Je, Mwanzi ni mti au nyasi?

Je, Mwanzi ni mti au nyasi?

Mwanzi ni nyasi, miwa ni nyasi, mahindi ni nyasi, mpunga ni nyasi na ngano, mtama, ulezi, matete na uwele.
 
Mwanzi ni jina la spishi nyingi za nyasi ndefu zinazoweza kuonekana kama miti. Mianzi yote huwa na shina ya aina ya ubao.

Mianzi hupatikana kiasili katika Afrika, Amerika na Asia lakini inastawi pia ikipandwa Ulaya.

Urefu wa spishi kubwa hufikia kina
cha mita 40.

Inaweza kukua zaidi
ya mita 1 kila siku lakini kwa kawaida ni sentimita 3-5 kwa siku.

Shina la mianzi huwa na umbo la bomba na unene wake ni hadi sentimita 30. Shina hugawiwa na vifundo.

Kila kifundo kina chipukizi na machipukizi yanaweza kuendelea kuota matawi.

Matumizi:

Mianzi ina matumizi mengi kwa binadamu.

Inafaa kwa ujenzi wa nyumba, madaraja au maboti.

Mashina hutumika pia kwa mabomba ya maji katika nyumba
na kilimo.

Wakati ni changa na laini yaani kabla ya kuwa ubao mwanzi unafaa kama chakula baada ya kupikwa.

Mtovu unakusanywa pia kama kinywaji hasa pombe.

Katika utamaduni wa China ya Kale vipande vya mianzi vilitumiwa
kama bao za kuandika matini.

Nyuzi zake hutumika pia kutengenezea magodoro
 
Back
Top Bottom