Je, nani anajua kama watanzania tunaibiwa kiasi hicho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, nani anajua kama watanzania tunaibiwa kiasi hicho!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Igembe Nsabo, May 22, 2012.

 1. I

  Igembe Nsabo Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Subscription Fee to Hello tunes, Je Serikali inapata kodi kutoka eneo hili?
  Ndugu zangu wana Janvi, Nillikuwa najaribu kufanya utafiti mdogo kuhusiana na mapato ya simu za mikononi na kuangalia namna Serikali yetu inavyokosa mapato hayo. Nimejaribu kuangalia eneo moja tu na ninategemea na wengine watakuja na maeneo mengine ili tujaribu kutoa maoni yetu:
  Eneo ambalo ninataka kuliangalia ni hili hapa: - “Charges za subscription fee to hello tune ya Shilingi za Kitanzania 210 kwa kila wiki na Monthly fee ya Shilingi za Kitanzania 400 kwa huduma hiyo”. Mtanzania wa kawaida ni vigumu sana kulielewa hili na ukiangalia kwa haraka haraka gharama hizi ni kidogo sana lakini ukifanya uchambuzi wa kina na kuoanisha na shughuli zingine au huduma zingine ambazo zinatozwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT -18%) utaona ni faida kiasi gani hawa watu wanapata bila kulipia kodi huduma hizi.
  Tufanye uchambuzi huu pamoja,
  A: Tuanze na huduma ya hello tune inayolipiwa shilingi 210 kwa wiki, Mwaka mzima una wiki 52 na tufanye assumption ya Air tel anawateja milioni tano tu (5,000,000) kati ya watanzania zaidi ya milioni 45 ambao wamejiunga na huduma hii. Maana yake ni kuwa Air tel anapata kiasi cha Shilingi za Kitanzania biilioni 54.6 kwa kilia mwaka kama mapato yatokanayo na hudua hii ya hello tune.(Rejea jedwali)
  B: Pili tuangalie pia huduma hiyo hiyo ya hello tune inalipiwa gharama nyingine ya shilingi 400 kwa mwezi. Assumption yetu ya wateja milioni tano iendelee. (Rejea jedwali)
  C: Jumla ya Mapato yote kwa huduma hiyo kwa mwaka, ni shilingi za Kitanzania 78.6 bilioni. (Rejea jedwali)
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 100%"]
  [TR]
  [TD="width: 100%, bgcolor: transparent, colspan: 5"]Jedwali: Mapato yatokanayo na Huduma ya Hello Tunes katika Simu
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 6%, bgcolor: transparent"]Na
  [/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]Gharama/Wiki
  [/TD]
  [TD="width: 23%, bgcolor: transparent"]Wiki /Mwaka
  [/TD]
  [TD="width: 18%, bgcolor: transparent"]Wateja
  [/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]Kiasi/Mwaka
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 6%, bgcolor: transparent"]1
  [/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]210
  [/TD]
  [TD="width: 23%, bgcolor: transparent"]52
  [/TD]
  [TD="width: 18%, bgcolor: transparent"]5,000,000
  [/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]54,600,000,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 6%, bgcolor: transparent"][/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]Gharama/Mwezi
  [/TD]
  [TD="width: 23%, bgcolor: transparent"]Miezi/Mwaka
  [/TD]
  [TD="width: 18%, bgcolor: transparent"]Wateja
  [/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]Kiasi/Mwaka
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 6%, bgcolor: transparent"]2
  [/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]400
  [/TD]
  [TD="width: 23%, bgcolor: transparent"]12
  [/TD]
  [TD="width: 18%, bgcolor: transparent"]5,000,000
  [/TD]
  [TD="width: 25%, bgcolor: transparent"]24,000,000,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 74%, colspan: 4"]Jumla Kuu/Mapato kwa mwaka
  [/TD]
  [TD="width: 25%"]78,600,000,000
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Kutokana na mapato hayo, ukiachilia mbali huduma zingine ambazo sitaki kuziongelea hapa kama vile huduma za M-Pesa, Tigo Pesa, Air tel Money, SMS, na huduma zingine nyingi tu ambazo ni chanzo cha mapato kwa kampuni hizi. Swali la kujiuliza hapa, Je Serikali yetu inapata kiasi gani kutokana na mapato hayo? au inaambulia patupu?. Inawezekana ukawa WIZI MTUPU!!!!
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  hapo huibiwi unawapelekea mwenyewe!!!
   
Loading...