Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Kumekuwa na wimbi kubwa hususani Tanzania la baadhi ya watu na viongozi kumshukuru Rais kwenye mambo ambayo yametendwa na Raia.
Mfano Jana Usiku imepigwa mechi baina ya Tanzania na Algeria kwenye michuano ya kufuzu Afcon kwenda Nchini Ivory Coast (Cote D'Ivoire). Lakini cha kushangaza Sifa zote zinamwagwa kwa Rais. Tazama post ya Mbunge "Babu Tale" hapo chini.
Huu upuuzi uwezi kuuona Nchi zilizoendelea, hata hapo Kenya uwezi kuona huu upuuzi kwamba Wananchi wanafanya kazi yao, alafu Sifa zinaenda kwa Rais. Marekani au Uingereza uwezi kuona Timu ya taifa inashinda alafu Wananchi wanasema "We thank president Joe Biden" au "We thank Queen Elizabeth". Hata Kenya ni nadra sana kuona rais anapongezwa kwa kitu kilichofanywa na Raia.
Ikumbukwe kusema neno "Asante Rais kwa kufanya hivi" ni kama vile Rais ametoa msaada, wakati kiuhalisia hile ni nguvu ya Umma. Chochote anachofanya Rais ni Mali ya Umma, hata Fedha anazotoa ni Mali ya umma. Anachofanya Rais sio msaada bali ni wajibu wake kama Rais, kama vile Mwalimu anavyofundisha, Mwenyekiti wa mtaa anavyosaidia mtaa, Daktari anavyotibu na jinsi ilivyo kwa watumishi wengine wa serikali. Kitendo cha kusema asante Rais kwa kitu fulani, utafikiri asingekuwepo yeye tusingeweza ni ujinga wa watanzania ndio maana wanasiasa wanaendelea kujifanya miungu watu, kwa sababu wanapokea sifa ambazo kimsingi ni wajibu wao na kazi yao kuyafanya hayo kama ilivyo kwa watumishi wengine. Ndio maana hizi Asante uwezi kuziona kwenye Nchi zinazotambua Wajibu na Kazi (Duty and Responsibility) ya Raisi.
Pesa tumpatie sisi kupitia kodi, na akifanya maendeleo kwa Kodi zetu, tunaanza kumramba miguu na kusema Asante. Utafikiri Pesa ni zake, au alichofanya ni msaada. Rais anakuja kutuomba kura ili akatekeleze haya anayoyafanya, ni moj ya majukumu yake ambayo ndio yamemuweka madarakani na hasipoweza kuyafanya hayo basi ataondolewa madarakani kwa kushindwa kuyafanya. Hivi ndivyo nchi za demokrasia ufanya kazi, na si kushukuru serikali wakati ni wajibu wake kuwezesha kila sekta kupiga hatua.

kwenye sekta ya michezo tumeona ndani ya mwaka mmoja namna ambavyo mama umefanikiwa.. Tuliiona Simba ikicheza Robo fainal CLUB BINGWA AFRICA na tukashuhudia Yanga akicheza FAINAL KOMBE LA SHIRIKISHO.. nasasa tunaenda kuiona Taifa stars ikiwa ni miongoni mwa timu 24 zitakazo wakilisha mataifa yao pale IVORY COAST/kiukweli Mama unaupiga mwingi kutokana na hamasa yako kwenye mpira wetu.. nikiwa kama mdau wasoka naanza kukupongeza wewe.. naipongeza TFF ikiongozwa na Karia..
Nawapongeza wachezaji wetu,navipongeza vyombo vya habari vyote vya hapa nyumbani.. namwisho nawapongeza wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwanamna ambavyo wanaendelea kuisapot timu yao..