1-Kwa kawaida mwanaume huweza kufurahia tendo la ndoa bila hata kumpenda mwanamke, lakini kwa mwanamke, hiyo ni tofauti, kwani hawezi kufurahia tendo la ndoa kama hajampenda mwanaume. Kwa mwanaume tendo la ndoa halihusiani kabisa na kupenda.
Katika kipengele hicho hapo ndipo nawaona wanaume kama wadudu, maana anaweza akamsifia mwanamke kiasi ambacho yule mwanamke akadhani kapendwa kumbe mtu anataka free game tu, sasa najiuliza kuwa ni kwa nn husemi kuwa nahitaji free game,au One night stand na wewe halafu kwisha kuliko kumdanganya mwenzio anabaki na matumaini kumbe wewe unae aliyerohoni kwako.
Pia ni kweli mwanamke hawezi kufurahia tendo la ndoa bila kumpenda mwanaume, lakini mwanaume hata kama mmegombana yeye anaona lile tendo ndilo suluhisho la ugomvi wenu ndani ya nyumba, na ukimwambia huwezi kushiriki hilo tendo kwa sababu una hasira yeye anadai ugomvi ni kati yako na yeye, lakini Adam na Hawa hawana ugomvi, wao wanatakiwa wasalimiane kama kawa. Hapo ndipo nashindwa kushangaa kuwa wao wanawezaje kushiriki tendo ihali wanahasira.