Si alisema hapo kuwa aliachana na huyo mchumba wake baada ya mke kuwa na mimba.Unaambiwa kosea kujenga na sio kuoa...
Bila kupepesa macho kosa ni lako wewe. Sijui huwa mnakuwa na maana gani kusema huyu mke hakuwa wa ndoto zangu, halafu bado ukamtia mimba na kumuoa. Huo ni upuuzi uliopitiliza.
Umesema mwanzoni kabisaa alikuwa a nawasiliana na ☓ halafu ulivyo na akili nyingii ukamwambia chagua mmoja, huku ukijua fika una mchumba wako umpendae mkuu hapo ndo ulianza kujipika mwenyewe....
Baadae mchumba wa ndoto zako akarudi, bado yule uliyempa nafasi ya kukuchagua unampa kipigo kitakatifu sababu tu eti ana wivu na wewe?????!
Maumivu yake yalianzia hapo sababu alijua fika humpendi na hilo ulimtamkia mwenyewe ingawa sio sahihi anavyolipiza kisasi lakini chanzo ni wewe apo...
Msiwe mnaendeshwa na hisia, fuata moyo wako. Huko kuna uliyempotezea muda kwa miaka 7,unafikiri machozi yake yatakuacha salama???!
Kaa na mkeo ongea nae na ikiwezekana mpe mipango yako ya talaka, sioni ndoa hapo mie naona mafahali wawili wako kwa boma moja
Nashangaa hadi leo bado anaifuga hii takataka tu.Pole xana mkuu,lakin nakushanga xana mwanaume kukosa maamuzi ya kiume,huyo mwanamke kashakuona ww hujielewi ndio maana anafanya tena makusdi,eti analipiza kisasi.Hiyo ndoa bado changa xana kaka na huyo mkeo ni gamba yafaa ulivue mapema.kilichobaki ni kumkuta mume mweza amelala kitandan pako,kwani huna house girl hapo wakuchukua nafasi yake?
Nafanya yote haya baada ya uvumilivu wangu kufika mwisho, yaan hapa naanda taaratibu za mwsho kabla sijamwonesha mlango wa kutokea.We umesema ndo Warudi nyumbani mida kama hii, unafikiri yeye anawaza ulikuwa wapi???
Yaani wote mmekaa kukomoana tuu!!!! Mkuu hakuna ndoa ya hivyo, na mwanamke haolewi kwa kigezo cha mimba. Usipoangalia mtaleteana magonjwa sasa
Mkuu nishamuomba radhi saaana na akaridhia, ila akasema hawezi olewa maaana hatatokea mwanaume wa kumwamni, yupo Bunda Mara kwa sasa kaajiriwa mamlaka ya mapato hataki kusikia kiumbe aitwae mwanaume.Tatizo hapo lipo kwenye agano mliloweka kwa binti yule aliyekuwa Kampala. Mtafute muombe radhi tena akiridhia yeye kukuachilia kabisa moyoni mwake bila kufikiri muda aliopoteza basi laana yake itakuachia maisha yako yatakuwa sawa kabisa na ndoa yako utaifurahia.
Nishaongea nae saana,kashakubali japo shingo upande.Ubaya nao ni mbegu huna budi kula mazao yake
Binti wa chio Kampala ndio kabeba hatma ya yote mtafute myamalize kiustaarabu ila sio kumuoa tena
Na hiyo ndoa vunja mapema hata Mungu anaelewa katupa ruhusa kuachana unapobainika uzinzi
Wanaume tumelogwa, wakati ukishafika ukamchoka mtu unamtafutia sababu zote mbaya ili kumtoa kasoro tu. Ulivyomuacha mchumba wako wa mwanzo unafikiri hakuumia? Nani alikudanganya ndoa inabadili tabia ya mtu?
Mkeo unamuonea tu, hiyo ndio tabia yake toka mnafahamiana hadi baada ya kuoana, hajabadilika chochote. Unatafuta sababu tu! Inaonyesha ulifikia maamuzi ya kumuoa kwa shinikizo la mimba tu.