Je? Musa, Eliya na Henoko wako wapi?

Je? Musa, Eliya na Henoko wako wapi?

"""""Hakuna aliyepata kwenda mbinguni,,, isipokuwa mwana wa mtu ambaye ameshuka kutoka mbinguni""""
YOHANA 3:13 BHN.


Hii ni kauli ya YESU, wakati akiwa duniani. Ila kwenye kitabu cha mwanzo kinasema
HENOKO alitwaliwa,

Eliya naye akaenda na upepo wa kisulisuli halikadhalika na MUSA.

Wakuu hii imekaaje?

Baba mtakatifu91, Matunzo 02, and others
Wapo paradiso ,
 
REJEA marko 9:1-25
Wengine hawatakufa ila wataingia mbingun bila kuonja mauti musa, eliya walikuwa ni watumishi wake MUNGU waliofanya makubwa sana kwa Mungu hivyo Mungu akawapa zawadi ya kutoonja mauti
Hivi jamani Mussa si alionyeshwa nchi ya ahadi na kisha akafia milima ya Sinai au mimi nd'onimechemka katika kumbu kumbu zangu?
 
"""""Hakuna aliyepata kwenda mbinguni,,, isipokuwa mwana wa mtu ambaye ameshuka kutoka mbinguni""""
YOHANA 3:13 BHN.


Hii ni kauli ya YESU, wakati akiwa duniani. Ila kwenye kitabu cha mwanzo kinasema
HENOKO alitwaliwa,

Eliya naye akaenda na upepo wa kisulisuli halikadhalika na MUSA.

Wakuu hii imekaaje?

Baba mtakatifu91, Matunzo 02, and others
Kitabu cha Biblia kinazungumzia aina tofauti za mbingu. Kumbuka neno hili linatumika kwa maana 3 tofauti kama vile ifuatavyo,

1. Mbingu ya kwanza ni Anga Hewa. Hii ni mbingu tunayoiona kila siku ambayo ndege huruka ndani yake, rejea Mwanzo 1:20 Ndege warukao juu ya nchi katika anga ya wazi ya mbingu"_
Mawingu, mvua, radi ziko hapa rejea Zaburi 104:12 ndege za mbinguni hukaa karibu nazo. Kwa lugha ya Kiingereza ni "sky"

Mbingu nyingine ni Anga ya Nje. Hapa ni mahali zilipo jua, mwezi, nyota na sayari, rejea Mwanzo 1:14
"na ziwe ishara na nyakati, na siku na miaka"
Zaburi 8:3 Nikitazama mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziweka
Kwa lugha ya Kiingereza "space / universe"

Mbingu ya Tatu ni Makao ya Kiroho ya Mungu. Hapa ni mahali wanapokaa Mungu, malaika, viumbe vingine vitakatifu.

Mathalani, rejea 2 Wakorintho 12:2 Paulo anasema, "Namjua mtu katika Kristo, alinyakuliwa hata mbingu ya tatu."
1 Wafalme 8:30 "Sikia kutoka mbinguni, mahali pa kukaa kwako"
Mathayo 6:9"Baba yetu uliye mbinguni"

Hapa ndipo pia kuna kiti cha enzi cha Mungu rejea Zaburi 103:19

Wayahudi wa kale waliamini uwepo wa hizi mbingu 3. Lakini kupitia kwa Yesu Kristo na Paulo zinafunguliwa uwepo wa mbingu nyingine zaidi ndani ya mbingu ya 3 ambazo ni mahali pengine pa makao ya viumbe wa Mungu.

Na ukweli kuhusu hili ulifumbuliwa katika Agano Jipya kutokana na ujio wa neno jipya "Paradiso" linatokana na lugha ya Kiyunani, yaani "Paradeisos" likiwa na maana ya "Bustani nzuri" au "Hifadhi ya kifalme" ama kwa kifupi Paradiso ni mahali pa makazi ya kiroho bila ya dhambi, wala maumivu au mateso yake

Katika Biblia ina maana ya Paradiso kuwa ni mahali zilipo Roho za Waaminio baada ya kufa.
Yesu alitumia neno hili pale msalabani rejea
Luka 23:43 Amin, nawaambia, leo utakuwa nami katika Paradiso. Hapa ni mahali pa kupumzika kwa muda kwa Watakatifu wakisubiri ufufuo.

Paulo akiwa katika Roho pia alipelekwa katika mbingu ya tatu, rejea 2 Wakorintho 12:3-4 na akasikia maneno ambayo hayawezi kusemwa.

Tunafunuliwa pia ujio wa Mbingu ya Mwisho ni Ufalme wa Mungu wa Milele. Hii ni maana ya mwisho na kamili, rejea Ufunuo 2:7 Mshindi nitampa kula katika mti wa uzima, ulio katikati ya Paradiso ya Mungu rejea Ufunuo 22:1-2 inazungumzia Mto wa Uzima na Mti wa Uzima katikati ya Paradiso mpya.

Hapa ndipo Watakatifu watakapoishi na Mungu milele. Hakuna machozi, hakuna maumivu rejea Ufunuo 21:4

Mbingu Mpya itakuwa ni makao yajayo ya Mungu ambayo itakuja sambamba na Nchi Mpya rejea Ufunuo 21:1

Kupitia katika kanuni lugha ya Kibiblia ya namba, namba tatu humaanisha mpango wa Mungu kwa mwanadamu hudumu kwa muda kisha huenda katika ukamilifu wake wote.

Tuna kila sababu ya kuamini juu ya uwepo wa mbingu saba tofauti kwani kupitia katika kanuni hii ukamilifu wote wa Mungu hukaa kutokana na ahadi zake kwa mitume na manabii.

Ni ahadi ya Mungu kwa wale wote wanaomwamini Yesu rejea Yohana 14:2-3 Katika nyumba ya Baba yangu kuna makao mengi, nitaenda kuwatayarishia makao.

Hivyo basi, katika moja ya mbingu hizi 7, sehemu mojawapo ndipo Henoko, Eliya, na Musa hukaa, wakingojea kumalizia majukumu waliyopangiwa kuyafanya katika ulimwengu huu wa mwili ili nao wapate kuishi katika Nchi Mpya katika miili mipya.
 
Musa na Eliya,na Watakatifu wote,wako peponi siyo Mbinguni! Peponi na Mbinguni ni tofauti.
Peponi ni mahali ambapo Watakatifu wanaenda baada ya kutoka duniani.
Mbinguni ni mahali ambapo Mungu anakaa!
Yesu Kristo alikuwa Mbinguni kwa Baba,akarudi Mbinguni aliko Baba.
 
Mbinguni ni makao ya MUNGU aliumba mwenyewe na dunia akaiweka iwe makao ya wanadamu milele.
Mwanzo 1
Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi......,
Sayari nyingine hazina viumbe?kwa nini Mungu allichagua sayari ya dunia ndio binadamu waishi?
 
Hivi jamani Mussa si alionyeshwa nchi ya ahadi na kisha akafia milima ya Sinai au mimi nd'onimechemka katika kumbu kumbu zangu?
upo sahih musa alikufa na kuzikwa lakin musa hakufa kama watu wengine yeye macho hakufunga wala damu mwilin mwake haikuacha kutembea rejea kumbukumbu la torati 34
 
Back
Top Bottom