kupelwa
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 1,087
- 450
Wote wako makini sana hawa vijana nashukuru namna wanavyopambana na chadema, sisi C C M tungepata mzee makamba akawa mkabala na Mzee Mukama wakashirikiana na hawa vijana makini wawili(Nape na Mwigulu) tungeshawamaliza kabisa Chadema. Hawa vijana wanapeleka chama chetu cha CCM vizuri sana
Kwa kasi ya mageuzi , nape na chemba hawaiwezi.Kuna kasi kubwa sana ya mageuzi na hoja mahususi za kukijenga chama.Ikumbukwe nape kapewa cheo hicho baada ya kutetewa na JK asifukuzwe chama na lowasa na nchimbi kwa ajili ya uropokaji wake.Chama ni sera na uongozi mzuri na sera ni lazima zitekelezeke, anayetekeleza sera ni serikali na si nape.Wakati huko serikalini nape hatakiwi kugusa masilahi ya wenyewe ambao walipendekeza kumfukuza chama.Pia JK kampa cheo ili anyamaze abwate ujinga lakini kukija maswala ya serikali asiguse .naye ndo anachokifanya.sasa atakuwa mchapa kazi kivipi wakati serikali inayotekeleza sera imeoza, na nape hapashwi kuigusa?chama cha ccm, kinatakiwa kuwa na wazee wenye sauti na falsafa tekelezi .Vinginevyo unaposema anachapa kazi , kwa muono wako labda anakufurahisha kwa comedi na uropokaji lakini chama ndo kinakufa.CCm mbona wapo wasomi wazuri tu wa maana wanaweza kujenga chama na si hao waropokaji, wakija kwenye namna ya kujenga chama wanaonekana mbwakoko wasio na sauti.changamkeni wazee na wadhamini wa chama kuingilia.