Je, ndoa hii nani mkosaji?

Mkuu mchumba sikumwacha maksudi,nilipompa mimba huyu mwanamke sikuona sababu ya kumtelekeza,nimelelewa maisha mabaya saana sikutaka kumtesa mtu,by the way nimekuja kuombe ushauri hujamaliza na conclusion nn nifanye.

Mimba haifanyi mtu umpende, na hata yeye kuwa na mimba haikuwa warranti ya wewe akupende.Busara , fikra ilikuwa lazima isimame kwenye shati nako ni kuachana naye ila ulee mimba na mtoto, Hapi hakuna ndoa kubali ulikosea achana naye jipange uanze maisha mapya na wanaokipenda
 
Chozi la mtu aliyetendwa,ni uchawi mkubwa,sisi wachawi tunaamini mtu ukimfanyia ubaya utakurudia mara tatu.mchawi wako ni mpenz wako wa mwanzoni, mtafute umuombe msamaha
 
Kama mlifunga ndoa huo ndio msalaba wako uliopangiwa duniani kufa nao. Ndoa za kanisani hazivunjwi. Sikushauri kuachana kwa kuwa gharama za kuachana ni kubwa kuliko mkiwa pamoja. Komaa mkeo akikua ataacha

Ushauri mwingine wa kimtaani uswahilini ile mbaya: Nenda Kilwa mtafute mzee Makongonyongo akutengenezee tego la pozo, mtu akimtongoza mkeo wakikubaliana akienda nae chumbani au popote pale dudu linasinyaa na halisimami mpka aje kukuomba msamaha.
 
Mdau unajisikiaje kuongea pumba, jukwaa kimsingi ninmahala pakuzungumzia mambo yenye upe uliochanya na si vinginevyo kikatiba , ni kinyume kuua maana kila mwanadamu ana haki ya kuishi, pia kwenye penal code kuua ni kosa.Kwahiyo kumchochea aue huoni unashiriki kosa na ni kinyume cha sheria?amekuomba ushauri nadhani hakutaraji negative alstitude ndo uwe ushauri, omba radhi mdau .mambo ya kijinga si ya kushabikia
 
Sio kila ushauri lzm aufanyie kazi ,anaweza asiufuate na akafanya maamuzi yake binafsi,kwa sababu mamb ya ndoa yanasehem zake za ushauri, kwani wkt anamuach mpenzi wak wa zaman aliomb ushaur,si yenyew aliamua, wengi huomb u wkt walishaharib,
 
Pole sana mkuu,huyo sio mke mwema tafuta namna muachane tu atakutesa maisha yako yote mkuu.
 
My dear hapo hamna ushauri ushaur unao mwenyewe coz unamjua zaid ya ulivoandika maamuz unayo wala ndugu ama jiran ama jamaa hawez kukushauri fanya maamuz yakiume ambapo hutajutia maisha yako yote
 
Bro binafsi nakushauri huo mzigo utakutoa uhai. Kung'uta mavumbi nenda zako. Achana kabisa na huyo mwanamke nakuomba sana na bila shaka mtoto ni mkubwa hivyo fanya mipango namna utakavyomlea mwanao
 
Kosa sio kosa, mpaka pale tunapokubali kurudia maumivu tukidhani hatutoumia tena... ndo tunapojua kua tumekosea.... kumbadilisha binadamu tabia ambayo kwake kashafanya kama ngozi ni jambo gumu sana'... na kama wewe ni mkristo jaribu kuweka ili swala kwenye maombi, au kama una amini katika imani yako ili mwenyezi Mungu akupe maamuzi yenye busara na sahihi... kwa akili za kibinadamu "uyo sio mke, mke mwema anaempenda na kumuheshimu vyema mme wake hawezi kufikia alipofikia mwenzi wako".... pole sana rafiki.
 
Bro binafsi nakushauri huo mzigo utakutoa uhai. Kung'uta mavumbi nenda zako. Achana kabisa na huyo mwanamke nakuomba sana na bila shaka mtoto ni mkubwa hivyo fanya mipango namna utakavyomlea mwanao
Sawa mkuu
 
Asante mkuu
 

Mi nilikuwa nasikia kuwa kuna limbwata tu kumbe kweli zipo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kaka kwa taarifa yako ni kuwa umewekwa kwenye chupa na usitegee kama utaweza kumwacha huyo
Labda ukaombewe ili chupa ivunjike uwe huru
 
Ninalia kwa ajili ya huyu mtoto atakayeachwa hapo.

Dah sijui niandike insha ngapi kuwaonya vijana..USIOTESHE SHAMBA LISILOKUWA LAKO...USIMWAGE MBEGU KWA SHAMBA USILOTAKA KUMILIKI.

Mtoto ni zaidi ya shamba la kukodi jamani. Hao watoto tunazalisha hovyo hakika kuna siku watakuja kutupiga wakikua wakubwa. Hawakuomba kuletwa kwenye dunia hii ilhali hamkujipanga.

Hebu ona sasa insha yote hujaongelea hata una mpango wa kufanya nini na mwanao ukishamuacha mamaye.

Tuache uzinzi jamani..haulipi kabisa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…