Je, mtoto anaweza kulelewa kwa mafanikio ikiwa sheria za malezi za wazazi/walezi wake zitakuwa tofautitofauti?

Oct 5, 2018
33
58
Je, mtoto anaweza kulelewa kwa mafanikio ikiwa sheria za malezi za wazazi/walezi wake zitakuwa tofautitofauti? Yaani Baba ana kanuni na taratibu hii, Mama ana kanuni na taratibu hii. Yapi maoni yako?
 

Attachments

  • UMOJA WA WALEZI.png
    UMOJA WA WALEZI.png
    123.6 KB · Views: 1
Mkuu hii kitu ngumu sana.

Mtoto hawezi kukua vizuri kimaadili.

Anajengeka kiburi kwa kufuata kule anakoona rahisi hata kama ni kubaya.

Atachukia upande wenye ugumu kufuata hata kama ndiko kunakomfaa.

Ni ngumu kuacha vitabia fulani kwa kuwa anajua kuna utetez upande fulani na rahisi kujenga vitabia vingine vichafu.

Ni ngumu mtoto kulelewa vizuri katika hayo mazingira.(Kutokana na experience)
 
Mkuu Justine Kakoko kwa maoni yangu binafsi nadhani ni ngumu sana kulea watoto wazazi wakiwa na kanuni na maoni tofauti tofauti,

linapokuja swala la malezi nadhani ni muhimu kwa wazazi kuungana na kuwa kitu kimoja ili kumshape mtoto na kuwa yule wanayemtaka awe,

kwa nini ni ngumu? kwa sababu mtoto ni malezi yote ya baba na mama,sasa inapotokea kutofautiana maanake ni kwamba mtoto atashikama na upande ambao unamfavour na kudharau kabisa upande ambao uko against naye hata kama upande ulio against ni upande unaomtakia mema na ndio wenye malezi bora Zaidi,

imagine baba hapendi kitu Fulani na mtoto kakifanya,baba akamuonya au kumtia nidhamu mtoto then mama haoni sababu kwa nini baba kafanya hivyo,kisha mama anaanza kumfariji mwanae labda na kumhoji baba kwa nini kafanya vile tena mbele za mtoto mhusika,katika hali kama hii ni lazima mtoto kwanza hatajua kipi ni bora au ni sawa as baba kaonya mama kafariji na kumquestion baba,kisha mtoto ataangalia ananufaikaje na jambo alilolifanya au analipenda kiasi gani,kisha akiona jambo alilolifanya linamnufaisha au analipenda sana,basi hapo kupitia mwitikio wa mama ambaye kamfariji mtoto na kumquestion baba mtoto atachagua kuendela kufanya jambo hilo hata kama ni baya akijua sikuzote mtetezi wake atakuwepo na kwa kuwa ni jambo ambalo analipenda basi atalikumbatia sikuzote.

Mkuu inaniwia vigumu sana kulieleza hili kinagaubaga lakini mwisho wa siku linapohusu swala la malezi wazazi wanapaswa kuungana na kuwa na lao moja,watengeneze kanuni,misingi na sheria ambazo wangependa watoto wao waziishi na wakubaliane wangependa watoto wao waje kuwa watu wa ina gani katika jamii,kisha wasaidiane kufanikisha hilo,hata ikitokea utofauti baina yao uwe ni mdogo tu na ambao hata watoto hawawezi kujua,wazazi wanamalizana wenyewe huko,kwa njia hiyo watoto wanaweza kuwa watu bora sana,tofauti na hapo ni mpasuko na kutengeneza familia isiyoeleweka na isiyo na Umoja.
 
Back
Top Bottom