Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,512
- 16,735
We ni dini gani.Kwetu huyo ni halali yako.Kuna binamu yangu ambaye nimetokea kumpenda sana, mtoto wa shangazi yangu mama yake na baba yangu wana mama mmoja wa baba tofauti.
Uyo shangazi ana mtoto wake wakike nampenda sana mpaka inafika kipindi sasa nashindwa kudhibiti hisia zangu, naona ni waite wazazi niwambie ukweli kuwa nimetokea kumpenda mtoto wa shangazi yangu, na nataka kuoa.
Je, ni halali kweli mtu kuoa binamu yake au ni maneno tu ya kijiweni?
Nisije jikoroga huko!
Sisi kwetu kila kitu kipo kisharia.Aya zinazotuongoza hapo ni hizi na angalia kama huyo hayupo hapo ndio ni halali yako
Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu; isipokuwa yale yaliyokwishapita. Bila shaka jambo hili ni uovu na chukizo na ni njia mbaya (kabisa). Mmeharamishiwa (kuoa) mama zenu, watoto wenu, dada zenu, shangazi zenu, ndugu za mama zenu, watoto wa ndugu zenu, watoto wa dada zenu, na mama zenu waliowanyonyesheni, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, walio zaliwa na wake zenu mliowaingilia. Lakini kama nyinyi hamjawaingilia basi si vibaya kwenu (kuwaoa). Na mmeharamishiwa wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na (mmeharamishiwa) kuwaoa madada wawili wakati mmoja, isipokuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kurehemu na Mwenye kusamehe. (4:22-23)."Na pia mmeharamishiwa wanawake wenye (waume zao) isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ndiyo Sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) minghairiya hawa..." (4:-24)