Je, namba sifuri siyo namba ikisimama yenyewe?

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
7,918
13,391
Tukae kwa wana mahesabu wa hapa kwetu tusitegemee wingi wa mahesabu kutoka kwa wakuu wa mataifa tajiri ndani ya vikao vyao watuamulie kama sifuri inatosha kuitwa namba kamili ilihali ikisimama yenyewe haina chochote inacho wakilisha.

Wanahisabati wa ndani kwanini bado inahesabika kama namba kamili badala ya namba 7 iliyozoelewa na inayosadiwa hata kiimani kama imani zingine hampatani nazo je hadi yenu ile ya magharibi?

"Sifuri siyo namba kama ikisimama yenyewe" huu ni utaalamu niliowahi kukubaliana nao mfano 04 tunasema inawakilisha idadi ya vitu 4 tofauti na 70 inayowakilisha idadi ya vitu 70. Hata kwenye akidi ya vikao nyeti na wazi bado sifuri haiwezi kutumika kuwakilisha mjumbe asiyefika bali utasikia tu akidi haijatimia kwa ukosefu wa wajumbe labda 06 kati ya wajumbe 10, waliotengeneza akidi ya wajumbe 04 asilimia pungufu ya 50% ni 49-% je ni halali kuendelea na kikao?

Sijasahau mahesabu ya mwalimu wangu pale shule ya msingi aliyeniambia na kunielewesha kwa maneno mawili "Mpe" na "Mtoe" aliyenifundisha kuwa namba ni utambulisho wa idadi ya vitu kama ndivyo je sifuri ni utambulisho wa vitu gani na vingapi ikisimama yenyewe?, jibu li wazi si utambulisho wa idada ya vitu vyovyote bali hewa. Ndiyo ni hewa na hewa ndio chanzo cha uhai wowote.
 
Ni utambulisho wa hewa inamaana ni hakuna kitu mkuu,binafsi sifuri ikikaa kushoto mwa namba ni kama inathibitisha namba hiyo ii pekee yaani haijafikia makumi.. ila ikikaa kulia inaongeza thamani..
 
Sifuri ni namba kamili

Inatambulika ikisimama yenyewe

Uzito wake utategemea na position ilipo kwenye namba husika

Katika principles za mathematics kuna discrete na integral summation,

Unapojumlisha discrete namba kutoka 0 to 1 utapata just 0+1

Lakini ukitumia integral summation from 0 to 1 hapa utazihusisha hadi pia zile small values like 0.1, 0.01, 0.001, 0.2, 0.002 n.k

So uzito wa namba sifuri utategemea pia ni mfumo gani wa argeibric au mathematics unaoutumia kupata unachokitaka

Tukija kwenye trigonometry pia sifuri au zero ina thamani yake tena kubwa tu, sin 0 ni 0 but cosiness ya 0 ni 1, umejiuliza why? okay tuachane na hili

Njoo kwenye differentiation, hapa zero inacheza kama constant zote na ni zao la differentiation of constant so zero ni namba na inasimama yenyewe kama yenyewe

Zero ni namba ambayo kimahesabu tunasema no count have made, yaani bado haujamake step

Yaani kwamfano una namba x, hii namba itaendelea kuwa x kama x if no any additional itafanyika it means kwa lugha nyingine kama uta add 0, you see...??? Zero kama zero bado inasimama yenyewe kama yenyewe hapo

Sisi ma engineer tunaithamini sana zero because inatusaidia Sanaa kwenye issue nyingi, kwa mfano;

1. Inakuwa kama reference level kama una deal na issue za elevation, Mfano reservoir, ( maswlaa ya maji) the lowest point ambayo maji yatakuwa hayaflow tunaiterm kama zero elevation, consider elevation from the sea level

Sea level tunaiterm kama zero reference level, you see zero ina umuhimu sanaa na ndo mana from this reference level tunaweza kupata kujua muinuko wa mlima, mti,jengo n.k

2. Case nyingine ambayo zero inahusika ni kwenye cut and fill.... daaah mkuu naskia raha sana kuielezea zero, daaah wakati wa kuweka level ya barabara huwa kuna sehemu tunapunguza level zingine tunaongeza level, Kuna formula huwa tunazitumia kutambua wapi tupunguze na wapi tuongeze na kiasigani cha material kitahitajika either kuongezwa site ama kuhamishwa sasaa basi ukiadd up ukapata zero maanake hapo hapahitaji kuongeza ama kupunguza chochote, you seee,,,, zero ina umuhimu sanaa man

Daah yaani nina mengi ya kukwambia kuhusu zero ila Leo naomba niishie hapa
 
Back
Top Bottom