Mkuu
Kiranga nazingatia post yako No.526 nitaegemea kwenye mambo mawili kati ya kadhaa ulioyaongelea
1.Kwamba dini ilianza kwa watu kutaka kujipa majibu ya maswali ambayo hawakuwa na majibu yake
Sasa Mbona mpaka leo ambapo kuna technology,,innovation na design za ajabu bado kuna almost watu 5 billion wanasali.Hauoni hapo kuna jambo zaidi ya kukosa majibu ya maswali..Huhisi kusali ni natural characteristics aliozaliwa nayo binadamu na sio tabia alioikuta baada ya kuzaliwa.??? Hudhani kwamba unahitaji mda zaidi ujiulize kuhusu sala na ibada kwa Mungu kwamba na wewe inakuhusu ila umechelewa tu??
Hii technology unayoiona kubwa leo wewe, bado ni ndogo sana. Ndiyo kwanza tumeanza kugundua vitu. Einstein's Relativity imethibitishwa miaka 100 tu, na hata hiyo watu wengi mpaka leo hawajui inazungumzia kitu gani.
Ukienda Kariakoo usimamishe watu kumi, uwaulize mmoja baada ya mwingine, theory ya Relativity ya Einstein inazungumzia nini, wangapi wanaweza kukupa jibu sahihi angalau la jumla tu?
Watu wengi ni watumiaji tu wa hizo technology na innovation, hawaelewi zinavyofanya kazi. Watu hawaelewi Einstein's Relativity inavyo support GPS na Satellite na Internet, wanatumia tu hivi vitu bila kujua hata kwa juu juu vinavyofanya kazi.
Sasa hawa nao unawahesabu kwamba wanaelewa technology kiasi cha kuwafumbua macho wahoji habari za Mungu?
Inawezekana watu wakawa wanazaliwa na hali ya kutaka kusali au kuabudu, lakini hilo halitoshi kufanya Mungu awepo. Watu wanazaliwa na hali ya kujiona wanaona, lakini macho yao yamenyimwa uwezo wa kuona X-Rays, Gamma Rays, Ultraviolet Rays, Radio waves etc. Kutoiona hiyo miale hakufanyi isiwe muhimu au isiwepo.
Pia unaweza kuzaliwa ukaangalia kwa macho ukaona the earth is flat, naturally unaona the earth is flat, lakini kuona hivyo hakufanyi dunia iwe flat kama ni ya mviringo. Unahitaji uchunguzi zaidi kujua mambo magumu na mazito, si mambo yanayojulikana kwa kukubali vitu kirahisi tu.
Huoni magharibi baada ya kuacha makanisa matupu wameamua kufanya Mambo machafu mno ndoa za jinsia moja,,beastility na upuuzi usiosemekana ambapo dini na sala vilipokuwepo waliogopa kuvifanya?
Sala/dini, zaidi ya kuwa therapy kwa masikini, ina kazi nyingi sana.
1. Inatumiwa na matajiri na watawala kuwafanya masikini watumwa.
2. Inatumiwa na wabaguzi wa rangi kujitenga wao kundi hili ili wawabague wengine (ndiyo maana makanisa mengi Marekani unakosema watu wanasali sana yamegawanyika kwa ubaguzi wa rangi, ni social clubs za kubaguana kwa rangi)
3. Ni sehemu za watu kujionesha na kujitangaza, nani katoa sadaka kubwa, nani ana gari kubwa nani ana familia nzuri.
4. Ni sehemu ya hata wasioamini Mungu kwenda na kusema "Hata kama Mungu hayupo, dhana ya kuwepo kwake ni muhimu sana katika kuweka usalama, watu wengi, hususan masikini, wakijua Mungu hayupo, watafanya fujo sana.
5. Ni sehemu ya kwenda kutoa sadaka ili ujisikie umelipia mabaya yote uliyofanya. Ni therapy hata ya matajiri. Wezi na wauza madawa ya kulevya kibao wanaenda makanisani kutoa sadaka kubwa tu Mungu awabariki katika kazi zao. Angalia historia ya Mafia Mob na kanisa uone wakubwa wa Mafia walivyo Wakristo wazuri.
Mbona hayo mambo watu wanafanya mpaka kanisani huko Roma kila siku wana scandals?
Mbona kuna watu hawaamini uwepo wa Mungu na kwa kutoamini huko wanaishi Maisha yenye higher moral grounds?
Mimi nisipoamini kuwepo Mungu, naona mtu hawezi kunijaza ujinga nikaingia katika "holy war" na kumuua mtu kwa jina la Mungu. Hapo tayari kutoamini uwepo wa Mungu kumenisaidia kutoingia katika ujinga wa kulipua watu wenzangu kwa kisingizio cha mungu.
Huko Afrika watu wanapoamini Mungu sana mbona nako kuna ushenzi mwingi sana tu?
2.Sala ni therapy ya watu maskini wasio na therapist
Hivi Mbona kuna matajiri wengi sana wanasali,,,angalia Marekani ambayo bado kanisa lina nguvu uone ni matajiri wangapi wanasali,,,nenda kwa wayahudi wa ultra orthodox,,nenda Moscow utaona matajiri wakisali,,,majirani zangu waislam pitia Riadh,,tehrani mpaka Azerbaijani utaona matajiri wakisali,,njoo Africa ndio usiseme.Labda ungeniambia hao wasio na dini wanatafuta therapy artificial kwa kuwa hawajataka kujua natural ilio katika dini.