Je, Mtoto wa kambo ana haki ya kurithi mali?

Habari wapendwa?

Tuna watoto 4, ila mtoto mkubwa wa kwanza sio wangu nilioa mke wangu akiwa tayari ana mtoto, watoto watatu ndio nilizaa naye. Huyu mtoto wa kufikia tangu akiwa mdogo miaka 2 nimemuhudumia kila kitu hata shule hajawahi kusoma hizi shule za kata, sasa hivi yupo kidato cha 3.

Wakati namuoa nilimpa masharti sitaki mawasiliano na baba mtoto wako, hata yeye anadai hawezi kuwasiliana naye maana aliikataa mimba. Miaka minne iliyopita niligundua anawasiliana na mzazi mwenzie ikafikia hatua kipindi nipo safari alikuwa akimpeleka mtoto kwa mzazi mwenzie nikaona haina shida maana ni damu yake, ila nikamuuliza baada ya miaka 11 leo hii mtoto amekua mkubwa ndio ameona umuhimu wake?

Alikataa mimba leo unamuona wa maana? Ndani ya miaka 2 naona amebadilika sana amefikia hatua anaanza kumwambia mtoto baba yake ndiye anayemuhudumia kila kitu, huyu mtoto ameanza kupunguza upendo kwangu ni tofauti na zamani.

Kiuchumi MUNGU amenisaidia nipo vizuri nilichofanya mali zangu zote pamoja na pesa nimewaandikishia watoto wangu wa damu, huyu wa kufikia nimeachana nae sijampa chochote licha ya kumlea kwa miaka 12. Je, kuna kosa kisheria? Maana mama yake anataka kwenda mahakamani ili na yeye mtoto wake apate sehemu ya mali.

NB: Katika mali zangu huyu mwanamke hana mchango wowote wakati namuoa kila kitu alikikuta
Huyo mtoto hana chake mkuu,,,mwache aende POPOTE,,,,mtoto huyo sio DAMU yako,,,na hakuna mahakama itakayompa ushindi huyo mama,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najibu hapo mwisho kwenye mchango wa mwanamke. Mke wako ana haki na mali zako hata kama amezikuta.. mchango wake sio lazima uwe pesa..Kama anatekeleza majukumu ya kulea familia na kukutunza huo ni mchango tosha. Haki anayo kama hajakiuka mambo mengine ya mahusiano yenu.

Kuhusu mtoto wa kambo subiri wanasheria wabobezi waje. Ila mtoto kufahamu baba yake mzazi ni Jambo la kheri sema bidada kakiuka makubaliano yenu.

Binafsi niliolewa nikiwa nina mtoto. Mume akanipa masharti kama hayo nikaona poa tu maana baba mtoto hakuwa responsible kwa mwanae. Na jina akataka nimbadilishe atumie la kwake nikakubali lakini kishingo upande.

Miaka inasonga sioni akitekeleza majukumu kwa mtoto ipasavyo..hata ukaribu wa baba na mtoto hakuna, anatoa matunzo kwa kujivuta vuta as if sio mwanae vile. Uzuri ni kwamba mie sio mlalamishi naridhika na chochote kidogo ila ikawa inaniuma sioni kama mtoto anatunzwa ipasavyo na uwezo anao mkubwa tu. Napambana mwenyewe kila siku ninastress za matunzo.

Nikaona isiwe taabu.. nikamrudishia jina lake la awali..nikamtafuta baba yake na shangazi zake nikawakutanisha na mtoto wao.

Maana niliona nampeleka mtoto kwenye ukoo ambao ipo wazi kabisa hawamchukulii uzito, why nimpe jina lao?Now nina amani moyoni!

Kama jamaa angelibeba jukumu ipasavyo nisingefanya hivyo. Na mbaya zaidi mtoto alianza kumuulizia baba yake mzazi..loh nikasema isije niletea matatizo makubwa baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo haki za kuinjoy mali alizozikuta umempa wewe au reference ni ipi kisheria?
 
Kitakachouua wewe ni mkeo, mume aliyezaa naye na huyo mtoto wa kambo.

Mtoto msomeshe hujui kesho yake.

Mali hauondoki nazo, wagawie watoto wote sawa,

Mkeo naye ana haki hata kama alivikuta, si anakupikia, kukufulia, kuzaa, kukuandalia hata maji uoge, naye mgawie.

Ila, ikitokea umetangulia kufa hao wanao wako taabuni.

Hakuna mtoto mbaya kuliko mtoto wa kambo japo siyo wote.

Mtoto wa kambo wa mume wangu nilieenda kwa mguu wangu kumkomboa kwa bibi yake kule tpc na lile jua tena nikiwa mja mzito,

alichonifanyia ni aibu kusema na mwisho hapo alipofariki mr alinitafutia wahuni nusura waniuwe mie na watoto wangu siku tumetoka makaburini,

tena vita hiyo yote ni kajumba tulikojenga ujanani na mr na kagari kamoja,

Anyway, chukua comments zetu changanya na zako,

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo dogo mwehu! Wanakuwaga bitter sababu mama zao hawajaolewaga!
 
Nyie ndio mnakera. Utake atumie jina lako halafu nikate mawasiliano na baba yake halafu usihudumie ipasavyo?

Nifanye hivyo kwaajili gani sasa? Alilazimishwa kunioa nikiwa na mtoto au ni kiherehere chake tu. Ndio maana tunawatafutaga baba zao...kikubwa ni makubaliano mliyoingia mwanzoni. Mambo ni mengi..si kila kitu nimeandika hapo.

Mi wala sina tatizo sana, silazimishi mtu ahudumie..akishindwa natafuta another alternative, asilalamike tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hii hati ni kuwa jamaa mwenye watoto mapenzi nae huna kabisaaaa 😅😅😅😅😜
 
Habari wapendwa?

Tuna watoto 4, ila mtoto mkubwa wa kwanza sio wangu nilioa mke wangu akiwa tayari ana mtoto, watoto watatu ndio nilizaa naye. Huyu mtoto wa kufikia tangu akiwa mdogo miaka 2 nimemuhudumia kila kitu hata shule hajawahi kusoma hizi shule za kata, sasa hivi yupo kidato cha 3.

Wakati namuoa nilimpa masharti sitaki mawasiliano na baba mtoto wako, hata yeye anadai hawezi kuwasiliana naye maana aliikataa mimba. Miaka minne iliyopita niligundua anawasiliana na mzazi mwenzie ikafikia hatua kipindi nipo safari alikuwa akimpeleka mtoto kwa mzazi mwenzie nikaona haina shida maana ni damu yake, ila nikamuuliza baada ya miaka 11 leo hii mtoto amekua mkubwa ndio ameona umuhimu wake?

Alikataa mimba leo unamuona wa maana? Ndani ya miaka 2 naona amebadilika sana amefikia hatua anaanza kumwambia mtoto baba yake ndiye anayemuhudumia kila kitu, huyu mtoto ameanza kupunguza upendo kwangu ni tofauti na zamani.

Kiuchumi MUNGU amenisaidia nipo vizuri nilichofanya mali zangu zote pamoja na pesa nimewaandikishia watoto wangu wa damu, huyu wa kufikia nimeachana nae sijampa chochote licha ya kumlea kwa miaka 12. Je, kuna kosa kisheria? Maana mama yake anataka kwenda mahakamani ili na yeye mtoto wake apate sehemu ya mali.

NB: Katika mali zangu huyu mwanamke hana mchango wowote wakati namuoa kila kitu alikikuta
Na wewe waambie watoto wako huyu si ndugu yenu sawa bro.
 
Hiyo haki mke anayo kisheria au hayo ni maoni yako kutokana na uelewa wako?

Na wanaume vipi tuna haki na Mali ambazo wake zetu wamerithishwa na wazazi wao?
Sisi kwa Tamaduni zetu mtoto wakike hana urithi kwa wazazi wake, Watoto wakiume ndiyo wana rithi kwa wazazi wao, Mtoto wakike ana rithi mali za mume wake na siyo mali za wazazi wake.
 
Hapana., baba mwenyewe hana mbele wala nyuma so hanishtui.
Kwa hiyo ukiona mzazi mwenzio hana mbele wala nyuma wwe ndiyo furahaa yako, ila angekua na mbele pamoja na nyuma ndiyo rohoo yako ingestuka!? Wanawake Mungu anawaona mnavyotamani na kufurahia ma ex wenu wakiwaa wanataabika na maisha!!
 
Sio furaha yangu. Lkn ukweli ndo huo hashtui kwa lolote. Atafute pesa alee mrtoto wale maana hampi hata senti hata akipata, ni mchoyo thats why habarikiwi.
 
Back
Top Bottom