Je, Nape Nnauye na Mwigulu Nchemba ni mwiba mkali kwa vyama vya siasa au ni kansa inayoimaliza CCM .

Wote wako makini sana hawa vijana nashukuru namna wanavyopambana na chadema, sisi C C M tungepata mzee makamba akawa mkabala na Mzee Mukama wakashirikiana na hawa vijana makini wawili(Nape na Mwigulu) tungeshawamaliza kabisa Chadema. Hawa vijana wanapeleka chama chetu cha CCM vizuri sana

Kwa kasi ya mageuzi , nape na chemba hawaiwezi.Kuna kasi kubwa sana ya mageuzi na hoja mahususi za kukijenga chama.Ikumbukwe nape kapewa cheo hicho baada ya kutetewa na JK asifukuzwe chama na lowasa na nchimbi kwa ajili ya uropokaji wake.Chama ni sera na uongozi mzuri na sera ni lazima zitekelezeke, anayetekeleza sera ni serikali na si nape.Wakati huko serikalini nape hatakiwi kugusa masilahi ya wenyewe ambao walipendekeza kumfukuza chama.Pia JK kampa cheo ili anyamaze abwate ujinga lakini kukija maswala ya serikali asiguse .naye ndo anachokifanya.sasa atakuwa mchapa kazi kivipi wakati serikali inayotekeleza sera imeoza, na nape hapashwi kuigusa?chama cha ccm, kinatakiwa kuwa na wazee wenye sauti na falsafa tekelezi .Vinginevyo unaposema anachapa kazi , kwa muono wako labda anakufurahisha kwa comedi na uropokaji lakini chama ndo kinakufa.CCm mbona wapo wasomi wazuri tu wa maana wanaweza kujenga chama na si hao waropokaji, wakija kwenye namna ya kujenga chama wanaonekana mbwakoko wasio na sauti.changamkeni wazee na wadhamini wa chama kuingilia.
 
Nape hapendwi na wazee wa ccm he's a threat to them...Nape wants to get rid of all the old heads ccm kiwe ni chama cha vijana wazee wakapumzishwe sasa hapo mizee ya ccm inabif nae
 
Huyo Mwigulu sina habari zake ila huyu Nape naona ni Cancerous tumour inatakiwa inyofolewe mapema kabla 2015 isije ikasambaa sana ikaua chama cha jembe na nyundo maana huyu bwana Nape anahusudu sana makundi. Nilitegemea kwa position yake awe neutral.
 
Ngoma ikivuma sana, haikawii kupasuka. Debe tupu haliishi kuvuma. Mark my words, tunajua mantiki ni nini na show ni nini.

Na hapa kwa magarasha haya mawili hamna hata show, achilia mbali mantiki.
 
Nyie kina Nape na Mwigulu mkiwa pamoja ndio 0 kabisa. Nadhani mnajifagilia wenyewe mnajiona wajaanjaaa. Haya bana 2015 sio mbali.
 
Nape na mwigulu wanakiua chama manake badala ya wao kujibu hoja kwa busara nakutoa fact wao WANAROPOKA NA KUONGEA UONGO ILI CHAMA KIPENDWE NA KURUDISHA IMANI KWA RAIA. Hawana jipya hawa wote wana save interest zao na si za chama.
 
Nape na mwigulu ni wahujumu wa ccm wamekuwa kama mbwa wabwekao lakini hawana nguvu! Wanaiangamiza ccm! Kazi ni umalaya tu!!
 
Wanasadia kuimalizia CCM.

Jambo moja nina hakika nalo, ADUI YAKO AKIKUSIFIA, JAMBO HILO LIACHE MARA MOJA!!ADUI YAKO AKIPONDA JAMBO HILO NDIO SAWASAWA LISHIKE USILIACHE. sasa kwakuwa CDM na wapambe wao wanawaponda Nape na Mwigulu sana, hawa ndio CCM inapaswa kuwashika sana maana WANAWASUMBUA SANA UPINZANI.
 
wanataka kuimaliza chadema, then waimalize ccm halafu wabaki wao wawili tu waendelee kuitwa chama.
 
Kama hawana nguvu yeyote hebu hesabu threads za Nape na Mwigulu kwa siku moja.
 
Nap+Nchemb ni wasaidizi wa kuimarisha CDM, bila wao cdm hawatapata msukumo wa kuelimisha na kuwakomaza wananch kisiasa
 
Kwa wanaojua tz politics watakumbuka after o r mapuri kuchemka alikuwa gumzo! I think hawa ni gumzo kwa mfumo huo!
 
Sanasana mwigu yeye ndio mchemkaji kwa joto la kuyeyushia chuma! Hanaga point huyu dogo! Lakini mm nawapenda saana!
 
Nape huwa anajitahidi though ni mala chache anakuwa yupo sawa! Ila nae anachemkaga sometimes! Mpaka basi, ila ana nafuu
 
Jambo moja nina hakika nalo, ADUI YAKO AKIKUSIFIA, JAMBO HILO LIACHE MARA MOJA!!ADUI YAKO AKIPONDA JAMBO HILO NDIO SAWASAWA LISHIKE USILIACHE. sasa kwakuwa CDM na wapambe wao wanawaponda Nape na Mwigulu sana, hawa ndio CCM inapaswa kuwashika sana maana WANAWASUMBUA SANA UPINZANI.

Akili yako wala siishangai maana ina - undergo the principle of diminishing return kama ilivyo akili ya wana Mabwepande wenzako. Endeleeni na huo ulevi tu mtaisoma namba very very soon.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom