Je Kwenda JKT baada ya form6 imerudi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Kwenda JKT baada ya form6 imerudi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donn, Jul 10, 2012.

 1. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,451
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nimepata tetesi kuwa mwaka 2013 wahitimu wa form 6 katika shule kongwe watatakiwa kwenda JKT, Je hili ni kweli?

  Na je, ni lazima ama hiari kujiunga?
   
 2. The_Emperor

  The_Emperor JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 884
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  razima kutemberea jeshi,hatutaki vijana wauza sura na masharobaro mashoga.tunataka hiri rinchi riwe ra kina marwa,chacha...
   
 3. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WABUNGE vijana walioko katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapaswa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Mujibu wa Sheria kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2012/13.
  Waziri wa Ulinzi na JKT, Shamsi Vuai Nahodha alisema hayo alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya wizara yake bungeni jana. Alisema wabunge vijana watakuwa sehemu ya kundi la kwanza la vijana 5,000 katika mafunzo yatakayoanza Machi, mwakani.

  Alisema wizara hiyo imelifanyia kazi ombi la kuandaa mafunzo ya JKT kwa wabunge vijana kama ilivyoombwa mwaka jana na kwamba wabunge hao wameandaliwa mafunzo hayo ya wiki tatu.
  "Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Wizara yangu imelifanyia kazi ombi hilo na kuandaa utaratibu wa mafunzo maalumu ya wiki tatu kwa waheshimiwa wabunge vijana," alisema Nahodha na kuongeza:

  "Kwa hiyo wabunge vijana wataungana na kundi la kwanza la vijana 5,000 niliowaeleza hapo juu… naomba waheshimiwa wabunge mjiorodheshe kwa maandalizi ya mafunzo haya."
  Waziri Nahodha alisema ni imani yake kuwa, pamoja na wabunge kunufaika na mafunzo hayo, watahamasisha urejeshwaji wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na kutoa taswira nzuri ya mafunzo hayo kwa jamii.

  Alisema JKT tayari imefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kambi tano zenye uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja zimeshaandaliwa kwa ajili hiyo.
  Alizitaja kambi hizo kuwa ni Bulombora na Kanembwa za mkoani Kigoma, Mlale ya Ruvuma, Msange mkoani Tabora na Oljoro hukoArusha.

  Hata hivyo, alisema gharama ya kuendesha mafunzo hayo ni kubwa hivyo JKT haitaweza kuchukua vijana wote na ndiyo maana imeamua kuanza na hao 5,000.  "Vijana hao ni miongoni mwa vijana 41,348 ambao watahitimu mafunzo ya kidato cha sita katika mwaka 2013," alisema Nahodha.
   
 4. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  eeh waende.. Wakanyoshe viungo.. Waje kulitumikia taifa kiukweli.. Sio kivivu na kifisad
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  wanafikiri wakiwapeleka huko ndio wataipenda ccm!!!!wasiwasi wangu wasitumie intelijensia yao kuwaumiza kwa mazoezi makali wenye mapenzi na upinzani ili washindwe kumaliza mafunzo...
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,590
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu jamani kwani BAJETI haitoshi wataanza na watu 5,000, Mwakani.
   
 7. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa wakati ule ukimwi ulikuwa kidogo sana, lakini Vd zilikuwa nyingi, uzinzi ilitawala sana, sijui kama hii kitu inamaslahi kwa vijana. Labda hawa maafande wahasiwe kwanza. Mwananyanya atakuja, nataka niwe afande wake.
   
 8. C

  CAY JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mnataka kupandikiza uccm kwa vijana eeh?
   
 9. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Na ukimwi kwa wingi sana. naongea kutokana na experince. Labda haya makambo yasiwe Co.
   
 10. D

  Dabudee Senior Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  "Those who receive this priviledge therefore, have a duty to repay the sacrifice that others have made. They are like a man who was given all the food in a starving village inorder that he may have strength to bring back supplies from a distant place.

  If he takes all the food and brings no help to his brothers, he is a traitor. Similarly, if any of our young men and women, who are being educated by the people of this republic, adopt an attitude of superirity, or fail to use their education to help the development of this country, they are betraying our union."-J.K.Nyerere DOES IT STILL STAND TRUE TODAY?
   
Loading...