Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,725
- 6,730
Kumekuwepo na biashara kubwa ya vifaa vya umeme unaotokana na mwanga wa jua (solar energy system). Biashara hii imeshamiri kila kona ya nchi ikiwa inafanywa na wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Pia biashara hii imevutia makampuni mengine ya kigeni kama Off-Grid ambao makao yao kwa Tanzania yapo Arusha, Solar Sister (kanda ya ziwa), M-Kopa Solar Ltd (Dar es Salaam) ambao wao wanawafungia wateja wao vifaa vya solar bure kisha wateja hao kulipa malipo ya kila mwezi kwa kampuni.
Sasa nikiangalia uwekezaji unaofanywa na serikali kwa sasa hivi kwenye kuzalisha umeme na kuusambaza kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na mradi uliopo wa umeme wa REA utakaosambaza umeme hadi vijijini, najiuliza kama bado hii biashara ya solar ina muda mrefu wa kuendelea kuwepo na kutengeneza faida kwa wafanyabiashara/wawekezaji kama hao Off-Grid, Solar Sister, M-Kopa Solar? Hebu wadau tuchangie ili kuelimishana.