Je, umegeuzwa chaka la uovu?

Motowntzjpm

Senior Member
Jun 16, 2023
118
191
Leo hii nimetizama KBC ambapo Festus Mwakerubi aliibua swala la uzalendo – uzalendo ni nini - na swali lake liljibiwa na Dkt. Zebedayo Kiungu, Mkuu wa Chuo cha Veta – Tabora.

Kwa miaka nyingi sasa tafsiri ya Uzalendo kwa Watanzania umeeelekezwa kuwa na maana ya tuwachukie wao ili tuonekane kupenda cha kwetu. Kwamba usipomzungumzia vibaya mgeni au ukimzungumzia kwa mazuri asiyekuwa mtanzania umekosa uzalendo.

Jibu lake Dkt. Kiungu limenikosha mno na naomba nitoe mifano:

01. Alinijibu ndugu yetu mmoja kwamba hakukuwa na sababu ya kutoa taarifa kwa bosi wake (ambaye alikuwa Mgeni) huku yeye na ndugu zetu wengine wakiwa wanakwamisha jambo lenyewe. Huyo ataondoka sisi tutabaki hapa hapa.

02. Miaka kadhaa iliyopita swala la uKurugenzi wa Vodacom ulichafua hali ya hewa huku wanasiasa wakidai kampuni inashindwa vipi kupata Mtanzania mmoja wa kupewa wadhifa huo. Marehemu Ali Mfuruki alimuomba kwa maandishi Jenista Mhagama ampe majin 5 ya Watanzania wenye sifa. Jenista hakujibu barua. Lakini Vodacom waliliaumiwa kwa kukosa uzalendo na nia yao ya kumteua mkenya Sylvia Mulinge ukakwamishwa kwa Zaidi ya miezi 6. Hatimaye dada Sylvia aliteuliwa Mkurugenzi wa MTN Uganda ambapo anaendelea kunufaisha mtandao huo namba moja Nchini Uganda.

03. Hivi Karibuni mkataba wa ukarabati wa Kivuko ulileta zogo kwa kuwa aliyeshinda zabuni aliku kampuni ya Marine Services ya Mombasa Kenya kwa bilioni 4. Kulikuwa na kelele nyingi kwamba kazi ingepewa kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine ambao waliomba kwa B7 na sababu zilikuwa hizo hela zingetumika humu humu. Neno uzalendo ulitumika.

04. Vijana wa Kitanzania 200 wapo Israel kwa mafunzo ya kilima cha kisasa (pole nyingi kwa familia ya mmoja aliyeuwawa na Hamas) na Marekani. Taasisi iliomba fedha kutoka kwa mabenki (tunayoyaita ya Kizalendo) ambayo yote hayakuona umuhimu wa maudhui. Waliotoa hela walikuwa Benki ya Equity ya Kenya. Benki ambayo kwa muktadha hiyo siyo ya kizalendo. Swali langu kama wao waliona umuhimu iweje tusione uzalendo wao? Au uzalendo kwa muktadha huo wa mabennki ya Kizalendo una maana gani.

05. Waziri mdogo kabisa(anapenda kujipambanua hivyo) akiongea Clouds aliulizwa kuhusu maji mkoa wa Singida (kijiji sikumbuki) . Kwenye jibu lake (ilikuwa kujisifia kwa kufikisha maji 83% ya vijiji vyetu Tanzania) Aweso alisema yule mkandarasi wa kigeni tutamtoa, bila kusema kosa lake-au kuashiria kosa lake ni kutokuwa Mtanzania.

Mifano yote inaashiria alichosema Dkt. Kiungu kwamba sasa hivi tuumelipa uzalendo maana kwamba ukichukia mgeni yeyote basi wewe ni mzalendo namba moja.

Unaweza ukauliza tatizo liko wapi?

Tatizo upigaji anayozungumza CAG haufanywi na wageni. Utepetevu shuleni na vyuoni au kwenye hospitali zetu unafanywa na sisi.

Swali ni je Uzalendo umegeuzwa Chaka cha Uovu?
 
NDIYO.
mabadiliko ya maana ya maneno kulingana na nyakati au manufaa ya kikundi fulani tu.
I'll kwa Sasa hili neno Lina maana mbaya Zaid kuwahi kutokea.

Mzalendo kwa Sasa ni mlinzi wa uovu na mfumo kandamizi.
 
Back
Top Bottom