Je, Mwanamke wa hivi anaweza badilika katika ndoa?

Dandamerci

Member
Apr 14, 2021
14
26
Jambo ndugu zangu,

Nahitaji msaada wenu.

Mimi ni kijana nina miaka 22 niko kwenye mausiano na dada fulani ambaye tuna tarajia kuoana. Sasa kuna vitu ambavyo vina ni tatizaga na jiulizaga sipatagi majibu.

Na vitu hivyo ni kuhusiana na tabia ya huyo binti. Mara nyingi huyu mtoto wa kike huwa hanisikilizi. Kila nikimwambia sitaki kitu fulani nikione kwako utakuta tunabebana, kama atakubali yaani ni kwa mbinde kabisa na tena baada ya siku fulani kupita utakuta tena ulicho mkataza ndicho anachokifanya.

Na mara nyingine utakuta anaongea na mimi kwa sauti kubwa; hata ukimwambia mwanaume hafokewi yeye huwa hajali hata kidogo. Na ukizidisha kumwambia kuhusiana na kuongeya kwako uta kuta ana ni jibu ndo maana sipendagi kuongea na wewe.

Yeye ndo rafiki wa wanaume utakuta mwanaume akimwambia njoo twende huku anakubali, anapokuwa yeye ndipo wanaume walipo kuwa na matani nao ya kugusana gusana. Hata nikimwambia aache tabia hiyo utakuta najibiwa "jiamini"

Yeye ndo mtu wa kupost picha na video za kijinga kwenye status za Messenger na WhatsApp utakuta amepost picha mara anapiga kiss mara anatoa ulimi nje mara anaimba, mara anabinuwa matako yake.

Nikimshauri naambiwa mimi ndo nina wivu.

Mwanaume akimsimamisha hata kama yuko na mimi utakuta anasimama na akiombwa namba anatoa bila tatizo.
  • Ni muongo sana
  • Anapenda mauzo sana
  • Ana dharau watu wengine mpaka na mimi
  • Ana kiburi
  • Hujiona mrembo na mara nyingi husema hawezi kosa soko yeye ni mrembo
Sasa huyo mtoto wa kike nimeshafunga naye ndoa. Kulingana na mila zetu sisi hufunga kwanza ndoa halafu mke utaenda kuchukua siku ya kwenda kuweka mali.

Sasa hapo ndipo nina maswali. Je, mwanamke wa hivi kweli anaweza badirika katika ndoa au pesa zangu niziwekeze kwenye mambo mengine?
 
Huyo manzi ako atakuwa either bado ni teenager au ndio katoka kwenye u teenage.

Na wewe kwa umri wako huo naona bado sana kuingia kwemye ndoa. (Japo sikupangii)

Na hizo mapigo zenu za kuahidiana kuoana ni utoto tu unawasumbua mkikua mtaacha. Wewe kama unapata huduma endelea kula mzigo acha kumfuatilia sana utajitesa bure kwa maumivu yakiwaki.

Pia mkuu Kiswahili chako nimekipenda sana nikizuri japo ni adimu.

Ila lazima mtakuja kuachana tu hamna ndoa hapo.
 
Kaza rohoo kaka ushauziwa mbuzi kwenye gunia
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
uyo amuwezani Mzee mtafikishana pabaya embu mpe muda kabla ya kupelekq pesa uskute uko alipo walimwengu wanamsasambua
emoji23.png
 
Mwache mtoto mwenzao akue, hata hajamaliza usichana wake vizuri unamuwazia ndoa. Ndo kipindi chache cha kujishebedua.

Na wewe katafute hela ili baadae uweze kutunza familia, kwa umri huo umejaa ubabe mwingi sijui ukikua utakuwaje.
 
Hili linahitaji ushauri?
Anaombwa namba mbele yako anatoa?
Anaweka picha kabinua makalio Kwa status?

Unakuja kuomba ushauri kweli?

Hadi umkute telegram na badoo anatangaza bei ndo uje uelewe?
Mnamlaumu bure mtoto under 20 hebu mwacheni.
 
Mwandiko mgumu kinoma!! Hata hivyo nimekuelewa!

Ushauri!! Umri wako bado ni mdogo sana kuyabeba hayo maudhi, shukuru Mungu umeyajua mapema! Hana sifa za mke hata kidogo, nakushauri jikatae mdogo mdogo!

Ukioa huyo, baada ya mwaka utarudi hapa kulalamika kuwa kuishi na mke ni pasua kichwa! Tafuta mke anayekusikiliza na kukutii.
 
Back
Top Bottom