anaweza kunikutanisha na January afanye hivyo huu mradi ni mzuri na mkubwa mno utafanya hyo mifuko isionekane popote binafsi huwa inanichefua sana. Tafadhalini wadau nahitaji kupata pakuanzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nakumbushia tu kuwa Mwezi wa nne Mwaka 2016 hili ndiolo tamko lililotolewa kwa wananchi:
"SERIKALI imepiga marufuku uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, kuanzia Januari Mosi mwakani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipiga marufuku jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM).

Mwalongo alitaka kujua lini Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira itakaa na wadau wa mazingira kujadili suala la uzalishaji na matumizi ya mifuko hiyo ambayo imekuwa ikiongoza kwa uchafuzi wa mazingira.

January alisema sasa wanaendelea kufanya majadiliano kuhusu suala hilo na kwamba JANUARI MOSI MWAKANI itakuwa mwisho wa uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Awali, akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri katika ofisi hiyo, Luhaga Mpina alisema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wenye viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ambao wanakiuka sheria na taratibu zilizowekwa."

Sasa kama hayo hapo juu ndiyo yaliyoahidi kwenye Bunge letu Tukufu kwanini Januari anafanya Danganya Toto? Sasa imepita miezi NANE suala hili limewekwa uvunguni. Januari hatukuachi mpaka utuambie hivyo viwanda vinavyochafua mazingira vinafungwa! Haijalishi wameajiri watu wangapi suala lazima lifike mwisho. Hatuwezi kuendelea kuwa na mji uliozagaa viplastiki vyeusi kila mahali. Ushauri wa Bure - Wananchi wnaweza kubuni miradi hata mifuko inaweza kushonwa kutumia reject khanga na kutengeneza mifuko yenye mikono na kubebea bidhaa mbalimbalimadukani. Januari tunasubiri jibu lako. Hapa hakuna chenga hapa! Tunataka kuona unachokifanya kwenye suala hili.
Huwa inaniuma sana pale unapoona viongozi ambao wanaweza kuongoza wakitoa matamko bila kuwa na njia mbadala. Nilijua hawez tekeleza maana hana njia mbadala. ..nipo hapa Nina Njia mbadala na rahisi kuifanya mifuko hyo iwe lulu kubwa nchini.

Mwenye kunilink na January tafadhalii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ooh jaman km kuna MTU humu anaweza kunikutanisha na January afanye hivyo huu mradi ni mzuri na mkubwa mno utafanya hyo mifuko isionekane popote binafsi huwa inanichefua sana. Tafadhalini wadau nahitaji kupata pakuanzia

Sent using Jamii Forums mobile app

Wiser1, Mimi nakushauri uonane na Katibu Mkuu, Wizara ya Mazingira Prof Faustin Kamuzora japo most of the time yuko Dodoma. Fanya appointment kupitia Secretary wake anaitwa Mage huko Dodoma, Tel: (026)235 20 38 or mvizie akiwa Dar: 211 69 95. Itafaa uongee nae direct, siku hizi kuwaona wakuu sio shida sana kama enzi hizo.
 
Shukran mkuu ntafanyia kazi ushauri wako na ntaleta mrejesho kadri ntakapopata nafasi hyo. Asante mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran mkuu ntafanyia kazi ushauri wako na ntaleta mrejesho kadri ntakapopata nafasi hyo. Asante mno

Sent using Jamii Forums mobile app
Wiser1, Good Luck! utaingia kwenye Guiness Books of Record iwapo utafanikiwa kuzi-recycle hizi "Taka za Januari".

Ishu nyingine - itabidi wadau tupaaze sauti kuhusu miziki inayopiga maeneo ya makazi ya watu hasa ile inayokesha hadi asubuhi, walokole wanapiga sana mayowe, na mabaa uswahilini mwetu mitetemo nayo imezidi! - hili nalo kero tupu! Je Wiser1 unaubunifu wowote kwa hili?
 
Makonda akiweza kutatua hii changamoto.... nitaamini kweli wale viongoz ni wapumbavu.... juz mkuu wa mkoa wa karibu na ziwa victoria alimuaaibisha sana waziri wa wavinda...

Wa hapahapa Personally mimi ninaimani 100% kuwa Makonda akipewa rungu anaweza kutatua tatizo hili. Simwoni kiongozi yoyote jasiri. Trust me on this one. Jamaa anangozi ya mamba!
 
Makonda akiweza kutatua hii changamoto.... nitaamini kweli wale viongoz ni wapumbavu.... juz mkuu wa mkoa wa karibu na ziwa victoria alimuaaibisha sana waziri wa wavinda...

Wa hapahapa option nyingine ni kumwona Makonda. Ninaimani kabisa ukiweza kumwona Makonda na kumshirikisha idea yako hata chelewa kukupa support, after all hata yeye anataka jiji lake liwe safi. Inavyoelekea kuna nguvu kubwa inayofanya issue ya mifuko ya plastiki lisishughulikiwe ipasavyo once and for all. Sasa kwa vile adea yako inaweza ku-recycle hizo plastiki (hasa hizo plaqstiki nyeusi ) basi nenda kamwone Makonda anaweza kusaidia. Dodoma labda itakuwa mbali wewe kwenda anza na Makonda for fast tracking.
 
Serikali ilitoa tamko rasmi lakini bado kimya ila kwenye Viroba walipewa siku 14 tu. Mpaka wengine wakajipiga risasi. Ukiona kimya ujue kuna mwenzao bado yupo kwenye system na mmiliki wa kiwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ilitoa tamko rasmi lakini bado kimya ila kwenye Viroba walipewa siku 14 tu. Mpaka wengine wakajipiga risasi. Ukiona kimya ujue kuna mwenzao bado yupo kwenye system na mmiliki wa kiwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app

umenikumbusha kitu hivi karibuni Rais alimchagua

Sasa umenikumbusha, hivi karibuni Mh. Rais alimteua Ali Mufuruki kuwa Mwenyekiti wa National Environment Trust Board. Sasa najiuliza Ali Mifuruki namheshimu sana sana. Ila na yeye anakiwanda cha Plastiki sasa kwa madaraka hayo ya Uenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Mazingira anawezaje kukubali kufunga kiwanda chake?? Hapa napo mtihani aisee! Kama mradi wa Wiser1 wa kurecycle hizo plastiki utakosa support, itakuwa ni shida!
 
Marufuku ya kwanza kabisa ilikua kule zanzibar miaka ya mwanzoni ya Dr shein. Sina hakika kama kule walifanikiwa.Mifuko inatuathiri sana wafugaji. Nimepoteza ndama si chini ya kumi 2yrs.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marufuku ya kwanza kabisa ilikua kule zanzibar miaka ya mwanzoni ya Dr shein. Sina hakika kama kule walifanikiwa.Mifuko inatuathiri sana wafugaji. Nimepoteza ndama si chini ya kumi 2yrs.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pole sana JETM, Sisi kule uswazi kwetu kila tukifanya usafi watu tunakutana na lundo la mifuko ya platiki imetupwa ovyo yote yana vinyesi! Ikifika Jumamosi siku ya kufanya kazi ni shida. Kwa kweli wananchi tumechoka sana. Mimi najiuliza hivi Januari nyumbani kwake kuna mifuko myeusi ya platiki yenye vinyesi? Je amewahi kuokota mifuko ya plastiki barabarani yenye vinyesi? Ndugu zangu wa TISS hebu mwambie Uncle Magu hili suala halikubaliki. Mitaro imejaa mifuko ya platiki, mashamba yetu yamejaa mifuko ya plastiki, sasa mifuko hiyo ndiyo imekuwa inahifadhi vinyesi!! Sasa fikiria maumivu uliyoyapata kupoteza ndama kumi na mbili!! Haikubaliki hii jmani lazima tuendelee kupaza sauti.
 
Back
Top Bottom