Je nafsi hutabiri matukio yajao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je nafsi hutabiri matukio yajao?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Kacharimbe, Dec 30, 2011.

 1. K

  Kacharimbe JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wakuu heri ya mwaka mpya. Kwa muda sasa suala hili limekuwa likinisumbua. Imenitokea mara kadhaa kuwa naweza kuwaza kitu fulani au mtu fulani sura yake ikaja na baadaye kitu hicho hutokea au kama ni mtu unaona anakuja au unakutana naye. Leo nilikuwa naweza jinsi ya kutoka ofisini ili niende kwenye sherehe. Wazo likaniijia kuwa nisingizie kuwa kwa jirani kuna msiba. Wazo hilo nikalifuta haraka sana. Haijapita hata saa moja nikapigiwa simu kuwa jirani yangu amefariki. Hi ni nini au ni coincidence?
   
 2. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli mkubwa nafsi kupitia maumbile zina madaraja mbalimbali,wako watu wanapata ndoto za kweli kama taarifa ya tukio linalotarajiwa,wengine bila hata kuota bali wazo lolote litalomjia bila shinikizo huwa ni taarifa ya kweli,wako pia ambao akikuapiza au kukulaani kwa chochote hutokea kweli,hivi ni sehemu ndogo ya vipawa ambavyo baadhi ya binadamu wamepewa.ndipo wengine wakishajigundua kuwa na mambo kama haya hujifanya waganga kuibia watu.haya ni mambo ambayo manabii walipewa rasmi kabisa kuwa nayo na ndio chimbuko la miujiza,lakini hata watu wa kawaida hubahatika kuwa na baadhi ya mambo.
   
Loading...