MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Nianze kwa kusema, kanuzi za kisiasa hazina tofauti sana na kanuni za imani za dini. Kwa maana nyingine ulingo wa dini hauna tofauti sana na ulingo wa kisiasa hasa ikichukuliwa kuwa siasa ni imani kama ilivyo dini.
Hakuna kanisa au viongozi wa dini kama wananchi hawana imani nao. Vile vile hakuna chama cha siasa au mwanasiasa kama wananchi hawana imano nao.
Kwenye ulingo wa siasa kuna aina mbili za kufanya siasa. Aina moja ni siasa za kushambulia na aina nyingine ni siasa za kujihami.
Ni kawaida ya vyama vya upinzani kufanya siasa za kushambulia huku chama tawala kikiwa katika upande wa pili wa siasa za kujihami.
Ukiona vyama vya upinzani vinafanya siasa za kujihami basi hiyo ni dalili inayoonyesha udhaifu mkubwa sana lakini vile vile ukiona chama tawala kinafanya siasa za kushambulia hiyo ni dalili inayoonyesha mafanikio makubwa ya kisiasa katika chama tawala.
Kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka 2015, CCM ilitumia muda mwingi kujihami huku wapinzani wakishambulia. Ajenda kuu ilikuwa ni ufisadi na udhaifu wa serikali. CCM ilijikuta ikidhoofika polepole kutokana na mashambulizi ya wapinzani. Matokeo katika Chaguzi Kuu 2010 NA 2015 yalibainisha udhoofu wa CCM.
Baada ya Uchaguzi Mkuu 2015, siasa zilibadilika ambapo wapinzani walijikuta wakitumia muda mwingi kujihami badala ya kushambulia huku CCM wakiwa ni washambuliaji. Huu ni udhaifu mkubwa kwa vyama vya upinzani ambapo matokeo yake yatabainika katika Chaguzi Kuu zijazo.
Kama ilivyo kwenye siasa, hata kwenye ulingo wa dini kuna pande kuu mbili ambazo ni kushambulia na kujihami.
Kazi wanayoifanya viongozi wa dini ni kumshambulia shetani au ''imani potofu'' wakati huo huo shetani au ''imani potofu''hutumia muda mwingi kujihami.
Ukiona viongozi wa dini au kanisa limeanza kutumia muda mwingi kujihami badala ya kushambulia basi hiyo ni dalili mbaya sana katika uhai wa kanisa au uaminifu kwa Maaskofu.
Waraka wa Maaskofu kwa serikali umeanza kutoa fundisho ambalo nadhani hata Maaskofu hawakutegemea kulipata.
Kwa mara ya kwanza nchini kuona Maaskofu wanatoa waraka kwa serikali halafu wanaanza kutumia muda mwingi kuutetea kwenye makanisa au vyombo vya habari baada ya kugundua waraka unapingwa na waumini wao na pia wananchi wengi wengine. Badala ya Maaskofu kuwa washambuliaji kwa sasa wanatumia muda mwingi kujihami.
Ninakumbuka Maaskofu wakati wa utawala wa awamu ya nne walikuwa wakitoa waraka kwa serikali halafu serikali inaanza kutumia muda mwingi kujihami kwa wananchi. Ukichunguza utagundua kuwa Ufisadi na udhaifu wa serikali ulikuwa unawakera wananchi wengi ndio maana wananchi wengi hawakuwahi kuwapinga Maaskofu baada ya kutoa waraka kwa serikali.
Haikuwahi kutokea Maaskofu wanatoa waraka halafu wao kwa wao wanaanza kugeukana mbele ya waumini wao. Hii imetokea kwa sasa katika kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano.
Uaminifu wa Maaskofu kwa wananchi wengi kwa sasa uko kwenye makutano (crossroad) ambapo kama hawatachukua uamuzi mapema wanaweza kujikuta wanakosa uaminifu kwa wananchi au waumini wao.
Maaskofu walitakiwa wafahamu kuwa tatizo kuu la Tanzania sio Udikteta au uminyaji wa haki za binadamu bali ni ufisadi na udhaifu wa serikali katika kutoa maamuzi na kuyasimamia bila kuyumba. Kama tatizo la Tanzania lingekuwa Udikteta au uminyaji wa haki za binadamu basi Mwl. Nyerere asingefaa hata kuitwa Baba wa Taifa.
Kama nilivyosema, hakuna Askofu kama hakuna waumini na uwepo wa waumini unajengwa na imani kwa Kanisa au viongozi wa dini.
Je, Maaskofu walipuuza hisia za waumini wao kwa serikali?