Je, Mtoto wa kambo ana haki ya kurithi mali?

Naamini, 'mtoto' anarithi mali za 'mzazi' wake.

'Mzazi'haijalishi ni baba au mama kwa sababu, ikiwa mama yake ataachana na baba yake, basi katika mgawanyo wa mali mama atapata sehemu gake ambayo na "mtoto wa kambo" anaweza kurithi kwa mama yake.

Imekuwa ni desturi kwamba baba ndiye mwenye kurithisha mali za familia na sio mama, na hata kama baba akitangulia mbele za haki basi mali inagawanywa na familia inasambaa (bila kujali kuwa mama yupo), ikiwa ni tofauti na pale inapotokea mama akatangulia mbele za haki kabla ya baba huwa hakuna mgawanyo n.k

Naamini, japo sheria haimtambui mtoto wa kambo moja kwa moja, lakini ana haki ya kupata sehemu ya mali za mzazi wake pekee, kama ni baba au mama, lakini wale watoto waliozaliwa na pande zote mbili wao watarithi katika jumuisho la 'familia'.

Kumbuka, mama ana mchango wake katika mali za familia, kwa mtazamo wangu hata kama utarithisha watoto wa ndoa...najiuliza tu wakati unakutana na huyu mama akiwa na mwanae hakuwa na mali yoyote kiasi cha kutodhani mwanaye anastahili kitu pia?

Nadhani suala lenu linahitaji kuchimbwa vizuri, nami naona kabisa kuna sehemu ya mali atapata mtoto wa kambo kupitia mama yake (hata kama sheria haijataja moja kwa moja).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najibu hapo mwisho kwenye mchango wa mwanamke. Mke wako ana haki na mali zako hata kama amezikuta.. mchango wake sio lazima uwe pesa..Kama anatekeleza majukumu ya kulea familia na kukutunza huo ni mchango tosha. Haki anayo kama hajakiuka mambo mengine ya mahusiano yenu...
SIYO KWELI SHERIA INASEMA WANANDOA WATAGAWANA MALI ZAO AMBAZO WALIZICHUMA WOTE NDANI YA NDOA. KWA MAANA KILA ALICHOKUWA NACHO MWANANDOA KABLA YA NDOA NI MALI YAKE BINAFSI.
 
SIYO KWELI SHERIA INASEMA WANANDOA WATAGAWANA MALI ZAO AMBAZO WALIZICHUMA WOTE NDANI YA NDOA. KWA MAANA KILA ALICHOKUWA NACHO MWANANDOA KABLA YA NDOA NI MALI YAKE BINAFSI.
SIO KWELI MALI ZOTE ATABAKI NAZO YULE ALIYEBAKI HAI MPAKA MUNGU AMCHUKUE ndipo watoto /warithi na km kuna mtoto wa nje ya Ndoa Mama atamuangalia pia km aliandikiwa ni nini apate.

Mfano Baba kafariki ana umri wa miaka 89 hamuwezi kusema mali zake kabla hajaoa sizihesabiwe kama ni za mke pia, wameshazaa na wana wajukuu.

Huo mfano ulioutumia ni kwa vijana wa miaka 30 wameoana wakiwa na miaka 21 kwa 18
 
Aisee, pole sana mkuu. Muombe Mungu atakupitisha katika hilo jaribu. Katika swala hilo km lipo jinsi ulivyolielezea, basi hapo mwanamke amezingua sana. Kwann arud kwa mtu ambaye hamthamini na alimtelekeza?. Ameshindwa kutambua wapi pa kuelekea, ametawaliwa na mapenz ya nyuma.

Huyo mtt wa nje hana makosa, mpe tu ata kiasi kidogo cha kumsaidia km una uwezo uliojitosheleza wa kimali, msamehe tu man ni sumu ya mama yake ndiyo inayomuangamiza. Na kuhusu mama mtu ata kama alikukuta na hizo mali. Huyo ni mkeo tu na ana haki ya kupata na yeye, maana mmefunga ndoa na mmezaa wtt, mmesaidiana kwa miaka yote hiyo. Napo ana haki tu.

Na ukishindwa zaidi, basi jaribu kushirikisha wazee wa familia ili uweze kupata ufumbuzi wenye maana. Kila la kheri mkuu.

The Most Winner
 
Wanawake wa miaka hii wana mambo ya kisenge sana.

Kimsingi mimi hapo mkataba ungeisha.... Namwambia asepe.... Nitalea watoto wangu wa damu tu huyo mtoto wake na yeye waende kwa huyo mwanaume anaewasiliana nae...... Usenge tu kuendekeza.

Ukicheka na mwanamke katika mambo ya kipuuzi kama hayo ipo siku utashangaa unaletewa mimba nyingine na si yako. Tena hata hao watoto wengine kapime vinasaba kabisa.

Hivi kwann vijana huwa mnakuwa na mambo ya kiboya kuchukua mademu used.....?!

Kuna wanawake wanahangaika huko makanisani anatafuta mwanaume wa kufanya nae maisha.....

Wengine bado wapo vyuoni wengine sekondari na wengine wanazaliwa why nyie mnapata shida sasa kutafuta hadi mnachukua mizigo used?!

Ona sasa shukurani ya punda......... Fukuza huyo tena asitoke hata na kijiko hana akili.... Msyuuuuuuuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu suala la mtoto was kambo kurithi mali za baba mlezi hayo ni maamuzi yako....ukipenda unampa kidogo ila usipopenda bado pia hujafanya kosa. (,Huu no uelewa wangu, naweza kosolewa).

Ningependa kuwashauri vijana wenzangu, inapotokea mmemumimbisha mdada wa watu in vizuri mkachukua maamuzi ya kulea na sio kukimbia majukumu yenu.

Naamini matatizo mengi yanatokana na kuvunja maagizo ya dini na tamaduni zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
True

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wapendwa?

Tuna watoto 4, ila mtoto mkubwa wa kwanza sio wangu nilioa mke wangu akiwa tayari ana mtoto, watoto watatu ndio nilizaa naye. Huyu mtoto wa kufikia tangu akiwa mdogo miaka 2 nimemuhudumia kila kitu hata shule hajawahi kusoma hizi shule za kata, sasa hivi yupo kidato cha 3.

Wakati namuoa nilimpa masharti sitaki mawasiliano na baba mtoto wako, hata yeye anadai hawezi kuwasiliana naye maana aliikataa mimba. Miaka minne iliyopita niligundua anawasiliana na mzazi mwenzie ikafikia hatua kipindi nipo safari alikuwa akimpeleka mtoto kwa mzazi mwenzie nikaona haina shida maana ni damu yake, ila nikamuuliza baada ya miaka 11 leo hii mtoto amekua mkubwa ndio ameona umuhimu wake?

Alikataa mimba leo unamuona wa maana? Ndani ya miaka 2 naona amebadilika sana amefikia hatua anaanza kumwambia mtoto baba yake ndiye anayemuhudumia kila kitu, huyu mtoto ameanza kupunguza upendo kwangu ni tofauti na zamani.

Kiuchumi MUNGU amenisaidia nipo vizuri nilichofanya mali zangu zote pamoja na pesa nimewaandikishia watoto wangu wa damu, huyu wa kufikia nimeachana nae sijampa chochote licha ya kumlea kwa miaka 12. Je, kuna kosa kisheria? Maana mama yake anataka kwenda mahakamani ili na yeye mtoto wake apate sehemu ya mali.

NB: Katika mali zangu huyu mwanamke hana mchango wowote wakati namuoa kila kitu alikikuta
Ktk dini yetu Huyu mtoto wa kambo si sehemu ya warith wako kisheria,ila mke kama utatangulia kufa wewe yeye atarithi 1/8 ya Mali yako yote.

na Mke akifa mali akagawie ndugu zake au mwingine aliyemuoa?
sheria Mke hagawiwi mali bali atabaki nazo hadi kifo chake, na hapo Watoto ndio wataendelea na mgao wao ulioandikwa awali na Baba yao
(Hii ilitokana na wengine wangeolewa kwa wanaume wa mbali au kabila tofauti au Dini, na hapo huyo mwanamume mgeni angehamisha tena mali km mke angetangulia/ kufa) Faida kwa kuoa wajane na kuwazalisha upya
 
Mimi nina mtazamo tofauti,sitisha zoezi la kugawa mali zako.Endelea kupambana na kuisaka mali kwa kadri ya uwezo wako.
Subiri watoto wakue wakubwa.
Huyo mtoto wa kambo ni ndugu wa damu na watoto wako,hata ukifa leo,Yeye ndio atawatunza wadogo zake.Usisite kumpatia Elimu bora kisa ana baba yake mzazi.
Kama utaweza mpe ahadi kem kem za hata kumsomesha nje ya nchi,ili kumfunika hata baba yake mzazi.
Ukionyesha unataka kumtenga,unaamsha vita vya chinichini na mke wako,na kumpa nafasi baba mzazi wa mwanao kuingiza pembe,watakuua!Hizo ni cahngamoto za kuoa Single Mother
 
Naamini, 'mtoto' anarithi mali za 'mzazi' wake.

'Mzazi'haijalishi ni baba au mama kwa sababu, ikiwa mama yake ataachana na baba yake, basi katika mgawanyo wa mali mama atapata sehemu gake ambayo na "mtoto wa kambo" anaweza kurithi kwa mama yake.

Imekuwa ni desturi kwamba baba ndiye mwenye kurithisha mali za familia na sio mama, na hata kama baba akitangulia mbele za haki basi mali inagawanywa na familia inasambaa (bila kujali kuwa mama yupo), ikiwa ni tofauti na pale inapotokea mama akatangulia mbele za haki kabla ya baba huwa hakuna mgawanyo n.k

Naamini, japo sheria haimtambui mtoto wa kambo moja kwa moja, lakini ana haki ya kupata sehemu ya mali za mzazi wake pekee, kama ni baba au mama, lakini wale watoto waliozaliwa na pande zote mbili wao watarithi katika jumuisho la 'familia'.

Kumbuka, mama ana mchango wake katika mali za familia, kwa mtazamo wangu hata kama utarithisha watoto wa ndoa...najiuliza tu wakati unakutana na huyu mama akiwa na mwanae hakuwa na mali yoyote kiasi cha kutodhani mwanaye anastahili kitu pia?

Nadhani suala lenu linahitaji kuchimbwa vizuri, nami naona kabisa kuna sehemu ya mali atapata mtoto wa kambo kupitia mama yake (hata kama sheria haijataja moja kwa moja).

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeeleza vizuri, lakini kwa Tanzania watoto wote Ni sawa na masuala ya watoto yanaamuliwa na sheria ya mtoto ya 2009 ambayo ilifuta sheria za awali kuhusu mtoto kwa mfano Affiliation Act iliyokuwa inatambua illegitimate child.Hivyo watoto wote ni sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada wanasheria Mimi nimeoa mke na nikakopa benk hela ya kujengea nimeweka mshahara wangu dhamana je tukiachana tunagawana pasu kwa maana 50-50 waakati huo mkopo haujaisha
 
Tumia busara tu Ndugu yangu
Habari wapendwa?

Tuna watoto 4, ila mtoto mkubwa wa kwanza sio wangu nilioa mke wangu akiwa tayari ana mtoto, watoto watatu ndio nilizaa naye. Huyu mtoto wa kufikia tangu akiwa mdogo miaka 2 nimemuhudumia kila kitu hata shule hajawahi kusoma hizi shule za kata, sasa hivi yupo kidato cha 3.

Wakati namuoa nilimpa masharti sitaki mawasiliano na baba mtoto wako, hata yeye anadai hawezi kuwasiliana naye maana aliikataa mimba. Miaka minne iliyopita niligundua anawasiliana na mzazi mwenzie ikafikia hatua kipindi nipo safari alikuwa akimpeleka mtoto kwa mzazi mwenzie nikaona haina shida maana ni damu yake, ila nikamuuliza baada ya miaka 11 leo hii mtoto amekua mkubwa ndio ameona umuhimu wake?

Alikataa mimba leo unamuona wa maana? Ndani ya miaka 2 naona amebadilika sana amefikia hatua anaanza kumwambia mtoto baba yake ndiye anayemuhudumia kila kitu, huyu mtoto ameanza kupunguza upendo kwangu ni tofauti na zamani.

Kiuchumi MUNGU amenisaidia nipo vizuri nilichofanya mali zangu zote pamoja na pesa nimewaandikishia watoto wangu wa damu, huyu wa kufikia nimeachana nae sijampa chochote licha ya kumlea kwa miaka 12. Je, kuna kosa kisheria? Maana mama yake anataka kwenda mahakamani ili na yeye mtoto wake apate sehemu ya mali.

NB: Katika mali zangu huyu mwanamke hana mchango wowote wakati namuoa kila kitu alikikuta
Hao ulio waandikisha Mali umepima DNA?
 
Back
Top Bottom