Je, Mungu aliumba dunia kwa miaka Elfu 6?

Je, Mungu aliumba dunia kwa miaka Elfu 6?

Kwa mujibu wa Biblia takatifu Mungu aliumba Dunia kwa siku sita na kumpumzika siku ya saba kulingana na kitabu cha Mwanzo.

Lakini kuna dhana ya kwamba siku moja mbinguni ni sawa na miaka elfu moja duniani pia nikinyume na kwamba miaka elfu duniani ni sawa na siku moja mbinguni.

Pia kulingana na dhana hiyo tunaweza pata kitu hiki, kwamba Mungu alipumzika siku ya saba hii inaweza toa taafsiri kuwa Mungu alipumzika miaka elfu moja baada ya kuumba dunia.

Swali muhimu la kujiuliza ni kwamba siku ambazo dunia iliumbwa na Mungu zinahesabiwa katika hali ipi ya kuhesabu siku kidunia au kimbinguni?

Wajuzi wa mambo naomba ufafanuzi katika hilo.

El perdode
Kitendo cha muda kuwepo mbinguni, ndio tatizo linaanzia hapo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo "siku" sita ni nyakati sita.

Nyakati ni "cycles", umri wa dunia ni mabilions ya miaka, sasa ukigawanya hayo mabilions ya miaka utapa kila nyakati una umri wa bilions kadhaa za miaka.

Katika kila nyakati umbo la dunia lilikuwa likibadilika hadi nyakati ya mwisho (ya 6) dunia ilipochukua sura kamq hii t unayoiona leo, sura ambayo ina mito, maziwa, bahari, Ozone layer, atmosphere, viumbe hai nk,.

Mungu kupumzika katika siku ya 7, maana yake (yawezekana) ni kwamba katika nyakati ya 7 duniani hakukutokea au hakutatokea mabadiliko yoyote yaani Mungu hakufanya commandment yoyote kubadilisha umbo la dunia, Mungu kupumzika haina maana kwamba Mungu alichoshwa na shughuli za uumbaji na akaamua kupumzika, lazima tukumbuke kuwa Mungu ni mkamilifu katika kila hali, hasinzii, halali, hali, hanywi, hachoki nk, tukisema kwamba Mungu alipumzika jinsi tunavyopumzika sisi viumbe vyake basi ipo siku (apishe mbali) wstu watasema Mungu atakufa kama jinsi viumbe wake tunavyokufa. Mungu apishe mbali na atuepushe na fikra mbovu za kumdhalilisha.
logic yako imekaa vzuri ila ni uwongo
 
Unaelezwa ukweli, ni kwamba umekosea bro.

Weka huo ukweli hapa tuuone, sio kusema eti nimekosea huku hamuelezi kosa lenyewe na ukweli wenyewe!!😱, nyie Watz vipi???!!
 
Weka huo ukweli hapa tuuone, sio kusema eti nimekosea huku hamuelezi kosa lenyewe na ukweli wenyewe!![emoji33], nyie Watz vipi???!!
Soma hapo juu post namba 297 na post namba 301 nimejibu tayari. By the way nyakati moja ni mwaka mmoja wa kibinadamu, ndo maana nimekuambia umekosea bro.
 
Soma hapo juu post namba 297 na post namba 301 nimejibu tayari. By the way nyakati moja ni mwaka mmoja wa kibinadamu, ndo maana nimekuambia umekosea bro.

Wapi inasemwa kwamba nyakati ni mwaka mmoja wa kibinadamu (365days) ??
 
Mimi Nina majibu sahihi ya swali lako ila ni mvivu WA kuandika alafu muda pia
 
Kitu kiwe Logic halafu kiwe ni Uongo ??!!---- unajua maana ya logic au umejiropokea tu ili uonekane umeongea pumba!!??
Mkuu embu elezea logic tafadhali niongeze maarifa juu ya logic.
ahsante.
 
Mbingu nazo ziliumbwa according to Bible.
Mungu hakai mbinguni , kama anakaa mbinguni je, kabla ya kuziumba alikuwa anaishi wapi?
Je, tukubali kuwa alihamisha makazi alipokuwa anaishi na kuhamia mbinguni?
Nakupa challenge tu hapa ili ufahamu wako uondoe dhana ya kusema Mungu anaishi mbinguni.
Mbingun na kama mji wa Mungu , kwa mfano upo Tanzania lakini numbani ni mwanza
 
Mkuu embu elezea logic tafadhali niongeze maarifa juu ya logic.
ahsante.

Hebu soma hapa ili uelewe maana ya Logic;

Screenshot_20210911-210720.png
 
Kwani mimi nimesema 365 days au nimesema mwaka mmoja? Au hujui Calender tunayotumia sasa siyo iliyokuwepo zamani?

Anyway ukitaka kujua nyakati zimefafanuliwa wapi, soma kitabu cha Daniel mpaka ukute kile kisa cha mfalme Nebukadreza alipotolewa kwenye ufalme hadi nyakati saba zilivyopita juu yake ili ajifunze kuwa Mungu ndiye anayetawala na kumiliki, kisha baada ya hapo alirudishwa tena kwenye ufalme wake, ukishaelewa hapo sidhani tena kama utatafsiri Biblia vibaya ukisema Mungu aliumba dunia kwa nyakati sita badala ya siku sita.
 
Hapana Mungu aliumba dunia kwa siku sita na siyo miaka elfu sita. Kwani anasema hivi "ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku moja"
"ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili" n.k n.k mpaka siku zote sita na siku ya saba kupumzika, ni siku hizi hizi sita tunazozijua.

Dhana ya miaka elfu moja ni kwamba kwa uwezo alionao Mungu, mambo ambayo wanadamu wote duniani tutakayo yafanya kwa miaka elfu moja, technolojia, maendeleo n.k n.k, Mungu yeye anauwezo wa kuyafanya kwa siku moja.

Kingine kwa Mungu hakuna siku wala miaka, minguni hakuna usiku wala mchana, utahesabu vipi siku, kwahiyo siku zinazozungumziwa ni hizi hizi za kwetu huku duniani.
Ni kweli, mbinguni tutakakoishi milele hakuna muda

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Kwani mimi nimesema 365 days au nimesema mwaka mmoja? Au hujui Calender tunayotumia sasa siyo iliyokuwepo zamani?

Anyway ukitaka kujua nyakati zimefafanuliwa wapi, soma kitabu cha Daniel mpaka ukute kile kisa cha mfalme Nebukadreza alipotolewa kwenye ufalme hadi nyakati saba zilivyopita juu yake ili ajifunze kuwa Mungu ndiye anayetawala na kumiliki, kisha baada ya hapo alirudishwa tena kwenye ufalme wake, ukishaelewa hapo sidhani tena kama utatafsiri Biblia vibaya ukisema Mungu aliumba dunia kwa nyakati sita badala ya siku sita.

Wewe unadhani ni Biblia pekee ndiyo imesema kwamba Mungu aliumba dunia kwa siku 6 ??!!,

Soma hii aya ya Qur'an tukufu:

Katika Lugha ya kiarabu katika hiyo aya maneno siku sita yameandikwa "sitata ayyami", neno ayyami ni wingi wa neno "yaum"(siku moja) nalo pia lina maana ya wakati , kipindi, muda nk, (period, duration etc).---- hivyo kulingana na Science ya maumbile na umri wa dunia, hizo "SIKU 6", ni nyakati 6 zinazopimwa in terms of Billions or millions of years kipindi ambapo dunia/ ulimwengu ulikuwa unaumbika au unabadilika kimaumbile hivyo kubadilika kimaumbile kwa dunia katika hizo nyakati 6 (siku 6) ndiko kuumbwa kwake ili binadamu aweze kuja kuishi.

Soma hii aya ya Qur'an.
Screenshot_20210912-075928.png
 
Point of correction:
Mungu hakuumba mbingu na nchi kwa siku sita. Ukisoma Kitabu ca Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliiziumba Mbingu na nchi…” hapo MWANZO( ni kabla ya Uumbaji kuanza Duniani). Siku sita zilikuwa za Uumbaji kwenye sayari ya Dunia. Inaonekana Uumbaji wa Mbingu na sayari zote ulianza maelfu kama siyo mamilioni ya miaka hapo kabla. Ndiyo maana huwa siwapingi wana sayansi wanaposema Dunia ina mamillioni ya miaka.
Correct me if I’m wrong
 
Kwa mujibu wa Biblia takatifu Mungu aliumba Dunia kwa siku sita na kumpumzika siku ya saba kulingana na kitabu cha Mwanzo.

Lakini kuna dhana ya kwamba siku moja mbinguni ni sawa na miaka elfu moja duniani pia nikinyume na kwamba miaka elfu duniani ni sawa na siku moja mbinguni.

Pia kulingana na dhana hiyo tunaweza pata kitu hiki, kwamba Mungu alipumzika siku ya saba hii inaweza toa taafsiri kuwa Mungu alipumzika miaka elfu moja baada ya kuumba dunia.

Swali muhimu la kujiuliza ni kwamba siku ambazo dunia iliumbwa na Mungu zinahesabiwa katika hali ipi ya kuhesabu siku kidunia au kimbinguni?

Wajuzi wa mambo naomba ufafanuzi katika hilo.

El perdode
Kwenye siku hizo ulizozitaja hapa; Mungu alikuwa tayari ameshaumba dunia kabla; kwa hiyo dunia haikuumbwa ndani ya siku hizo ila ilikuwepo tayari Alichofanya Mungu kwenye siku hizo ni kufanya modification kwa kile ambacho tayari alikuwa ameshaumba huko nyuma, haijulikani ni lini ila ilikuwa ni kabla ya siku hizo sita unazoziongelea wewe hapa. Tulia, soma vizuri Biblia
 
Leta maandiko mkuu kila mtu asome na kuchangia mada hii ndo maana ya JF

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom