Je, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa na chuki binafsi dhidi ya Profesa Lipumba? III

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,494
54,906
JE, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD ALIKUWA NA CHUKI BINAFSI DHIDI YA LIPUMBA?

SEHEMU YA TATU: [FACTS FINDING] Katiba ya CUF;-

Na. Maharagande,

Lipumba alipaswa kufanya nini kama alikusudia kutaka kurejea katika nafasi ya Uenyekiti? Swali hili nitalijibu sehemu ya mwisho ya mfululizo wa makala haya. Awali ilikuwa tuishie sehemu ya Tatu. Hata hivyo mahitaji ya wadau/wanachama kujua masuala mbalimbali yameongezeka. Mpaka sasa kuna maswali zaidi ya 70 yaliyoulizwa na kuhitaji ufafanuzi kupitia inbox yangu. Aidha, tunaendelea na kukokoteza vihoja dhaifu vinavyotolewa na vitapata majawabu kupitia makala hizi. Pia Tutauchambua Mkutano Mkuu wa Tarehe 21/8/2016 jinsi ulivyofanyika na Ushauri uliotolewa na Ifriti Jaji Francis Mutungi kama una nguvu za kisheria. Ni mtu mwenye matatizo ya mfumo wa fahamu [Psychiatric Problem] pekee ndiye atakeyeweza kuendelea kuhoji kama Lipumba alijiuzulu au hakujiuzulu.

QUESTION NUMBER 13:

1. Je barua ya Lipumba ilikuwa na maana yeyote kwa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad?
2. Je Maalim Seif alifanya kosa kumueleza Lipumba kwamba asubiri mashauriano na wanasheria?
3. Je Maalim Seif alifanya kosa kutomjibu Lipumba barua yake?

COUNTER:

1]. Barua ya Lipumba haikuwa na maana na athari yeyote kwa sababu ilikuwa kinyume na matakwa ya Katiba ya CUF kupelekwa kwa Katibu Mkuu. Katiba imeelekeza kuwa Katibu Mkuu atapokea barua ya KUJIUZULU. Katiba haikuelekeza kwamba Katibu Mkuu pia anapaswa KUPOKEA BARUA YA KUTENGUA KUJIUZULU kutoka kwa Kiongozi Aliyejiuzulu. Katibu Mkuu hakuwa na [Constitutional Backup/Grounds]

2]. Je Maalim alifanya kosa. Hapana. Hakufanya kosa. Pia, swali hili lilijibiwa vizuri na Masoud Bin Kipanya katika 360Clouds TV. CUF ni Taasisi lazima iendeshwe kwa mujibu wa Sheria na Katiba, Maalim Seif akiwa Kiongozi Makini asingeweza kukurupuka na majibu kutoka mfukoni mwake.
LI.jpeg

Pichani ni siku ya uzinduzi wa manifesto ya CUF 2010 mbele ya waandishi wa habari Peacock Hotel.

3]. Je ni kosa kutojibiwa barua hiyo? Hakuna kosa lolote kwa sababu barua yake iko nje ya utaratibu wa Katiba ya CUF, alishaacha kutekeleza majukumu yake na kuondoka ofisini. Lakini pia Maamuzi si ya Katibu Mkuu [Maalim Seif] ni ya Taasisi chini ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ambalo lilishapokea taarifa ya kujiuzulu kwake. Vinginevyo tuamini kuwa Lipumba alikuwa anafanya mchezo wa ku-beep’ kujiuzulu. Ndio nakumbuka nasaha za Juma Duni Haji alipo mnasihi Lipumba kwa kumwambia “Mtu mzima hafanyi maamuzi kwa kughadhibika” Aidha, kualikwa na kuhuduria kwa Lipumba katika kikao cha Baraza Kuu na kuongozwa na Mwenyekiti asiyokuwa yeye ilikuwa ni majibu tosha kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu umeheshimiwa.

QUESTION NUMBER 14:

Je Barua ya Lipumba kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti haijafanyiwa kazi yoyote na Chama baada ya kupokelewa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad?

COUNTER:

Barua ya Kujiuzulu Lipumba iliwasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa Taarifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililohudhuriwa na Wajumbe zaidi ya asilimia 95% akiwemo Magdalena Sakaya, Abdul Kambaya, Masoud Muhina, Thomas Malima, Kapasha Kapasha wajumbe hawa kwa maslahi yao binafsi wamegeuka na kukana maamuzi waliyoyafanya. Baraza Kuu hilo lilipokea taarifa ya Kujiuzulu Lipumba na kwa kauli moja waliazimia KUUNDA KAMATI YA UONGOZI YA TAIFA kwa mujibu wa Ibara ya 101(1) ya Katiba ya CUF. Kamati hiyo ya wajumbe watatu iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Twaha Issa Taslima.

QUESTION NUMBER 15:

Je Maalim Seif ana chuki binafsi dhidi ya Lipumba?

COUNTER:

Hapana. Hakuna mtu ndani ya CUF aliyekuwa anamuheshimu Lipumba kama Maalim Seif Sharif Hamad. Hata kabla hajajiuzulu alimfuata nyumbani kwake na kumsisitiza na kumrai asichukue maamuzi hayo. Na kama kuna kosa lolote limefanyika basi wasameheane. Pamoja na Lipumba kukataa. Maalim aliendelea kusisitiza Lipumba aheshimiwe kwa mchango wake ndani ya Chama na alikuwa anapatiwa huduma zote alizokuwa anahitaji hali ya kuwa si mwenyekiti wa CUF. Ikiwemo kualikwa kwenye vikao vya Baraza Kuu nk.

LIPUMBA AMEHARIBU WAPI NA KUPELEKEA KUTOAMINIWA TENA NA MAALIM SEIF, WANACUF NA WAPENDA MABADILIKO NCHINI?

a) Lipumba kuanzisha kundi ndani ya CUF kwa lengo la kuwagawa wanaCUF na kuacha kufanya mashauriano na Hierarchy’ rasmi ya Chama, na badala yake kuwakumbatia watoto wadogo wenye maono finyu waliosababisha kumyumbisha na KUJIYUMBISHA MWENYEWE na hatimaye kuingia porini [kujivunjia heshima yake].

b) Lipumba kushirikiana na ‘matawi ya serikali ya CCM’ –‘System’ kwa lugha ya Masoud Kipanya – ‘Governmental Branches’ kwa malengo maovu dhidi ya CUF na viongozi wake, ili kufikia malengo aliyokusudia na kujinufaisha binafsi. Lipumba ameacha kuangalia maslahi Mapana ya Taasisi.

c) Kutoa tuhuma za urongo dhidi ya Maalim Seif na viongozi wengine ndani ya CUF.

d) Kusaliti na kuyakana maamuzi yake na au ya vikao vya Chama pale alipokuwa Mwenyekiti wa CUF.

e) Kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu na kuharibu taswira ya Chama na viongozi wake kwa kushirikiana na magenge ya wahuni, kuridhia kushambuliwa, kutukana na kudhalilishwa kwa wanachama na viongozi.

f) Kwenda kinyume na malengo na dhamira ya Chama cha CUF ya kusimamia na kupigania ukombozi wa Watanzania kwa hali na mali na nia ya dhati kutoka moyoni.

g) Kuhujumu Juhudi za kuleta Mabadiliko nchini kwa kuisaidia CCM ishinde uchaguzi na kusapoti sera mbovu za Uchumi na za Kisiasa zinazosimamiwa na serikali ya awamu ya Tano zenye kukandamiza mfumo wa Demokrasia na kuendelea kuwakandamiza Watanzania Bara na Visiwani. nk. Mifano juu ya kadhia hizi (a-g) ni mingi.

Ni yepi madhara alizozisababisha Lipumba na genge lake kwa Taasisi ya CUF, Tangu afanye uvamizi wa Ofisi Kuu, Buguruni Tarehe 24/9/2016? Usikose kufuatilia mfululizo wa makala hizi, mengi usiyoyajua, utayajua kupitia ukurasa huu.

ITAENDELEA SEHEMU YA NNE………….

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Maharagande,
DECEMBER 30, 2017

Majibu ndani ya Katiba CUF kuhusu Mgogoro ndani ya CUF. Lipumba amulikwa

Lipumba alipaswa kufanya nini ili kurejea katika nafasi ya Uenyekiti? Sehemu ya Pili
 
View attachment 663359

Kipanya ndiye rejea?!
 
Msitutoe kwenye agenda ya kufungia mwaka.
Apige tu-pushapu,abinuke sarakasi,acheze wushu,apige vigelegele lakini mwisho "ATUBU"!
 
Back
Top Bottom