Je, Makamba ameishiwa visingizio?

Je, Makamba ameishiwa visingizio?

Umesikia wanasema Mtera, kidatu au kihansi maji ya kuzalisha umeme hakuna?... hata haya ya matumizi ya nyumbani serikali imekuwa inashauriwa ijenge mabwawa-reservoir (kama ilivyo kwa uzalishaji wa umeme) hata mawilii mto Ruvu isiache maji yaingie baharini lakini imekuwa inapuuzia tu tangu enzi za Mkapa.

Pesa ambazo CCM waliidhinisha zitumike kuharibu vyama vya upinzani wangezielekeza hata kujenga mabwawa ya kutunzia maji mto ruvu (hata bwana moja tu) shida isingekuwa ya kutisha kama ilivyo sasa. Wakati mwingine priority zetu za ajabu ajabu zisizoangalia maisha ya kila siku ya watu ndizo hutuingiza kwenye taabu
Sasa wewe unaandika hivyo una uhakika kuwa pesa ilitumika kuvuruga pinzani nchini hapa..
 
Shituka Rais Samia. Takriban 50% ya wakosoaji au wanaochukia Serikali yako wanasababishwa na January Makamba.

Kama ni fadhila kwa wakongwe JK na Yusuf Makamba, tayari umelipa kwa kumpa kazi nyeti. Ila Januari haiwezi kabisa kazi ya kusimamia sekta nyeti ya Nishati. Kama Samia utadika mwaka 2025 na Makamba Januari akiwa Waziri basi utakuwa na kibarua kigumu na CCM yako kushawishi wapiga kura.

Ni hayo tu
Una HAKIKA Gani unayemshauri Si mmoja wao?
 
KAMBA akimaliza 2022 akiwa Waziri,

PEMBE zake zitakuwa ndefu Kutoka mwanzo Hadi mwisho wa Nchi na hapatakuwa na mtu yeyote wa kumzuia even wanaomfuga bandani.
 
Shituka Rais Samia. Takriban 50% ya wakosoaji au wanaochukia Serikali yako wanasababishwa na January Makamba.

Kama ni fadhila kwa wakongwe JK na Yusuf Makamba, tayari umelipa kwa kumpa kazi nyeti. Ila Januari haiwezi kabisa kazi ya kusimamia sekta nyeti ya Nishati. Kama Samia utadika mwaka 2025 na Makamba Januari akiwa Waziri basi utakuwa na kibarua kigumu na CCM yako kushawishi wapiga kura.

Ni hayo tu
Ongeza na nape .yaani mama asipokuwa makini hasara ya february kuwepo huko kwenye carbinet ni kubwa sana .sema kenge asikii mpaka damu imtoke
 
Ndugu Rais Samia Suluhu Hassani.

Zawadi pekee ya kufunga mwaka ni kumuondoa KAMBA na MWIGULU kwenye Uwaziri, na kutuletea Ndugu Kalemani na ndugu KIMEI.

Aamen.
 
Alianza kuondoa wataalamu bobezi, kwenye uongozi Tanesco!
Akaweka Maharage kwenye uongozi Tanesco!
Akaondoa wataalamu wa fani kwenye Bodi Tanesco!
Akawaweka kina Bakhressa Jr, kwenye Bodi mpya ya Tanesco.
Akaongeza kina Gachuma Jr kwenye bodi mpya ya Tanesco.

Akaja na mkataba "tata" na Mahindra kutoka India.

Akaja na taarifa kwamba Magufuli alitoa amri mitambo ifanye kazi bila service na hivyo kuichakaza!

Akasema baada ya ukarabati, mgao au katika katika ya umeme itakuwa historia.

Baadae akawa anakagua vina vya Maji, kwa kutumia helikopta.

Lakini msimamizi wa Bwawa la Mtera, akajitoa kafara.
Akaanika hadharani kwamba hakuna upungufu wa maji kwenye bwawa lile.
Na Makamba hakubisha na ikaachwa hewani kimyakimya.

Akaja na mkataba mwingine na kampuni nyingine kwa alichokisema kuifanyia ukarabati mifumo ya uendeshaji Tanesco.

All at all....Umeme umezidi kuwa tatizo kadri siku zinavyosonga mbele.

Sasa tumeingia mgao wa umeme nchi nzima huku Makamba akiwa kimya kabisaa....

Hatumsikii akiongea chochote kama waziri mwenye dhamana ya Uongozi pale wizarani.

Yuko Bize na kuipigia Promo gesi ya Taifa gas ya Taikuni Rostam.

Je!
Huu ni mwisho wa Uongo wa Makamba?

Alamsikhi!

View attachment 2402373
View attachment 2402380
voicer Njoo huku tuanzie ulipoishia
 
Shituka Rais Samia. Takriban 50% ya wakosoaji au wanaochukia Serikali yako wanasababishwa na January Makamba.

Kama ni fadhila kwa wakongwe JK na Yusuf Makamba, tayari umelipa kwa kumpa kazi nyeti. Ila Januari haiwezi kabisa kazi ya kusimamia sekta nyeti ya Nishati. Kama Samia utafika mwaka 2025 na Makamba Januari akiwa Waziri basi utakuwa na kibarua kigumu na CCM yako kushawishi wapiga kura.

Ni hayo tu
Nashukuru Samia amefuata ushauri huo hapo juu
 
Back
Top Bottom