Je kweli huyu bi dada atanilipa Deni langu ?

Je kweli huyu bi dada atanilipa Deni langu ?

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,198
Huyu bi dada nilikutana nae shoping wakati niko pale naangalia baadhi ya nguo.

Haikuwa mara ya kwanza kuonana nae la hasha,nilishawahi kuonana nae zaidi ya mara moja kwa sababu tuko tunatokea Eneo moja.

Sasa wakati yupo anaangalia angalia nguo zitakazomfaa akaona seti ya pichu pembeni rangi ya pink na nyeupe akazitamani lakini wakati anaulizia bei hela aliyokuwa nayo ilikuwa pungufu kama elfu kadhaa ili iweze kutosha kununua zile pichu( vifuniko vya Asali).

Bila hiyana kwa sababu ananifahamu akaniomba bwana shemu naomba nikopee niongezee hapa then nipe namba yako nikirudi nyumbani nitakutumia kwa M-Pesa.

Kwa moyo wangu wa Huruma nilimpa ile hela na namba nikampa akanibip fresh.

Sasa jioni ilivyofika nilichokuwa naona ni sms tu.
Mara shemu mambo vipi.
Vipi umelala .
Shemu umekula nini?
Shemu msalimie wifi yangu.


Nilikuwa namjibu sawa lakini katika Meseji zote hizo sijaona sms ya kuthibitisha muamala wangu wa M-Pesa mpaka ile siku kunakucha.

Siku ya pili ikawa vile vile na sms zake ,ya tatu pia sasa hivi wiki imeisha sijaona hiyo sms ya kuthibisha muamala wangu.

Sasa cha kushangaza jana jioni kanitumia sms kwamba ,
"Shemu naomba kesho nije nikutembelee yaani leo akamalizia na nimekumisi sana ".

Mi nilichomjibu ni sawa unataka kuja saa ngapi?

Akajibu muda wowote unaotaka nitakuja mi niko free.

Nimemjibu aje saa 2 usiku na kasema ok.

asubuhi leo nimeamka akanisalimia fresh mchana pia na muda si mrefu kanicheki kwamba nisimuangushe yeye ndio anajiandaa muda ukifika aje.


Sasa hapo nipo nawaza ndio anakuja kunilipa hela yangu cash ina maana mtandao kwenye M-Pesa kwake unasumbua?

Pia sio vibaya nimeshafanya usafi wa geto pako fresh lakini bado najiuliza je kweli atanilipa deni langu.?


IMG-20180918-WA0019.jpeg
 
Back
Top Bottom