Je, Makonda kavunja mwiko?

Je, Makonda kavunja mwiko?

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,776
Afrika kwa ujumla na hususan Tanzania (baada ya Uhuru) Polisi wamekuwa ni watu wa kuogopewa na jamii kama vile nyoka.

Nnakumbuka miaka ya mwanzoni mwa nchi yetu kupata Uhuru Polisi walikuwa ni watu wanaopendwa na jamii, enzi hizo ilikuwa utawakuta polisi wa Kizungu, Kihindi, Kiarabu na Kiafrika.

Kama watoto, kila mmoja wetu alikuwa anatamani siku moja awe askari Polisi. Kilichotupelekea kuwa hivyo ni jinsi enzi hizo polisi walivyokuwa na upole kwa watoto, nnakumbuka wakija mashuleni kutupa mafunzo ya kila aina na kutueleza vipi tuwe raia wema wenye kusaidia wengine. Nnakumbuka pia polisi wakituvusha barabara kwa upole na ingawa magari yalikuwa si mengi.

Nnachokikumbuka zaidi kwa polisi wa siku hizo ni tabasamu zao, awe wa kiume au wa kike (wa kike walikuwa wachache sana), ilikuwa siku zote nikiwaona polisi amma njiani amma wakija mashuleni walikuwa na tabasamu lisilokwisha na wenye nyuso za furaha kiasi cha kukufanya uliye karibu nao uwe na amani.

Hayo yaliisha mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha.

Baada ya hapo mpaka hii leo, Polisi wamekuwa ni watu wasiocheka na watu, polisi imekuwa ndiyo tishio kwa watoto, mtoto wako akikosa ukimtajia polisi basi anaingiwa na uoga.

Jee, tumejiuliza kwanini? Mimi nna-majibu mengi sana kuhusu hilo lakini nnawaachia wachangia mada nanyi mjinafasi na kutoa dukuduku lenu kwa mtazamo wenu.

Paul Makonda, ameweza kuwasema polisi hadharani, tena kinaga ubaga. Mwiko ambao hata wakubwa zaidi ya Makonda kwenye uongozi wameshindwa kuuvunja kwa hapa kwetu Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika kwa ujumla. Jee, kwanini?

Binafsi nnaona kitendo cha Makonda ni cha kishujaa sana. Wewe jee?

Nnaomba tuchangie hii mada huku tukielekeza maoni yetu kwa viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa majeshi ya polisi kwa nia ya kuitaka polisi iwe rafiki zaidi wa wananchi na iwe ni kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili ya viongozi wa nchi au watawala wa nchi pekee.
 
Vita ya wanasiasa (wanafiki flani vile) dhidi ya watumwa wao polisi (wanafiki wakujipendekeza)........Ni ngumu kuitabiri

lazima mmoja anatolewa kafara

Namsubiri mzee mtukufu kamanda Siro anene kututoa tongotongo.
 
"Ushujaa" nadhani hata Makonda alidhani hivyo..,,anzia kwa Kabwe.....ngoja nikueleze Makonda angekuwa shujaa Kama angesema hayo katika hali gani...
1. Mpinzani wa serikali.
2. Angekuwa Na cheo cha chini kabisa nje ya kamati ya ulinzi Na Usalama.
3. Angekuwa yeye Mwenyewe Ni polisi...
Neno "Shujaa" lingefi"t Sana hapo

Kwa ujumla, Makonda sio "Shujaa" na huwezi kuwa "shujaa" kwa kusema Tu, Na kitafuta umaarufu hewa.....
Ngoja nikwambie baadhi ya mashujaa WA siasa za Bongo baada ya uchaguzi mkuu hadi Leo Nov. 2016.
1.Bashe
2.Lema
3.Lissu
4.NA wengine wengi...
 
Ni kitendo cha kishujaa sana. Jwtz nao wako kikaangoni, askari wake wengi wanajifanya wababe kwa raia na barabarani, ukiwahoji wanaweza kukuchangia kukupiga, wanajenga ukuta na raia! Nidhamu ya uoga dhidi yao ma wananchi ndo kilichopo katikati!
 
Afrika kwa ujumla na hususan Tanzania (baada ya Uhuru) Polisi wamekuwa ni watu wa kuogopewa na jamii kama vile nyoka.

Nnakumbuka miaka ya mwanzoni mwa nchi yetu kupata Uhuru Polisi walikuwa ni watu wanaopendwa na jamii, enzi hizo ilikuwa utawakuta polisi wa Kizungu, Kihindi, Kiarabu na Kiafrika.

Kama watoto, kila mmoja wetu alikuwa anatamani siku moja awe askari Polisi. Kilichotupelekea kuwa hivyo ni jinsi enzi hizo polisi walivyokuwa na upole kwa watoto, nnakumbuka wakija mashuleni kutupa mafunzo ya kila aina na kutueleza vipi tuwe raia wema wenye kusaidia wengine. Nnakumbuka pia olisi wakituvusha barabara kwa upole na ingawa magari yalikuwa si mengi.

Nnachokikumbuka zaidi kwa polisi wa siku hizo ni tabasamu zao, awe wa kiume au wa kike (wa kike walikuwa wachache sana), ilikuwa siku zote nikiwaona polisi amma njiani amma wakija mashuleni walikuwa na tabasamu lisilokwisha na wenye nyuso za furaha kiasi cha kukufanya ulie karibu nao uwe na amani.

Hayo yaliisha mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha.

Baada ya hapo mpaka hii leo, Polisi wamekuwa ni watu wasiocheka na watu, polisi imekuwa ndiyo tishio kwa watoto, mtoto wako akikosa ukimtajia polisi basi anaingiwa na uoga.

Jee, tumejiuliza kwanini? Mimi nnamajibu mengi sana kuhusu hilo lakini nnawachia wachangia mada nanyi mjinafasi na kutoa dukuduku lenu kwa mtazamo wenu.

Paul Makonda, ameweza kuwasema polisi hadharani, tena kinaga ubaga. Mwiko ambao hata wakubwa zaidi ya Makonda kwenye uongozi wameshindwa kuuvunja kwa hapa kwetu Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika kwa ujumla. Jee, kwanini?

Binafsi nnaona kitendo cha Makonda ni cha kishujaa sana. Wewe jee?

Nnaomba tuchangie hii mada huku tukielekeza maoni yetu kwa viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa majeshi ya polisi kwa nia ya kuitaka polisi iwe rafiki zaidi wa wananchi na iwe ni kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili ya viongozi wa nchi au watawala wa nchi pekee.
JF imejaa vijana wengi wa mwendo kasi hata hilo Azimio la Arusha wanalisikia tu.

Ungewasaidia tu kujua nini kimetokea kuliko kuwapa mtihani wa Harvard Univ.
 
Ajira ya Paul Makonda kwa sasa inamlinda... Polisi wanamuangalia tu...
Jeshi la polisi linadumu...
Ajira ya Makonda itakapoisha ndio tutajua kama Makonda kavunja mwiko au polisi wanasubiri muda ufike...

Ajira yake iishe afu aseme hadharani namna ileile kuwa Sirro kapewa Rushwa... hapo ndio tutalijua jeshi la polisi lina uvumilivu.
 
"Ushujaa" nadhani hata Makonda alidhani hivyo..,,anzia kwa Kabwe.....ngoja nikueleze Makonda angekuwa shujaa Kama angesema hayo katika hali gani...
1. Mpinzani wa serikali.
2. Angekuwa Na cheo cha chini kabisa nje ya kamati ya ulinzi Na Usalama.
3. Angekuwa yeye Mwenyewe Ni polisi...
Neno "Shujaa" lingefi"t Sana hapo

Kwa ujumla, Makonda sio "Shujaa" na huwezi kuwa "shujaa" kwa kusema Tu, Na kitafuta umaarufu hewa.....
Ngoja nikwambie baadhi ya mashujaa WA siasa za Bongo baada ya uchaguzi mkuu hadi Leo Nov. 2016.
1.Bashe
2.Lema
3.Lissu
4.NA wengine wengi...
Lema ana ushujaa gani? Wa "kuota" wakati hajalala??
 
Yeye makonda ndio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa,mmoja kati ya wajumbe ni RPC,akiwasema maana yake yeye ndio kashindwa kazi ya kuwasimamia kama alivyosema waziri mkuu pale mkutanoni.

Kama unashindwa kuwasimamia,serikali inatafuta wa kuwasimamia vizuri,kwa maana ya replacement ya makonda.
 
"Ushujaa" nadhani hata Makonda alidhani hivyo..,,anzia kwa Kabwe.....ngoja nikueleze Makonda angekuwa shujaa Kama angesema hayo katika hali gani...
1. Mpinzani wa serikali.
2. Angekuwa Na cheo cha chini kabisa nje ya kamati ya ulinzi Na Usalama.
3. Angekuwa yeye Mwenyewe Ni polisi...
Neno "Shujaa" lingefi"t Sana hapo

Kwa ujumla, Makonda sio "Shujaa" na huwezi kuwa "shujaa" kwa kusema Tu, Na kitafuta umaarufu hewa.....
Ngoja nikwambie baadhi ya mashujaa WA siasa za Bongo baada ya uchaguzi mkuu hadi Leo Nov. 2016.
1.Bashe
2.Lema
3.Lissu
4.NA wengine wengi...
Nakubaliana nawe mkuu mia ya mia. hongera kwa andiko zuri
 
CCM ndio chanzo cha yote hayo,wacha wafu wazikane.Kila siku wapinzani wanapiga kelele juu ya reform ya jeshi la polisi mnawaona wapuuzi.Leo Makonda kazungumza kidogo mnakimbilia Jf kumuita shujaa,shame.Hv mmerogwaa au?Hao polisi wameanza pigiwa kelele toka lini?Si ndio mkawapa kiburi cha "kupiga tu"?toeni upuuzi,mnatukumbusha machungu
 
Nakubaliana na wewe kuwa makonda ameonyesha ushujaa sana na hasa alipomuuliza waziri mkuu, mpaka waziri mkuu akafadhaika kuwa wanadai wewe ndiye unayewapa vibali vya kuuza shisha
 
CCM ndio chanzo cha yote hayo,wacha wafu wazikane.Kila siku wapinzani wanapiga kelele juu ya reform ya jeshi la polisi mnawaona wapuuzi.Leo Makonda kazungumza kidogo mnakimbilia Jf kumuita shujaa,shame.Hv mmerogwaa au?Hao polisi wameanza pigiwa kelele toka lini?Si ndio mkawapa kiburi cha "kupiga tu"?toeni upuuzi,mnatukumbusha machungu
Ufinyu wa akili ni pale unapolalamika kuwa kitu hakiko sawa ila haupendekezi kirelebishwe vipi.
Ebu tupia hiyo reform ya polisi ifanyikaje?
 
Heshima yako mkuu.

Kwa sasa ni vigumu sana kwa polisi kuwa rafiki kwa raia kwasababu;
1: Serikali haiwajali kwenye maslahi ya yao(mishahara, nyumba za kuishi, usalama wao na mazingira mazuri ya kazi.). Hiyo imepelekea pokisi kujiingiza kwenye rushwa ili kujikimu ki mahitaji. So uzalendo na urafiki kwa raia haupo tena.

2: Ugumu wa maisha unaopelekea kuongezeka kwa uharifu mfano majambazi,wizi na vikundi viovu mfano panya road. Hupelekea polisi kuto kuwa na imani na upendo kwa raia. Miaka ya nyuma matukio ya kuuawa kwa polisi yalikuwa machache lakini sasahivi hali ni tofauti. Hii inawafanya polisi kuondoa ukaribu na raia kwa sababu raia wenyewe kwa asilimia kubwa ni wahalifu.
MAONI YANGU:
serikali ijali na kutatua kero na matatizo ya polisi kwa kuwapa haki zao za msingi.
Pili, serikali itengeneze ajira kwa wananchi ili kupunguza wimbi la uhalifu unaohatalisha usalama wa nchi.
 
Hakuna ushujaa wowote, na hata kama anautaka kupitia polisi hataupata kwani boc wake hataki jeshi lichangamane na raia. hata polisi jamii ilifutwa, waganyakazi wasio polisi walitimuliwa, polisi inayotakiwa ya kuogopwa. rushwa ya barabarani ni kwa kuburush viatu. Hivo Hivo Makonda anaendeshwa na kutafuta kick eneo gumu.
 
Makonda angekuwa "shujaa" zaidi kama angewataja na kuwapeleka wale waliotaka kumpa mamilioni ya shilling badala ya kutoa fumbo. huo ushujaa ambao wanatufundisha sisi tuwapeleke watoa na wala rushwa serikalini mbona yeye kama kiongozi hajafanya kama serikali yetu inavohimiza. Hapo katufundisha nini??
Hii serikali ya Tano imedhamiria kupigana na rushwa. Yeye Makonda hajui anapunguza kasi ya Raisi wetu ya kupambana na rushwa.!!!
Ushujaa gani wewe wa kumkosoa kiongozi mwenzio ndani ya kadamnasi badala ya kumpigia simu au kukaa nae na kumwuuliza kulikoni? Je nae akija kujisafisha ktk kadamnasi si atakuacha na aibu?
 
Heshima yako mkuu.

Kwa sasa ni vigumu sana kwa polisi kuwa rafiki kwa raia kwasababu;
1: Serikali haiwajali kwenye maslahi ya yao(mishahara, nyumba za kuishi, usalama wao na mazingira mazuri ya kazi.). Hiyo imepelekea pokisi kujiingiza kwenye rushwa ili kujikimu ki mahitaji. So uzalendo na urafiki kwa raia haupo tena.

2: Ugumu wa maisha unaopelekea kuongezeka kwa uharifu mfano majambazi,wizi na vikundi viovu mfano panya road. Hupelekea polisi kuto kuwa na imani na upendo kwa raia. Miaka ya nyuma matukio ya kuuawa kwa polisi yalikuwa machache lakini sasahivi hali ni tofauti. Hii inawafanya polisi kuondoa ukaribu na raia kwa sababu raia wenyewe kwa asilimia kubwa ni wahalifu.
MAONI YANGU:
serikali ijali na kutatua kero na matatizo ya polisi kwa kuwapa haki zao za msingi.
Pili, serikali itengeneze ajira kwa wananchi ili kupunguza wimbi la uhalifu unaohatalisha usalama wa nchi.
Tatizo JPM akijaribu kupanga mbowe and co., wanapangua!
 
Ajira ya Paul Makonda kwa sasa inamlinda... Polisi wanamuangalia tu...
Jeshi la polisi linadumu...
Ajira ya Makonda itakapoisha ndio tutajua kama Makonda kavunja mwiko au polisi wanasubiri muda ufike...

Ajira yake iishe afu aseme hadharani namna ileile kuwa Sirro kapewa Rushwa... hapo ndio tutalijua jeshi la polisi lina uvumilivu.
Sawa kabisa, sasa hivi wanamuangalia kama chui mwenye njaa anapomuangalia ngedere au baboon aliyepo kwenye mti mrefu huku akiomba kwa Mungu ateleze na kuanguka chini
 
Back
Top Bottom