Je, ni kampuni ipi inaongoza kwa huduma bora za kuagiza magari ya nje hapa Tanzania

Huduma kwa wateja ni mbovu mno, lugha chafu, hasa kutoka kwa waswahili wenzetu walioko huko Japan, kama kawaida yetu kutaka kukomoana kisa kuna taarifa hukuiona katika mlolongo wa barua pepe zao, ukiuliza inakuwa nongwa. Sijui hata wanafikiri nini kuwa katika nafasi walizonazo.
Pengine ilinitokea mimi tu, ninachoeleza ni uzoefu wangu kwa mara (moja)ya kwanza kuwatumia beforward. Kama nitawatumia tena, sina uhakika.
 
Beforward hawa au siyo?
 
Ha haaaa.. We jamaa bhana.. Aliyekuambia watu wanafunga ndoa na magari nani? Nunua tumia uza.. Nunua tumia uza.. Nunua tumia uza...
Hahah sawa mkuu,maana naona watu hua wanatangaza kuuza magari yao humu jf unawaambia hilo gari kama litakuwepo mpk wiki ijayo ntalinunua sasa nikajua bado hujanunua aisee.
 
Autocom inakidhi vigezo #1 hadi #5

Pia kizuri zaidi kuhusu Autocom ni kuwa mmoja kati ya wafanyakazi wake hapa TZ ni active member wa JF ni huyu ndugu renyo .

Mwl.RCT , una real experience with Autocom Japan? I mean ushawahi kuagiza gari kupitia Autocom Japan?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…