Habari wanajukwaa poleni n'a majukumu lengo langu niombe ushauri kwenu kuhusu utaratibu wa uhamisho. Mimi ni mwalimu secondary nilivamiwa n'a kupigwa n'a mtu ambae ninamfahamu nikaumizwa Sana nilienda kuripoti polisi n'a kupewa p3 nikapatiwa matibabu Hali yangu kiafya imeimarika kidogo tatizo ni kwamba taratibu za kumkamata muhusika zimeshindikana n'a mhusika anaendelea kutoa vitisho vya kukatiza uhai wangu kwa njia ya sms. Tatizo ni kwamba mtu huyo anarekodi mbaya za uhalifu n'a bado hajakamatwa."je naweza kutumia kigezo hicho kuhama n'a je taratibu zinasemaje. Ah asanteni