Ukiona unamchagulia yapi anafanya na yapi hafanyi kwa kutazama mazuri na mabaya basi tambua huyo Mungu sio muweza wa yote bali wa machache tena yale tu yanayo kufurahisha.
Mkuu, kwa nini umesema hivyo? Je, umefikiri kwa kina na mawanda yote kuhusu hii mantiki yako?
Hakika kamanda ili swali huwa linanifanya nisiende kanisani
Sasa iwapo hutaki kwenda huko yanakopatikania majibu, utaokokaje?
Unashindwaje mtihani hivyo hata kabla ya kuanza kuufanya?
Ninacho maanisha ni kuwa, hapa Duniani tupo kwenye mtihani
Mtihani huo ni matokeo ya Adamu na Hawa kushindwa mtihani wa awali alioagizwa asile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Ukifeli mtihani wa Mungu, anakupa mtihani mwingine wa SUP (ambao kimsingi huwa mgumu na tekniko kidogo kuliko ule wa awali!)
Kimaandiko hiyo inaitwa rehema ya Mungu. Kila mtu amepewa nafasi ya pili.
Ikiwa mwanadamu ataichezea hiyo nafasi, basi kwa jinsi hiyo anakuwa amethibitisha kutofaa kwake kuishi maisha yanayolingana na maisha ya Mungu Mwenyewe--umilele.
Uajabu mwingine wa Mungu ni uwezo Wake wa kutupatia sie wadhambi rehema na haki kwa wakati mmoja.
Haki ya mdhambi ni kufa milele (mshahara wa dhambi), ilhali rehema ya Mungu ni uzima wa milele kwa wale wamwaminio.
Ili kubalansi mlinganyo huo wa kiungu, ndiposa kigezi (factor) cha Yesu Kristu kinaingia hapo kati ya haki ya Mungu na rehema Yake.
Pasipo kifo cha Yesu Kristu Bwana wetu msalabani Kalvari, sie ni wapotevu tusiokuwa na tumaini.
^Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kutuletea Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye Kristu Yesu asipotee bali awe na uzima wa milele.^ ~ Yohana 3:16