Je, ni haki Mapadre kuacha kuoa

Je, ni haki Mapadre kuacha kuoa

Hodar

Member
Joined
Oct 27, 2018
Posts
16
Reaction score
8
Wanaopinga swala la mapdre kuacha kuoa nawashangaa sana je wamewahi kusoma haya maandiko yanayoelezea msimamo wa Yesu na Paulo katika vitabu hivi;

Maneno ya Paulo Mtume:
1Wakorintho 7:1.8
"Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo"

Maneno ya Yesu mwenyewe:
Mathayo 19:10-12,
"Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutoa kabisa.Lakini Yeye akawaambia 'si wote wawezao kulipokea neno hilo, ila tu wale waliojaliwa, maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako MATOWASHI waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako MATOWASHI WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI. Mapadre wameamua kujifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
 
Kesi za ulawiti ni nying sana kwa hao hao Matowashi wa kujifanya. Ok ishu za dini ni pana sana, no battle.
 
Kesi za ulawiti ni nying sana kwa hao hao Matowashi wa kujifanya. Ok ishu za dini ni pana sana, no battle.
Mtu anayewapinga anaweza kutumia sababu kama yako hiyo japo ukweli ni kwamba unaweza ukakuta ni wanne miongoni mwa watu mia ndo wanafanya hivyo, hatutegemei kuwa wawe wasafi kama malaika, wao ni binadamu tena wametokea kwenye jamii hizi hizi tunazozijua. Lazima watakuwepo waliotaka kuwa matowashi wa aina hiyo lakini mbele safari wameshindwa, sasa tukisema tuchukue mifano michache ya walioshindwa eti ndo tuwawekee wote itakuwa sio sahihi.
 
Maisha ya mwingine yasiyohathiri mfumo wako wa kuishi yanawasumbua nini

Ishi utakavyo wewe maisha yako ya wengine yaache
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom