Je, Meli ya Mv Victoria ni mbovu?

Je, Meli ya Mv Victoria ni mbovu?

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,708
Reaction score
8,746
Hii meli ilipark pale bandari ya Mwanza kusini (Mwanza South Port) kwa miaka mingi.

Hivi karibu kwenye utawala wa Magufuli meli hii imekarabatiwa kwa kupakwa rangi na kutengenezwa baadhi ya sehemu, inasemekana hadi Injini ilibadilishwa.

Hivi majuzi kuna jamaa yangu wa karibu alisafiri na hii meli kwenda Bukoba, kwa kweli kwa maelekezo yake hii meli ni Kimeo, ilizimika Mara kadhaa njiani wakati Mvua inanyesha na baadhi ya maeneo kupitisha maji.

Siku kadhaa nyuma meli ilizima tena ikabidi watu wafaulishwe kwenye maboti.

Meli imekaribia bandari ya kemondo ikazima tena.

Sasa muhimu kuchukua tahadhali mapema ili kuepusha majanga.

Serikali isipende sifa kwamba imetengeneza meli kumbe meli yenyewe mtego tu wa kuua watu.


Source: abiria wa kwenda Bk
images%20(6).jpg
 
NDIO TATIZO LA KUFANYA KAZI BILA TARATIBU ZA WAZI ZA UZABUNI.....KAZI ZINATOLEWA KWA AMRI YA MTU MMOJA ....MIRADI MINGI YA AINA HIYO IMETUMIKA KUIBA KIASI KIKUBWA SANA CHA PESA ..NA HAIRUHUSIWI KUONGEA ...WATU WANAKAAA KIMIYA ...HUKO MBELE KUNA WATU WENGI SANA WATAJAAA KISUTU.....HAPO ZAIDI YA RANGI HAKUNA KITU ...NI MV DAR ES SALAAM NYINGINE ..
 
Kuna post humu ndani nilimwambia mmwaga sifa mmoja wa serikali hii kuwa miradi mingi ni substandard, mfano barabara, majengo nk, alikuja sana, nikamwambia mingi haitafukisha miaka mitano itaanza kuharibika, kwani serikali ya sasa inachojali ni wingi na sio ubora. Kama kuna hilo la meli huo ni muendelezo wa mtazamo wangu.
 
Hii meli ilipark pale bandari ya Mwanza kusini(Mwanza South Port) kwa miaka mingi

Hivi karibu kwenye utawala wa Magufuli meli hii imekarabatiwa kwa kupakwa rangi na kutengenezwa baadhi ya sehemu ,inasemekana hadi Injini ilibadilishwa....
Siyo kazi ndogo wanayoifanya kina Zitto na Lissu!!

Mwishowe mmeshika somo sasa!

Yaani mnaamua kuwa waongo mchana kweupe kuwashinda hata walimu wenu siyo?

Yaani mzigo unaobebwa na Meli ufaulishwe kwenye boti??

Pumbavu
 
Kuna post humu ndani nilimwambia mmwaga sifa mmoja wa serikali hii kuwa miradi mingi ni substandard, mfano barabara, majengo nk, alikuja sana, nikamwambia mingi haitafukisha miaka mitano itaanza kuharibika, kwani serikali ya sasa inachojali ni wingi na sio ubora. Kama kuna hilo la meli huo ni muendelezo wa mtazamo wangu.
Mkuu, hii haiwezi kuwa kweli hata kidogo, usiuamini huu upumbavu!

Mzigo unaobebwa na Meli ufaulishiwe kwenye boti kweli?
 
Mkuu, hii haiwezi kuwa kweli hata kidogo, usiuamini huu upumbavu!

Mzigo unaobebwa na Meli ufaulishiwe kwenye boti kweli?

Hili sina uhakika nalo, ila kuwa miundombinu mingi ni substandard ili kusaka political millage, hilo halina mjadala. Inawezekana mzigo haukifaulishwa bali watu ili kuokoa maisha yao. Lakini kwakuwa vyombo vya habari haviko huru, huwezi kusikia hili kwenye vyombo rasmi vya habari zaidi ya huku mitandaoni. Hivyo wangalau tunaona 50% kuna ukweli, na 50% tunasubiri udhibitisho.
 
Mimi sio mwana CCM kabisa but huwa napenda mtu anapoleta post kama hii angalau kuwe na ushahidi..
Coz habari bila ushahidi zinafanya tunaochangia tuonekane hatuna akili pls wekeni habari na ushahidi ili JF iendelee kuwa bora..
Mkuu mara nyingine flow ya taarifa inaweza isiwe rasmi au kusionekane ushahidi dhahiri lakini haimaanishi kuwa taarifa nzima si sahihi.
Hii meli kwa sasa imekarabatiwa lakini kabla ya hapo ilikuwa na hali mbaya sana hivyo, rumours kama hizi si za kuzipuuza unless upewe ushahidi full kuwa ipo sawa
 
Back
Top Bottom